Ninatarajia kumng'oa Evans Aveva Simba , ameshindwa uongozi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,745
239,401
Kiukweli hali ya simba ni ya kusikitisha mno ! Hatua za haraka zisipochukuliwa wanachama tutegemee aibu zaidi .

Kitendo cha jana Songea cha timu kulala kwenye hotel yenye kunguni na wachezaji kutumia usafiri wa bodaboda hakivumiliki na cha aibu.

Nimejitosa rasmi kumng'oa Aveva na kamati yake ya utendaji ili kuleta heshima msimbazi .

Wadau niungeni mkono .
 
mimi mwana Yanga na huwa naiombea simba mabaya ila sio kwa jambo kama hili,nifedhea na aibu kwa timu kama simba kufikia hatua hiyo simba SC ni brand yaani kivyovyote vile inastahili heshima zaidi,inahitaji watu makini wanaojua mpira sio wapiga deal wanaopenda kutmia mpira kwa biashara zao..nakuunga mkono kamng'oe aveva timu mpeni MO tutengeneze competition ya ukweli
 
Kwa huu mtindo mtu unategemea timu ifanye vizuri halafu yule msemaji wa klabu na uongozi ndo hawana dira kabisaa, yaani wanataka kutuaminisha kwamba kufanya kwao vibaya kumetokana na kuonewa na hawataki kukili makosa na mapungufu yaliyojitokeza na waliyoyafanya.msemaji anatumia mda mwingi kulalamika tuuuu kwamba wameonewa Mara amekejeliwa Mara sijui nini yana kiufupi hawana future wala plan yoyote ya maana. Miaka ya karibuni nimethitisha mi ni mvumilivu na ninaweza kuhimili magonjwa nyemelezi Kama magonjwa ya moyo maana huku Arsenal huku simba ni shida.
 
Back
Top Bottom