Ninaomba kura zenu ili niwe Rais wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninaomba kura zenu ili niwe Rais wenu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dr Willibrod Slaa, Oct 30, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Ndugu wana JamiiForums, Mtandao wa IssaMichuzi, wana FaceBook na mitandao mingine na Watanzania wenzangu wote kwa ujumla mtakaosoma ujumbe huu, Salaam toka Mbeya Vijijini, ndio tumeanza mikutano midogo ya kufunga kazi asubuhi hii na tutahitimisha baadaye.

  Ninashukuru sana kwa maneno ya heri kwa siku yangu ya kuzaliwa hapo jana na ningekuwa sina shukrani kama ningeacha ipite bila kusema asante kwa maneno mema mliyonipatia humu na kwenye facebook na hata waliopata nafasi kwa njia ya simu. Ninawashukuru vile vile kwa mashauri mbalimbali, na pia kwa sala na dua zenu.

  Ninashukuru sana na ninaona fahari kuwa ni mwanachama mwenzenu.

  Kampeni zote zinaisha leo na kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu kama mnavyofahamu. Kwa upande wangu nimetembelea karibu maeneo yote ya nchi yetu kubwa, nimekutana na watu mbalimbali na nimeona mengi. Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimeona mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

  Ninaelewa vizuri zaidi sasa kupitia mang'amuzi binafsi hali ya Taifa letu ilivyo na ya kwamba ni lazima tubadili mwendo na huko tunakokwenda maana tutafika mahali ambapo tutashindwa hata kujiuliza tulifikaje. Watu makini hawawezi kuendelea na njia ambayo wanajua wamepotea. Kuendelea kung'ang'ania kwenda wakati mnajua mmeshapotea ni kutukuza kiburi cha kujiona. Taifa letu limepotea njia na hata kama tukijitahidi kwa nyimbo na masimulizi mbalimbali kuhalalisha huko tunakokwenda bado tutakuwa tumepotea.

  Ni kwa sababu hiyo nilipoombwa kugombea Urais nilitambua uzito wa mzigo huu mkubwa kwani utahusiana moja kwa moja na kubadilisha mwelekeo wa taifa letu na kuanza kutengeneza pale palihorabiwa, kuinua kilichoanguka na kumwagilia kilichoanza kunyauka. Hili linahitaji mawazo mapya, uthubutu wa kiuongozi na mtazamo mpya wa nini Taifa letu linahitaji. Ndugu zangu, Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ili tuweze kujipa sisi wenyewe na watoto wetu nafasi ya kuweza kufanikiwa huko mbeleni.

  Mabadiliko haya siyo mabadiliko ya mapambo yaani kuhamimisha maua na vitambaa sebuleni wakati nyumba inanuka na nichafu. Wote mliosikiliza au kumwangalia mgombea mwenzangu jana ni wazi hana ahadi ya mabadiliko yoyote makubwa isipokuwa mwendelezo wa yale yale yaliyotufikisha hapa. Ni kutokana na hilo natambua kuwa kura ya kesho siyo kura ya kawaida; siyo kura kama ya 2005 au ya miaka kabla yake.

  Kura ya kesho ni kura ya kuchagua kuendelea na vile tulivyo kwa miaka mitano ijayo au kubadilika ili tuanze upya kwa njia sahihi na kwenda ambako sote tunakujua tunataka kwenda. Ninaamini tunachohitaji ni mabadiliko yatakayoanzisha mwamko wa kuanza kulijenga upya taifa letu. Hili ndilo lililonifanya nikubali pale Chama changu kiliponiomba ninyanyue bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huu katika nafasi ya Urais.

  Naweza kuwaahidi mengi na kwa maneno matamu ya kila aina. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

  Tutawapa nafasi Watanzania hatimaye nao wafurahia matunda ya uhuru wao na vile vile kuweza kuanza kujenga Taifa la kisasa ambalo litakuwa ni tamanio nakinara cha mabadiliko ya kiutawala, kiuchumi na kiutendaji katika Bara letu. Tuna uwezo, tuna sababu na tuko tayari kuwatumikia.

  Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Usiuze, usiache kuitumia na pale utakapoitumia itumie kwangu, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wetu wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote tuliyowaahidi tutayatimiza na zaidi.

  Msiwe na shaka, hata toka Ikulu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa mitandao hii na kuwapa taarifa mbalimbali moja kwa moja na kujibu maswali mtakayokuwa nayo kuhusu serikali yenu pale inaponipasa mimi kutolea kauli. Asanteni!!

  Mungu Ibariki Tanzania
  Mungu Ibariki Afrika
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tupo Pamoja Dr.Slaa mm napiga kampeni ya kitanda kwa kitanda na nimesha fanikiwa sasa nimehamia kwenye simu.

