Kapokee buku 7 zako Lumumba.... Ni wehu tu ndio wataichagua CCM
Utaweka kiraka saa ngapi maana hao wanaotakiwa kukiweka ndiyo tunaowachagua sasa, na kura yako ndiyo itakayoamua wawe wangapi wa upande upi? Na kutegemea ni wapi watakuwa wengi ndiyo hasa wataamua ikiwa wanapenda kuweka hicho kiraka.Kumbuka katiba yako ya sasa ni ya mwaka 1977...kipi kitazuia kuweka kiraka hicho?
Kwa nini usimpigie hata mbunge wa ACT-Wazalendo kama hakuna mgombea wa CUF?Hapana Abel.....bado nitampigia Magufuli. Lakini nataka kumpigia kura Kubenea jimbo la Ubungo. Nataka ikiwezekana wabunge wa CCM hapa DSM wawe walau watatu (3) tu. Wabunge wchache kama Filikunjombe nitafurahi wakirudi.
Ndoto yako siyo halisi maana Katiba yetu haituhusu hayo. Kumbuka kwa Katiba na mfumo wa sasa kura unayompigia rais pia inamwongezea mbunge wa viti maalum! Mabadiliko pekee yatakuja kwa kuanzia kubadilisha Katiba - na siyo hii iliyopendekezwa maana bado haina hayo mabadiliko unayoyaota
Viti Maalum vya Wabunge na Madiwani Wanawake.
Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum, umeelekezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 78, kifungu cha 86A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2010 chini ya Kanuni ya 67.
Kwa mujibu wa taratibu hizo, kila Chama cha Siasa kilichoshiriki katika Uchaguzi Mkuu ambacho kimepata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za Ubunge zilizopigwa, kitapendekeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi majina ya Wanawake kwa kuzingatia uwiano wa Kura ambazo kila Chama kimepata katika Uchaguzi wa Wabunge.
Vile vile kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 endapo itajitokeza kuwa katika Jimbo la Uchaguzi, Mgombea wa Chama amepita bila kupingwa, idadi ya Kura halali za Urais wa Chama cha Mgombea huyo kama Chama husika kimeweka Mgombea, ndizo zitatumika katika zoezi hilo la kupata uwiano. Endapo itatokea kuwa Chama husika hakikusimamisha Mgombea Urais, asilimia hamsini na moja (51%) ya Kura za watu wote waliojiandikisha Kupiga Kura katika Jimbo hilo zitatumika kwa madhumuni hayo ya kutafuta uwiano.
Wewe hukuona mtu wa kumpigia isipokuwa yule mnafik kubenea? Unasikitisha sana.
Option nzuri ya kulisaida Taifa ni kupigia kura UKAWA. Kwa kuwa tumefika hapa tulipo kwa sababu wabunge wa ccm ambao ndio wengi wanatetea serikali ambayo imeshindwa kuwatumikia wanabchi badala ya kuibana. Huyu JK anayezurura duniani na ambaye ndiye mwenyekiti wa chama ana nguvu ya kumshughulikia mbunge yeyote asiyelinda chama ndio maana mawaziri wanalala hawana wasi.
Kwa hiyo kuchagua Rais na Wabunge wa UKAWA litakuwa ni somo kuwa wananchi hawataki mchezo. Na ni muhimu ccm ipoteze kimojawapo ama vyote yaani Urais na/au idadi ya wabunge wengi. Kwa kuwa hatuna uhakika kipi kitatokea ni vyema kuchagua UKAWA kwenye Urais na Ubunge ili kimojawapo kitokee au vyote. Na ni wazi kuwa na wabunge wengi wa ccm upinzani hiyo serikali haitalala kwani watataka kurudi madarakani na nchi itafaidi.
Hapana Abel.....bado nitampigia Magufuli. Lakini nataka kumpigia kura Kubenea jimbo la Ubungo. Nataka ikiwezekana wabunge wa CCM hapa DSM wawe walau watatu (3) tu. Wabunge wchache kama Filikunjombe nitafurahi wakirudi.
Kwa nini usimpigie hata mbunge wa ACT-Wazalendo kama hakuna mgombea wa CUF?
Kubenea ni kati ya watu wanafiki sana katika nchi yetu.
Kubenea ni kati ya wabunge watakaokuwa wananunuliwa ili kutimiza matakwa ya watu wabinafsi.
Acha uhuni wewe, Naona Lumumba mnaleta staili mpya ya kupata kura za Magufuli. Naona ile ya Chagua Magufuli na si CCM imebuma, Haaa haaaa haaaa.
Sheria ya Uchaguzi haina maelezo hayo! Unaweza kuniwekea umeyapata wapi. hata hivvyo bado kwa vyama vingi kura za Rais ndiyo determinant za idadi ya viti maalumuKura za Urais haziongezi wabunge wa viti maalum.
Kura za wabunge ndiyo zinaongeza idadi ya wabunge wa viti maalum.
Sheria kuhusu viti maalum inasema hivi,
Kama unasema sheria ya uchaguzi haina maelezo hayo, ingekuwa ni vizuri ukayakataa maelezo kwa kuleta maelezo yanayokinzana.Sheria ya Uchaguzi haina maelezo hayo! Unaweza kuniwekea umeyapata wapi. hata hivvyo bado kwa vyama vingi kura za Rais ndiyo determinant za idadi ya viti maalumu