Uongozi unaowajibika ni mhimili imara katika mapambano dhidi ya changamoto zinazotukabili

The Festival

Member
Aug 30, 2021
27
98
Habari za muda huu popote pale ulipo. Ni matumaini yangu sote ni wazima wa afya, ama kwa yule aliepatwa na mtihani wa maradhi tunamuombea shifaa apone haraka kwa idhini ya aliyetuumba.

Moja kwa moja kwenye neno. Kumekua na kukosoa pale mambo yasipoeleweka, kupongeza pale mambo yanapoenda sawa, na hata kulaumu pale mambo yanapoenda kombo. Mbali na hivyo, kuna mambo mengi sana yanahitaji ufumbuzi, mfano tatizo la ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei za bidhaa nchini. Ukiuliza jibu fupi ni vita ya Russia 🇷🇺 na Ukraine 🇺🇦. Lakini haya mambo yalikuwepo mda sana.

Ukiuliza utaambiwa madhara ya Covid19. Lakini Covid ilianza hapo 19 & 20, utaambiwa haya ni matatizo ya kilimwengu, kwa maana ya kwamba duniani kote kuna tatizo la ajira na bei za bidhaa hazipo chini, tena afadhali kwetu ni nafuu. Lakini kila kitu kina kiwango, sawa dunia nzima mbona hizo neema nyengine za duniani huku hakuna na rasilimali tumebarikiwa za kutosha, sisi tumekua ni kufanana shida za kilimwengu tu. Jibu la kueleweka ni nadra kulipata. Hapa tunapata picha kwamba hatuwezi kumlaumu mtu fulani au kikundi cha watu fulani kwa haya yote yanayotokea.

Mimi mwandishi ni muumini mzuri wa kuamini makadirio ya Muumba wetu, yani alichotaka huwa. Sasa haya yote Muumba wetu alitaka yawe ndio yakawa. Lakini yeye ndiye aliyetupa uwezo wa kufanya maamuzi kwa ajili ya dunia na akhera yetu. Hivyo, hakuna wakumlaumu kwa khasara tunazopata. Ametujaalia neema ya rasilimali chungu nzima basi ni haki yetu kushukuru kwa kuzitumia vizuri na tusipo tumia vizuri tutakua watumwa wa wale wanaotumia vizuri vile walivyo barikiwa.

Tumepewa ardhi yenye rutuba, bahari, maziwa, mito, misitu, madini, gesi, n.k. Mbali na hayo, tumepewa akili ya kutafakari na kuchanganua mambo, lakini tunafeli wapi? Sitatoa lawama kwa mtu mmoja mmoja, bali nitatoa uchambuzi wa wapi tunajikwaa. Kabla sijazungumza zaidi juu ya kile nilichanuia kukisema, kwanza ninaomba ieleweke silaumu, sikosoi, wala sisifii, bali tunachambua tu kama karanga. Na uchambuzi utabase zaidi kwenye baadhi ya changamoto zinazotukabili, hususani suala la uwajibikaji na tatizo la ugumu wa ajira.

Kwanza kabisa, nianze kwa kusema uongozi unaowajibika ni muhimili imara katika mapambano dhini ya changamoto zinazotukabili. Sasa basi, mchango wangu utajikita zaidi kwenye aina ya uongozi unaohitajika ili tujikwamue. Angalizo, uchambuzi huu si wakukosoa serikali, wala kupiga kampeni ya nani anafaa nani hafai bali ni uchambuzi tu kama uchambuzi wa mchele, ahsante. Nitataja vipengele muhimu ambavyo viongozi wa nchi hii wanapaswa kuvizingatia ili mambo yalainike kwa idhini ya aliyetuumba.

1. Proactive: Hapa ni kugusia jambo zima la kua ni mwenye maono ya mbali, kutizama yajayo yatakuaje kutoka na maamuzi fulani. Uongozi imara ni ule ambao upo "Proactive", yani upo makini na maamuzi na unatazama mbali kabla na baada ya maamuzi. Ni uongozi ambao hausubiri kushtuliwa nini kifanyike na nini kisifanyike. Mathalani wakati vita inatokea ya Russia na Ukraine, je viongozi waliweza kukaa chini na kutafakari madhara yake na kuchukua hatua stahiki? Au uongozi ulisubiri mambo yavurugike ndio uchukue hatua stahiki? Kama jibu halipo chanya kwa uongozi basi kuna mambo yanapaswa kubadilika.

Hivi sasa kuna tatizo la ajira si kwa vijana, si kwa watu wazima, si kwa wazee, wote mbombo ngafu. Je, uongozi umechukua hatua stahiki kudhibiti hali isiwe mbaya zaidi hapo baadae? Au kuwaambia vijana wajiajiri tu inatosha? Kama jibu ni hasi kwa maswali hayo basi mambo yabadilike. Hapa pia ningegusia swala moja, maamuzi mazuri kwa uongozi imara hua yanafanyiwa kazi kwa haraka. Nakumbuka kipindi fulani mwaka huu kuna kiongozi mmoja simjui jina lake kwa sababu sifuatilii sana siasa za bunge, alitoa maagizo kwa sekretarieti ya ajira nchini kuandaa na kueka mpango wa watahiniwa wa mchujo kufanya mitihani kikanda kwasababu za kupunguza adha ya gharama za muda na pesa kwa wananchi.

