Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,842
- 3,618
Mkuu nakuunga mkono kabisa....nafsi yangu hainitumi kabisa nimpigie kura Lowassa ingawa nimeipenda chedema kwa mda mrefu sana....nashukuru leo nimepata jibu....kura yangu udiwami cdm, ubunge cdm uraisi nasikitika sana kwamba nitampigia magufuli....kwangu kibaya hiki ni afadhari kuliko lowassa
Kumbe tuko wengi wa mawazo haya. Mimi nimeshabikia na kusapoti NCCR na baadae chadema tangu 1992. Mwaka huu nilikuwa na matumaini makubwa sana na chadema, lakini siyo kupitia kwa Lowassa, huyu nimemkataa siku zote.
Kwa hiyo kura zangu 3 ni kama ifuatavyo:
Rais: John Magufuli (namkubali yeye binafsi, siyo CCM yake)
Mbunge: Julius Mtatiro (namkubali yeye binafsi, siyo CUF yake)
Diwani: Simjui jina (lakini naikubali Chadema, kwahiyo hii itaenda chadema).
Kumbe chadema ingeniwekea wagombea ninaowakubali kwa nafasi zote ningepiga kura kwa raha sana. Au Magufuli na Mtatiro wangekuwa chadema ingenoga sana (hata hivyo bado naona kwa misimamo yao wanafanana na kile ninachopendea chadema, kwahiyo watapata kura zangu kiroho safi kabisa).