Ninaomba msaada wa kimawazo au ushauri wa kutatua changamoto ya usikivu mdogo (Hearing loss) au kupunguza adha zake

EP cosmetics

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
2,470
3,847
Habari za humu ndugu zangu.
Poleni kwa majukumu.

Changamoto inayonirudisha nyuma sana:
Ninachangamoto ya usikivu mdogo(Hard hearing, Hearing loss), kushindwa kuelewa kinachozungumzwa kwa kiasi fulani (Word deafness) hasa kwa sauti za besi sana sometime ninaweza nisikuelewe maneno utamkayo, watu wanaoongea kwa spidi sana au harakaharaka sana mara nyingi naweza nisielewe, au nikaelewa maneno ya mwanzo unapoanza kuongea, utakapoweka vituo na mwishoni tu unapomalizia, Sometime kuelewa utakachosema ni mpaka nikuface nitazame lips za mzungumzaji ndio ninaweza kuelewa maneno yote, Sehemu zenye kelele nyingi kama sokoni nk au tukiwa tunaongea huku kukiwa na sauti za labda tv, radio au sauti zingine zaidi (Background noises) tunaweza tusielewane kabisa (kukusikia nitakusikia vizuri tu ila sehemu kubwa ya speech sitakuelewa),

Kwa mfano ninaweza kuwa kanisani ambapo kuna vipaza sauti vingi tu na sauti ni kubwa sana ila nikikaa ndani nisielewe kitu na sehemu kubwa ya speech nikaipoteza lakini nikitoka na kukaa nje ya kanisa nikaelewa kila kitu na kila neno vizuri kabisa. Pia watu ambao wanaongea sauti ya chini sana mara nyingi siwasikii kabisa mfano mtu akiwa anaongea huku anatafuna labda chakula nk kumsikia nitamsikia vizuri tu ila kwa sehemu kubwa naweza nisimwelewe. (Auditory verbal agnosis)

Wakuu ni ngumu sana kwa wenye changamoto za masikio (Hard hearing) kuelezea hali zao mpaka kueleweka vyema kwa yanayowasibu (hasa kama hujawahi kuishi na mtu mwenye usikivu mdogo, Hearing loss) Hivyo nimejaribu kuelezea vyema hali yangu ya masikio na mazingira yanayonipa shida kumudu usikivu, natumaini kwa kiasi icho nilichojaribu kujielezea walau unaweza nielewa kidogo nini hasa ninachopitia.

Historia fupi ya hii changamoto:
ni takribani miaka 10 sasa tangu mwaka 2011 nimekuwa nikiishi na hali hii mpaka leo navoandika ivi sijafanikiwa kupata utatuzi wa changamoto yangu hii ya usikivu hafifu, changamoto hii ilianza kidogokidogo, nilianza kuitambua hasa na kujihisi usikivu unashuka nilipomaliza masomo yangu ya O-level mwaka 2011. (kiukweli mpaka sasa sijui chanzao cha changamoto hii wala sababu ya usikivu kushuka)

ikanibidi niendelee na masomo ya A-level na hali hii mpaka namaliza, Zaidi kuanzia Elimu ya degree ilinibidi niisome kwa nguvu nyingi na kupambana sana, Kiukweli Tangu level hii nimekuwa nikisoma kwa macho (kutazama) zaidi kuliko masikio (kusikiliza), kujifundisha na kujisomea mwenyewe vitabu ndio umekuwa msaada kwangu.

Tangu nilipogundua changamoto hii, nilianza kutafuta tiba kupitia clinics za masikio, hospitali ya aga ghan mara mbili, nikaenda muhimbili kote huko mwisho wa siku niliishia kupewa mashine za masikio (Analogy Hearing aids) bahati mbaya hazikunisaidia chochote hata nilipo jaribu kuzibadilisha sikufanikiwa kupata hata nafuu.

Mwaka 2018 nilienda bugando na kuishia kupata dozi ya vidonge vya "Neurobin" ambavyo nilitumia kwa muda wa miezi sita bila mafanikio yeyote baada ya dozi kuisha nikaambiwa nitafute Hearing machines, Mwaka 2019 mwishoni nilifanikiwa kupata mashine za kisasa kabisa zilizoboreshwa zenye latest technology (Digital Hearing AIds) kwa millioni 14 lakini bahati mbaya sana nazo hazijanipatia nafuu yeyote japo ni imara na nzuri zaidi ya zile za mwanzo za analogy.

Hivyo Wapendwa kwa yeyote anayewezakuwa anayefahamu tiba yeyote ya changamoto hii ya hearing loss, au hata kulipunguza kwa kuongeza usikivu na kunipunguzia adha nazokutananazo naomba anisaidie.

PIa hata msaada wa kimawazo na ushauri wa jinsi au mbinu yeyote ya kupambana na hali hii hasa kwa kupunguza changamoto na adha mbalimbali nazokutananazo nilizozieleza hapo juu nitashukuru sana.

1622142264152.png
 
Pole sana I can feel your pain ....ni Kama tatizo limekuwa sugu kwasasa

Kama hospital kubwa wameshindwa nadhani Kuna haja ya kutoka nje ya Tanzania Kama uwezo utapatikana
Ahsante

Ni kweli limekuwa sugu kwani kipindi cha nyuma shida ilikuwa sio kiasi cha kuweza kutambuliwa na mtu, hasa nikiongea na mtu asiyenijua, tunaongea vizuri kwani ilikuwa kwa mbali sana, lakini sasaivi nikikutana na mgeni mara kadhaa tukaongea maongezi mengi ni rahisi sana kujua ninashida ya usikivu
 
Jiamini unasikia km wengine

Potezea hali ya kuwa watu wananisikiaje ambavo siskii vizuri

Usiishi na watu jinsi wapendavyo Fanya upendavyo wewe

Fanya mazoezi ya kukimbia sana

Sehemu kubwa ya maisha yako iwe ni furaha

Toka mbali na jamii inayokusimanga kila wakati kuwa husikii vizuri kakaee mbali huko pia jibidishe kusikia wala usioneshe dalili za kutokusikia vizuri

La mwisho

KATAAHIYO HALI
 
Ahsante

Ni kweli limekuwa sugu kwani kipindi cha nyuma shida ilikuwa sio kiasi cha kuweza kutambuliwa na mtu, hasa nikiongea na mtu asiyenijua, tunaongea vizuri kwani ilikuwa kwa mbali sana, lakini sasaivi nikikutana na mgeni mara kadhaa tukaongea maongezi mengi ni rahisi sana kujua ninashida ya usikivu
Karibu unaonaje na Dkt Edwin

Jaribu ukaonane na Dkt Edwin katika hospitali ya Regency iwapo katika pitapita yako ya matibabu hukuwahi kuonana naye. Ni kujaribu.
 
Fanya mazoezi ya kukimbia sana

Sehemu kubwa ya maisha yako iwe ni furaha
Ahsante sana, kwa kiasi kikubwa ndio mambo ninayopambana nayo hayo, na kiasi kikubwa yanaonesha matokeo chanya, japo nalazimika kuishi kwenye ulimwengu mwingine kabisa kivyangu vyangu yaani.
 
Karibu unaonaje na Dkt Edwin

Jaribu ukaonane na Dkt Edwin katika hospitali ya Regency iwapo katika pitapita yako ya matibabu hukuwahi kuonana naye. Ni kujaribu.
Shukrani sana ahsante kwa ushauri nitajaribu kufanya namna.
 
Mkuu pole Sana, naonja jinsi unavyopata shida.Niliwahi kusikia pale Muhimbili kuwa Wana uwezo wa kuweka kifaa Cha kukusaidia kusikia,sasa je ulishawahi kwenda Muhimbili??.
 
Pole ila wakishindwa kukutibu kuna kifaa kinaitwa earing aid wanatoa hospitali unavaa unasikia normally kama watu wengine!
Bibi yangu hasikii kabisa so anatumia hiki kifaa unaongea nae vizuri ila akivua ukitaka kuongea nae uandike kwenye karatasi!
 
Nilipewa Kcmc aisee kinakusanya sauti nyingi labda upunguze kinaboa sana sometime
 
Jikubali mkuu.
Bora wewe hard hearing, wenzio ni viziwi kabisa but tumejikubali tulivyo maana Allah ana makusudio yake kutufanya hivi.
Karibu katika jamii ya viziwi ujifunze lugha ya alama hutojisikia mpweke maana haupo peke yako.
 
Tupo wote mi ni tinittus kabisa sipati concept kabisa ya neno husika hata iweje sauti nasikia ila sielewi mm nililost nikiwa naenda advance mpaka nimemaliza chuo nimehudhuria interview moja nimefanya poa na nafanya kazi mwaka wa pili sasa sina tabu na mtu

Mbaya niliondoka home sana kutokana na mara advancd mara dar chuo so marafiki zangu wananiona nina dharau kwa kitaa ni msomi pekeangu hawaminj kabisa kwamba sisikii
Job ndo matatizo matupu kutokana na contacting za watu wengi wanakuja kuulizia huduma siku moja alikuja jamaa akanikuta na kitambulisho changu basi akawa ananipa salama nilipata kutokana na ishara ya mkono sasa akawa anahitaji msaada ananielezea kaka anarudia mara nne wapi sisikii kabisa aliondoka kwa hasira nilifadhaika sana siku nzima kwa kweli😥😥😥jamaa alisema eti wafanyakzi wa pale wana dharau mi nilichafua. Image ya kampuni kabisa

Kingine kufanywa kama katuni ilihali wanajua siko poa all in all ilivunja mpaka mahusiano yangu huko nyuma still niko katika good postion of earning ndo ninachotabasamu ningkuwa empty sina kitu
 
Nakubaliana na wewe mkuu

Japo hatumkatishi tamaa, lakini ndio hali anayoipitia hivi sasa japo anaendelea kuyatafuta matibabu.

Hivyo kikubwa ni kujikubali na kujitahidi kukabiliana na mazingira kwa hali aliyonayo kadri inavyowezekana.

Asipo jikubali kila siku azidi kujiona mnyonge na kero kwa wengine hata kama wengine hawamuoni hivyo.

Japo wapo watakao mchukulia vibaya lakini hilo halitokuwa tatizo kama yeye mwenyewe atakuwa amejukubali.

Mimi ninasheji yangu anatatizo kama hili lakini anaishi vizuri tu jamii yake.
 
Mkuu pole Sana, naonja jinsi unavyopata shida.Niliwahi kusikia pale Muhimbili kuwa Wana uwezo wa kuweka kifaa Cha kukusaidia kusikia,sasa je ulishawahi kwenda Muhimbili??.
Ahsante!

Nafikiri unamaanisha conchlear implants, nilishajaribu kuomba hiyo huduma mara mbili baada ya kutofanikiwa kwa hearing aids machines lakini mara zote niliambiwa kwa kiasi cha usikivu kilichopo sasa kufanya conchlear implants haitafaa, haitanisaidia inaweza niharibu zaidi kwani sijafikia percentage za usikivu kiasi cha kuhitaji hiyo huduma hivyo niendelee kupambana na hearing aid machines tu.
 
Back
Top Bottom