Ninavyoimudu ndoa ya Wake Wawili

Ninavyoimudu ndoa ya Wake Wawili

Makanisa ya sasa duniani ukiwa na mke zaidi ya mmoja unatengwa fasta! Ila ukiwa changudoa au shoga wala hutengwi! Yaani wanavyochukia polygamy sijui imewakosea nini wakati manabii kibao hadi walioongea ana kwa ana na Mungu walikuwa na wake zaidi ya mmoja na Mungu hakuwahi kuwaambia marufuku! Hawa ambao hata sauti ya malaika hawaijui ndiyo wanapiga vita polygamy, ushoga ambao Mungu hakuwahi kuhalalisha na alichoma moto mji mzima ndiyo tunaambiwa tuwavumilie tuwa tolorate ila polygamists tuwatenge!
Mimi pia huwa siwaelewi kabisa kwa hili. Wanaipinga polygamy kuliko hata kuchepuka nje
 
Siamini katika mgawano wa mapenzi..ila ni vyema kujichagulia kinachokupa furaha na amani kuliko kua mnafiki

Ukiongeza watatu ulete mrejesho mkuu

Kila la kheri
 
hebu
Umechagua fungu jema, kuna watu wanakomaa na mke mmoja na michepuko lukuki ukimwambia si uoe tu mke wa pili utasikia mimi mkristo dini hairuhusu, nyambaf dini hairuhusu kuwa na wake wawili ila kuchepuka inaruhusu? Am sorry ila sie kina Bwana asifiwe tuna unafiki mwingi sana, yaani furaha yetu tuonekane mbele ya jamii kuwa tu wakristo ila matendo ya kikristo hatuyaishi kabisa.
hebu chunguza vizur kati ya hao wenye mke mmoja na wenye wake wengi ni wepi wachepukaji konki. acheni kuhusisha mambo ya Mungu na tamaa zanu wenyewe, huyu mwenyewe sio mkristo hakuna mkristo wa design hio.
 
Huu uzi ukiutafakari unaona uko na ajenda pana ndani yake (upotoshaji) nikusahihishe
- kanisani hukushikwa shati kwenda kutoa sadaka ungekua unakaa tu na hakuna mtu anaekulazimisha na pia kwa taarifa yako kanisa halikua linategemea sadaka yako
- kanisani huzuiwi kuoa wanawake wengi ila unafundishwa maandiko ni maamuzi yako kuyafuata ama kuyaacha
-hizo ni tamaa zako tu, nina mke mmoja miaka 3 sasa na sijawahi kuchepuka na wala sitawahi kuchepuka
- mtu hujalibiwa kwa tamaa zake
-hulazimishwi kuwa mkristo ni maamuzi yako unaweza hata kuwa muislam na hakuna atakae kufuata.
-huu uzi upo kwa lengo la kuipotosha imani ya kikristo maana ninaamini ni wewe mbwa mwitu aliejivika ngozi ya kondoo
 
Baada ya utangulizi hapo juu leo nitatoa mrejesho wa mada tajwa.


Mimi niko na wake wawili na ninawapenda wote equally. Ilikuwa kazi ngumu sana kwangu kuanza maisha mapya, kwanza ndugu walianza maneno yao mengi tu na ifahamike nimetokea familia ya kikristo. Sikumsikiliza hata mmoja wao, nilikaa na my wife nikaongea nae kwa undani zaidi akakubali japo kwa mbinde.

Suala lililofuate nikatengwa church nikasema sasa ndio mmenipa amani nilikuwa natafuta sababu ya kutokuhudhuria mana sikuona lolote la msingi zaidi ya sadaka 9 kila jumapili. Na sasa si muamini, bali ni free man, nalo jitahidi kufanya kuonyesha upendo na kuwa social tu thats all. Naenda misibani, naona wagonjwa, kama kuna jirani anahitaji msaada na niko na uwezo nafanya. Dini im sorry i was once a slave. Note: Naamini uwepo wa Mungu turejee kwenye mada.

Mke mdogo amepewa siku 3, mke mkubwa siku 4 (protocol). Ila incase nitahitajika mahali popote na sio siku ya kwenda huko lazima niende ila namtaarifu wa upande wa pili. Mara nyingi kama naenda kwa bibi mdogo siku hyo nikitoka kwenye mihangaiko napitia kwa bibi mkubwanapiga nae story mbili tatu naondoka.

Nacho shukuru wote wanaelewana hawana shida. Na nimeongea nao wote wawili nawajengea nyumba sehemu moja viwanja vimepakana ila nitaweka fensi.Sheria yangu ni moja: Yeyote atakae choka anaruhusiwa kuomba taraka nitampa muda wowote akitaka. But so far, tuko vizuri na tuna miaka 3 sasa.

Ndugu zanguni, tuache hizi mbwembwe za dini za mafalisayo. Babu yangu mimi Guzman_ alikuwa na wake 6 leo mfarisayo amatokea sijui wapi anasema dhambi nasisi kama mazuzu tunasema sawa, na anaenda mbali zaidi kuwa dini zenu ni ushenzi tunakubali, ukijenga kaburi la babu yako ni dhambi kubwa sana, ukienda kutambika upate baraka unaabudu mizimu tukasema sawa.

Alivo maliza sasa wanaanza kusema watu weusi ni mikosi. Hakia nani sisi kweli ni mikosi na wenda wazimu na wakati wakitubagua kwa rangi zetu sisi tunabaguana kwa dini zetu tena zile tumeletewa. Sijui kama kuna mtu anaelewa hapa.
Mkuu sikushauri uwaweke sehemu moja, wanawake hawajawahi kupendana kamwe, usione wanachekeana, watakuja kufanyiana mambo hutoamini macho yako... Nna ushuhuda wa hili nalokwambia... Miaka fulani zamani kidogo rafiki yangu alifanya hicho unachokisema na aliamini hivyo unavyoamini, siku moja Bi mdogo akiwa mjamzito, wakiwa wanaongea kwa Furaha tu na Bi Mkubwa, Bi Mkubwa akachemsha maji kisha ghafla akamwagia Bi mdogo, yeye na mimba yake alifariki baada ya siku 2.
 
Umechagua fungu jema, kuna watu wanakomaa na mke mmoja na michepuko lukuki ukimwambia si uoe tu mke wa pili utasikia mimi mkristo dini hairuhusu, nyambaf dini hairuhusu kuwa na wake wawili ila kuchepuka inaruhusu? Am sorry ila sie kina Bwana asifiwe tuna unafiki mwingi sana, yaani furaha yetu tuonekane mbele ya jamii kuwa tu wakristo ila matendo ya kikristo hatuyaishi kabisa.
Ona msadukayo huyu umeandika ugolo tu, wewe utaweza kushea rungu wewe?
 
Makanisa ya sasa duniani ukiwa na mke zaidi ya mmoja unatengwa fasta! Ila ukiwa changudoa au shoga wala hutengwi! Yaani wanavyochukia polygamy sijui imewakosea nini wakati manabii kibao hadi walioongea ana kwa ana na Mungu walikuwa na wake zaidi ya mmoja na Mungu hakuwahi kuwaambia marufuku! Hawa ambao hata sauti ya malaika hawaijui ndiyo wanapiga vita polygamy, ushoga ambao Mungu hakuwahi kuhalalisha na alichoma moto mji mzima ndiyo tunaambiwa tuwavumilie tuwa tolorate ila polygamists tuwatenge!
If you don't know something you better ask na sio kuongea blah blah blah za kilevi levi
 
Duuuh ngoja ngalatia niongezee mmoja mana hakuna namna kuacha kuchepuka kugumu
Umechagua fungu jema, kuna watu wanakomaa na mke mmoja na michepuko lukuki ukimwambia si uoe tu mke wa pili utasikia mimi mkristo dini hairuhusu, nyambaf dini hairuhusu kuwa na wake wawili ila kuchepuka inaruhusu? Am sorry ila sie kina Bwana asifiwe tuna unafiki mwingi sana, yaani furaha yetu tuonekane mbele ya jamii kuwa tu wakristo ila matendo ya kikristo hatuyaishi kabisa.
 
Yaani wake wawili tu tena miaka mitatu tu unakuja kutamba mbele za wanaume, hata watoto bado kupatikana tayari unajigamba eti umewamudu.... bure kabisa.
 
umeongea point kubwa sana.hakuna mahali katika dini zote mungu amekataza usioe wake wawili au zaidi

Sio lazima Mungu aseme kila kitu ndio iwe katazo au ruhusa. Vitu vingine wewe mwanadamu unajiongeza na ndio maana umeumbwa special sana( KWA SURA NA MFANO WA MUNGU) na umepewa utashi.

Kama Mungu alimuumba Adam akampa Eva awe mke wake unashindwa vipi kujiongeza hapo na kuona kwamba mke ni mmoja tu? Haihitaji Mungu aseme hapo

Tamaa na uzinzi ndio vinatufanya tuhangaike, mara wake wawili mara wake wanne mara michepuko. Kwani huyo mke wa 2 anakupa kitu gani special ambacho mke wa 1 hakupi?

TAFAKARI
 
My freendiii acha kabisa huo mchezo...waislam wenyewe ishu za wake zaidi ya mmoja na wao wanapuguza siku hizi naona... usije amini hata siku moja kwamba mwanmake ana furaha kushare mb** na mwanamke mwengine.. we tarajia kitu kimoja tu...utakufa wewe au mmoja wao..bro watalogana tu ilhali hao sio dini yao kupokea hayo..na shida watapata watoto. Na pia hivi unadhani siku 4 au 3 za kuwa na mwanamke utamridhisha mkuu? We jua unasaidiwa tu... jikinge na magonjwa... halafu maisha yenyewe magumu unakidhi vipi mahitaji ya wanawake wawili? Kweli tamaa yako ya mwili imekufanya na uache kabisa hadi kuabudu? Kijana kifo chako Mungu atakifanya cha mfano. Rudi tubu kwa mwokozi wako...unalalamika kutoa sadaka 9 kwa Mungu wakati hulalamiki kujenga nyumba mbili kwa wanawake wawili? Leo matakwa ya binadamu mwenzako yako juu zaidi ya muumba wako anaekupa uhai? Doh ...nimetetemeka mzee....tutaja hadithia stori zako bwana Mungu atapofanya yake bro
 
Babu yangu Mzee Mbuna alikuwa ameoa wake watu kimila hali hii ikapelekea babu yangu Mdogo Francis akose kusomea upadri kwa sababu alikuwa analelewa na huyu babu yangu mimi hivyo kanisa lilimtenga babu mubwa na kupelekea huyu mdogo kokosa sifa ya kusomea upadri pale Kasita kwa wale wanaopajua Kohelanga ,Morogoro.

Katika wake zake watu kila mmoja alizaa mtoto mmoja kati yale watoto watatu wawili walisilimu wakawa waislamu ila mmoja mpaka leo yupo kwenye dini yake ya asili. Kati ya waliosilimu mmoja wapo ni baba yangu mzazi , babu yangu mdogo baada ya kusimamishwa ile shule ya upadri na yeye aliamua kusilimu hadi anafariki alikuwa muislamu na alikuwa ameoa wake wawili.

Mila zetu zilikuwa nzuri sana tulikuwa hatuna limitation kwenye issue za kuoa bahati mbaya hawa waliojipa utakatifu na kuita mila(dini zetu za asili) zetu ni ushenzi wametufikisha hapa tulipo leo.

Tunachukiana na kubaguana kisa dini iliyoletwa na eidha mzungu au mwarabu.
 
Back
Top Bottom