Ni kweli, maono yake ni sahihi kwani kuwakusanya Dodoma watahiniwa 1001 toka kigoma, mwanza, dar, mtwara, lindi, Zanzibar na maeneo mengine nchini kwa ajili ya nafasi 01 ni maamuzi dhaifu mno. Kwani watu wanapoteza nauli mara kwa mara huku probability ya kupata kazi ikiwa ni chini ya 0.1% (kiuhalisia). Wananchi na viongozi wengine walimpongeza sana kwa kuchangia points za maana. Cha ajabu tangu aliposema hayo, sijawahi sikia au kushuhudia watahiniwa wa ajira nchini wakitahiniwa kikanda. Je, wenye mamlaka hawapo "proactive" au yale maoni yalikua ni ya kisiasa zaidi?

2. Curious: Hapa sasa tunaangazia kuwa mchangamfu wa kufahamu nini kinaendelea katika jamii. Tatizo la ajira hapa nchini linaongezeka na kutojali yanayoendelea kunakoleza moto. Mfano, hivi karibuni Uber walifunga ofisi zao na Bolt walifunga kwa baadhi ya huduma, madereva waliojiajiri huko walilaza magari hatimae baadhi yao wamepokonywa magari na matajiri wao kwa kutopeleka hesabu yenye kueleweka. Uongozi imara ulipaswa kua curious and proactive simultaneously. Bundle za simu zimepanda sana kwa internet. Watu wanaingia mitandaoni kwa manati. Hebu tutizame watafiti wanasemaje kuhusu uhusiano wa matumizi ya internet na manunuzi ya wateja (sitafasiri kwasababu ya muda).

Ameandika Syed Akhter mwaka 2012, "The amount of time people spend using the Internet within a specific time period such as a week is referred to as online time. Research shows that as online time increases, people gain knowledge and feel comfortable in using the Internet for different purposes. The experience gained in using the Internet enhances perceived self-efficacy, which plays a determining role in influencing behavior such as online shopping and spending (Li and Chuan, 2010). Citrin et al. (2000) found that higher levels of Internet
usage positively influenced online shopping. Lohse et al. (2000) found that as online time increased, the probability of making an online purchase also increased. Online time significantly influenced online spending, as hypothesized. People who have had access to the Internet longer than others are more likely to spend more on online purchases.

Furthermore, people who spend more time online are also more likely to spend more money on online purchases. People who use the Internet for communication, entertainment, information acquisition, and education more than others are also more likely to spend more than others on online purchases. The findings are significant for firms that are investing in Internet infrastructure development, hoping to capitalize on the expected change in the buying behavior of consumers, especially with respect to developing a preference for making purchases online."

Sasa turudi nyumbani; kwa bundle hizi za 1500 mb 500 ni kwa wingi gani wateja wataspend more time online kutizama hata bidhaa za kununua? Jibu ni wachache sana na kwa muda mdogo sana. Sasa je, biashara hazijazoroteshwa hapo bado? Uongozi curious ni muhimu mnoo. Maisha yawe laini inapobidi, tusitie ugumu uso lazima kwenye mambo muhimu.

3. Flexible: Hapa tutizame uwezo wa kubadilika (flexibility). Uongozi imara unahitaji uweze kubadili maamuzi yasio sahihi pale yanapogundulika. Hatuwezi kuwalaumu sana binadamu wenzetu ambao ni viongozi kwa maamuzi mabovu kwani wao pia ni binadamu kama sisi, wanapatia na kukosea. Bali wanastahili kukosolewa kiheshima na staha pale wanapoyaganda maamuzi mabovu. Mathalani, watu wanalalamika tozo kuwa ni kikwazo, uongozi imara haupaswi kusema kua wananchi watazoea. Wasaka mirija ya asali wana lalamika Dodoma nauli zinaenda bure kufanya sahili, viongozi wanapaswa kukubali walifanya maamuzi ambayo si sahihi na wanapaswa waeke utaratibu mzuri sana ili wasaka ajira wote wawe na "equal chance" ya kutahiniwa si wale tu wenye uwezo wa kufika Dodoma kwa nauli na malazi kwa ajili ya usaili.

4. Life-Long-Learner: Hapa tutaangazia kutoridhika na uwezo mtu alionao. Uongozi imara ni ule unaohitaji kujifunza zaidi, kukubali kukosolewa, na kufanyia kazi mapendekezo ya kujenga . Sisemi mengi hapa, najua viongozi walioko bungeni na nafasi nyengine wanafahamu kua wao si wenye akili nyingi kuzidi wengine wasiokua wao kiasi wasikubali kujifunza.

5. Creative: Hapa ni kuwa na ubunifu. Uongozi imara ni ule ambao utakua na ubunifu katika kutatua matatizo ya wananchi wanao waongoza. Ubunifu si kubuni tozo tu, hapana. Kwani tozo haikatwi kwenye uzalishaji bali ni kwenye miamala ambayo hupelekea doubles taxation. Ubunifu unaohitajika ni katika ewekezaji, ubunifu katika sera, ubunifu katika kukuza sekta binafsi, ubunifu katika teknolojia, ubunifu katika utawala, n.k

Hitimisho: Tatizo la ajira ni ngumu mno kutatuliwa kwa ajira za serikali. Bali, sekta binafsi ndio zinaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kutatua tatizo hili. Sasa je, sekta binafsi nchini zinalelewa vizuri kukua au mazingira hayako sawa? Nini kifanyike? Yapi maoni yako. Naweka kalamu chini, Mungu atuongoze kwema!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom