KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 538
Kila la heri wapenda mabadiliko kura zetu umezipata. Tunakuombea umalize vyema kampeni huko Mbeya.
Daktari Slaa,
Kama unataka kura yangu, una masaa kama 20 hivi ya kujibu maswali yangu haya kabla sijaingia kwenye chumba cha kupigia kura.
- Naomba unieleze vipi mfuko wa cement unaweza kuuzwa TZS 5,000 (about USD 3.34 @ exchange rate of USD 1 = TZS 1,500) kwa mfuko. Naomba utupe CIF price ya mfuko mmoja mpaka bandari ya Dar es salaam) halafu ongeza gharama ya kusafirisha kontena kutoka bandarini mpaka warehouse na gharama za wapakuaji. Tueleze nini gharama ya kusafirisha mfuko huo wa cement kutoka warehouse ya Dar es salaam mpaka huko Arusha na gharama zingine za kupakia na kupakua hiyo mifuko kwenye gari. Na tuambie hao waagizaji wanaweka faida ya kiasi gani mpaka wanahakikisha mfuko wa cement unauzwa kwa shillingi za Kitanzania buku tano?
- Baada ya kuweza kuondoa ushuru wa forodha na VAT kwenye vifaa vya ujenzi pamoja na cement, je utalinda vipi viwanda vya ndani na ajira ya Watanzania. Kwa bei ya sasa hivi ya cement kutoka Pakistan, wenye viwanda wanalalamika kuwa wanashindwa kushindana bei na bei za cement ya Pakistan. Je wewe ukiondoa hizo kodi zote si viwanda vyote vya kuzalisha cement nchini vitafungwa? Na Watanzania elfu kadhaa kukosa ajira? Je utafanyajefanyaje hii issue?
- Naomba utueleze hiyo treni ya umeme uliyoahidi kujenga ndani ya mwaka mmoja ambayo itakuwa na uwezo wa kusafiri kutoka Mwanza mpaka Dar es salaam kwa masaa 3, pesa hizo utazitoa wapi hasa ukizingatia kuwa umeahidi kufuta kodi nyingi tu. Pia utatumia maajabu gani kukamilisha huo ujenzi ndani ya mwaka mmoja? Na hiyo treni itakuwa inasafiri kwa kasi (speed) gani na tueleze kama kuna treni yoyote duniani ambayo inasafiri kwa kasi hiyo sasa hivi.
- Maisha yako yote umesomea mambo ya dini yako ya Kikristo na mpaka PhD yako ni ya sheria za kanisa. Hii ikakupa wewe sifa zote za kuwa mtumishi wa mungu na ukafanikiwa kuwa Padri wa kanisa la Kikatoliki. Ulipoupata huo updari uliahidi kwa mungu wako kuwa utamtumikia kwa uwezo wako wote na utafuata masharti yake yote. Wakat unaendelea kumtumikia mungu wako ulishindwa kujizuia na ulikuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ulizaa naye watoto wawili kinyume na maagizo ya mungu wako. Sasa kama ulishindwa kutimiza ahadi yako kwa mungu, ni nini hasa Watanzania wanacho zaidi ya mungu cha kukufanya wewe usivunje hizi ahadi unazowapa kwenye kampeni za uchaguzi?
maana mliwacha kuwashawishi vijana wajiandikishe ,kampeni hizi ndizo zitakazowagharimu vibaya sana na kuwakosesha ushindi ,hongera kwa kuwavuta wananchi katika mikutano hilo halina mjadala. hofu wengi wao si wapiga kura,
Akiba ya maneno ikiwa utafanikiwa kuutwaa Ushindi basi 2015 uhakikishe WaTanzania waishio nchi za nje nao wanapiga kura huko huko waliko.
So far nakutakia kila la kheri.
Mwiba handakini.
yangu no, yafamilia yangu no, ya mtaa wetu no,ya kijiji chetu no, ya tanzania utapata 10%
Dr Slaa,
Kwa unyenyekevu mkubwa sana nakupongeza kwa ujasili wako na hari ysko katika mbio hizi za Uraisi.
Kama nilivyokubainishia mwanzoni wakati wa uteuzi wako ndani ya chama chako. Nilisema bado kabisa kwa wewe kugombea Urais mlitakiwa kuimarisha chama chenu katika ngazi za Ubunge na udiwani ili kuleta mageuzi makubwa ndani ya bunge la muungano.
Fahamu kubwa una wapambe wengi sana LAKINI WAPAMBE SIO APIGA KURA. Ninasikitika kukambia kuwa sidhani kama utaweza kufikisha hata 12% ya kura zako katika Uraisi.
Hongera sana kwa kujaribu.
Dr. Slaa kura yangu na weengi niliowashawishi kesho utazipata - ushindi wako ni ushindi wetu wapenda nchi. Usishangae kuwa wengine tupo concerned zaidi hata ya wewe na uchaguzi huu. Tuendelee kuhamasisha na tupo pamoja.