  Na uhakika kutoka kwangu na jamaa zangu tayari una kura 200 na za wabunge.
   
 3. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dr omba kitu kingine kura tumeshaamua siku nyingi tutakupa.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mungu akubariki pia wewe Dr. Slaa all the best and go get it!!!!!! Tunaendelea kuhamasisha mpaka 11 asubuhi kesho!
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Umezipata mheshimiwa Rais.... Nakupa yangu na watu 15 nyuma yangu. Pia nitachangia ktk akaunti namba ya chama fedha inayotosha kumlipa wakara mmoja kituoni ili kura yangu na hao 15 zisiibiwe na ccm. VIVA CHADEMA, VIVA SLAA (PhD)
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Oct 30, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Duh, ahsante mzee kwa kujali nguvu ya mitandao! Kila la heri kuelekea kesho.

  Najua uko busy lakini kwa kuamua kuja mwenyewe kumeonyesha unatujali na kuchukulia mitandao kuwa sehemu ya mawasiliano.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ofcourse this needs appeciation!
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mungu akulinde kwenye hizi Nyakati za mwisho za uchaguzi, KURA yangu ni yako Tuuu!
   
 10. T

  The King JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana Rais Mtarajiwa kwa waraka huu. Tunakuombea afya njema, maisha marefu na ushindi mkubwa kwako na wagombea wote wa chama chako katika nafasi za ubunge na udiwani. Mungu akujalie.
   
 11. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Nilipo soma habari hii nimetokwa na machozi, kweli tunastahili kufanya mabadiliko. Watu kama hawa wenye uchungu na taifa lao kuna umuhimu wa kuwapa nguvu, na kuwapigia kura.

  Ninapofikiria kuishi chini ya Uongozi wa CCM miaka mitana ijayo ni sawa na kuishi jehanum kwa miaka mia tano. Mwaka mmoja chini ya CCM ni sawa na miaka moja jehanum. Ndugu zangu wana JF nimeguswa, ninasafiri kwenda kupiga kura yangu kesho. Kura yangu ni lazima ichangie kuleta mabadiliko ya nchi yetu. Utajisikiaje kama kura yako haitachangia kuleta mabadiliko katika nchi yetu?

  Tupige kura na tumchague Slaa, tuchague Chadema. Asanteni.

  Kila mtu atume ujumbe huu kwa watu alio nao karibu.
   
 12. Profesy

  Profesy Verified User

  #12
  Oct 30, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sawa Sawa!!!
   
 13. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tulikuwa, tuko na tutaendelea kuwa pamoja! Najua JK na wapambe wake wakiona hili bandiko nao watakuja kubandika lao hapa! Ila uzuri wanajua awali ni awali tu, hakuna awali mbovu...presha inapanda, presha inashuka...
   
 14. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeshaconvert watu mtaani wa kutosha, sasa ni Slaa, hakuna kijani!! Tumechoka! Niko nampa maneno bibi yangu (78) anayeamini TANU na CCM ndio kila kitu(yajenga nchi), aachane na mawazo mgando. Ameanza anza kuelewa upepo na kesho naenda nae asubuhi akakupigie kura.

  Vote for Dr.Slaa, Vote for changes
   
 15. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mungu yu upande wetu. Hakuna wa kutushinda. Tupo pamoja baba. Mungu Ibariki Tanzania
   
 16. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Usiwe na wasiwasi Rais wetu, tuko pamoja, ur my president whatever the result, sababu sitamchagua mwingine. Mungu akulinde na Inshallah utashinda.
   
 17. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Amin amin, aluta continua! Viva Dr
   
 18. I

  Igembe Nsabo Member

  #18
  Oct 30, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya maneno ya matumaini, najua siku imefika ila wasiwasi wangu, hii mitandao kama IssaMichuzi imejaa U-CCM sana sijui kama inaweza kuweka hii taarifa kwenye blog yake!!

  Nashukuru na kama ingewezekana taarifa hii ingekwenda kwenda magazeti ambayo hayana mlengo wa ushabiki wa vyama! ( kama vile Mwanchi) na magazeti mengine ambayo si washabiki wa vyama.

  Mytake: Kuanzia jana na leo vyombo vyote vya Habari sidhani kama vitatoa nafasi kwa kuweka coverage ya Dr. Slaa.
   
 19. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Go Slaa Go... For the voices of the oppressed and the blood of the innocent ones is heard from a distance, the flesh of the poor children who were denied their right to live is vivid, nothing can stop them, the cry is everywhere, Go Slaa Go, NO river to stop you, no mountain to downslip you!

  Go Slaa Go, for the harvest is ready, go now for the sky has heard our prayers and our Ancestors ARE with you, go as MAN go, never dare to look back, for hundreds are with you, Go to serve them. Mpiganaji Elli
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  By any means necessary!​
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...