Ninauchukia sana ujana

Ninauchukia sana ujana

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
19,371
Reaction score
14,481
Wakuu Hbr za asubuhi...!!!, Km heading inavyojieleza, Mimi pia ni Kijana, nimekaa chini nikatafakari namna Hatua hii ya Ukuaji wa Mwanadamu inavyozua Majanga mengi.

Kutokana na Mihemko ya Mwili na Damu kuchemka Vijana Wengi tunajikuta tunaangukia pabaya hasa ktk Majanga mazito km vile Uzinzi, Ulevi wa kupindukia, Matumizi ya madawa ya kulevya, Matumizi mabaya ya pesa, n.k.Hali hii inatufanya Vijana Wengi tujitenge mbali sana na Uso wa MUNGU wetu aliyetuumba.

Binafsi Bora ningebaki tu kuwa mtoto asiyejua lolote au Bora niuingie Uzee nikatulia, Nampenda sana MUNGU Wangu Ila Tatizo ni Ujana, Hakika ninakuchukia sana Ujana kwasababu umenifanya niwe mbali na MUNGU wangu kwasababu ya Mihemko yako.

Ee MUNGU nisaidie nikupende na nikutii daima, lkn niendelee kuuchukia Ujana ambao unawatenga watu na Uso wako Mtakatifu.
 
Ni kujitambua tu bro.

Kuna vijana sio wazinzi, walevi na wanamtumikia MUNGU vema.
Amina. Ndio maana Nimesema nauchukia Ujana unaowatenga watu na Uso wa MUNGU. M.y ni kwamba Naupenda Ujana unaowaleta watu kwa MUNGU.
 
Amina. Ndio maana Nimesema nauchukia Ujana unaowatenga watu na Uso wa MUNGU. M.y ni kwamba Naupenda Ujana unaowaleta watu kwa MUNGU.
Biblia yenye kuna sehemu imesema "Fahari ya kijana ni nguvu zake "

So... Nguvu tu hii ya ujana bro ndo inaletaa mabalaa yote hayo.
 
Mathayo 6:24-26

"Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili,kwasababu ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine,au atamthamini mmoja na kudharau mwingine.huwezi kumtumikia mungu na Mali."
 
Biblia yenye kuna sehemu imesema "Fahari ya kijana ni nguvu zake "

So... Nguvu tu hii ya ujana bro ndo inaletaa mabalaa yote hayo.
Sure!!, Yaani Ujana ni maji ya moto.
 
Tabia ni kama ngozi haibadilikia kama ujanani mwako ulikua mzinzi,mvuta bangi,mtumia pombe,mpka uzeeni huwez kuacha
 
Mathayo 6:24-26

"Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili,kwasababu ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine,au atamthamini mmoja na kudharau mwingine.huwezi kumtumikia mungu na Mali."
Amina. Hapo dawa ni kuuchukia Ujana na kumpenda MUNGU.
 
Mjukuu wangu jitahidi utayashinda, uzee kazi sanaaa
Siku si nying hamtaniona Jf maana macho yameanza kufifia na vidole vinapishana kwenye keyboard,
Maombi yenu yanahitajika Sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom