Ninasumbuliwa na chunusi usoni

RTI

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
2,423
7,124
Mimi ni kijana wa miaka 23, kwa miezi kama 7 hivi nimekuwa nikishambuliwa na chunusi na upele usoni.

Upele wenyewe ni mkubwa na nikiuminya yanatoa usaha. Nimejaribu kutumia sabuni na mafuta aina mbalimbali lakini yamekuwa yakipona alafu yajirudia tena.

Wadau ninaomba msaada ninawezaje kuondokana na tatizo hili?
 
RTI,
Aise pole niliwahi kushambuliwa pia kila aina ya sabuni nilitumia wapi. Vilikuja kuisha nilivyokuja Dar maana nilikuwa naishi mikoa ya baridi (Iringa na Mbeya).
 
Aise pole niliwahi kushambuliwa pia kila aina ya sabuni nilitumia wapi. Vilikuja kuisha nilivyokuja Dar maana nilikuwa naishi mikoa ya baridi(iringa na mbeya)
Kwa hiyo baada ya kuhamia Dar viliisha vyenyewe bila ya kitumia dawa yeyote?
 
Pole sana, ila jitahidi usitumbue utapata makovu ambayo itachukua muda kutoka usoni,
Kipindi nipo shule ilinisumbua sana
 
Tumia tube inaitwa Persol 5 itamaliza kabisa, inauzwa maduka ya dawa baridi Tsh.3500/= hadi 4,000/=
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Tumia Baby Vaseline husafisha makovu, asubuhi saa moja kabla ya kuoga paka mate(kabla hujapiga mswaki) husaidia kuivisha vichunusi vizuri na pia kabla ya kulala paka mate. Chunusi usiikamue kama haijaiva. Niushauri tu waweza jaribu.
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Back
Top Bottom