Car4Sale Ninauza gari yangu PASSO namba DPD

Thaconfession

JF-Expert Member
Jun 16, 2021
295
575
Kwa mwenye uhitaji wa gari hii hapa,
Aina ya gari: Passo,
Piston 3,
CC 990

Gari ipo Dar es salaam, ukitaka kuiona nipigie kwa namba 0686866276

Nimeitumia kwa bolt na Uber kuanzia mwezi July mpaka sasa, naamua kuuza baada ya kupata scholarship nchini Denmark.

Kwa mwenye muda na yupo serious na biashara ya "tax mtandao" hakika na aifanye, pamoja na changamoto za hapa na pale, lakini inalipa sana.

Kwa atakayekuwa tayari kufanya biashara hii nitamwelekeza namna ya kufanya.

Bei ya gari hii ni Milioni 4.3 bila punguzo!

Wanunuzi serious, karibuni sanaaa...gari haina dalali, ni yangu mwenyewe!

IMG_20230413_163636_514.jpg
IMG_20230413_163604_329.jpg
IMG_20230413_163619_453.jpg
 
Kwa wale mnaodharau passo poleni sana. Ninayo yangu ni DRG nikitokea kwenye ingine ambayo ilikuwa DHF hizi gari nimezipenda sababu ulaji wwke wa mafuta.kwa wiki huwa natembea sio chini ya 700km na hii ni kila week.

Ningekuww na gari kubwa nisingetoboa. Huwa naweza kutembea nayo 1300km non stop kila baada ya miezi 3 ama 4 na haijawahi kunisumbua hata siku moja.

Hii ya mwisho nlinunua ikiwa na 30000km na sasa ina zaidi ya laki moja and bado ina hali nzuri sana kama hii yako. Still naezauza hata kwa 6miln
 
Kwa wale mnaodharau passo poleni sana. Ninayo yangu ni DRG nikitokea kwenye ingine ambayo ilikuwa DHF hizi gari nimezipenda sababu ulaji wwke wa mafuta...
Watu wengi humu wanajikweza kuliko uwezo wao, kila mtu anajifanya kumiliki gari nzito nzito, VX, V8, BENZ VANGUARD N.K Lakini ktk uhalisia wengi wao wanagombania daladala mitaani.

Passo sio gari mbaya, kwa pilika za utafutaji mjini ni very perfect!
 
Watu wengi humu wanajikweza kuliko uwezo wao, kila mtu anajifanya kumiliki gari nzito nzito, VX, V8, BENZ VANGUARD N.K Lakini ktk uhalisia wengi wao wanagombania daladala mitaani...

Passo sio gari mbaya, kwa pilika za utafutaji mjini ni very perfect!
Unakuta mtu ana harrier new model, vanguard ila ana print sababu hawezi kulitumia sana linalamba wese. Mimi hata mabasi nishaacha kupanda, ikitokea huwa najiona nimeteseka sana
 
Sorry kama nitakua tofauti na wewe,, kama unavyosema Uba na Bolt inalipa kwanini badala ya kuiuza utafute kijana umpe mkataba kwanza hii itakupa zaidi ya m8 ndani ya 2yrs pekee badala ya hiyo m4 na labda ukaambulia m3 tu
Hii usithubutu kufanya kwa vijana wa Tanzania, ukiwepo tu wanasumbua (Nina uzoefu mzuri kwenye hili) kwa hiyo kumuachia mtu gari bila uaimamizi wowote ni Sawa na kuamua kuitupa kabisa!

Nilifanya mwenyewe kwa hyo miezi mitatu, mwezi July nilipata 1,270,000/= mwezi August nimepata 1,407,000/= na September (mpaka jana) nimepata 1,075,000/=
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom