Ninaomba jibu la hesabu yangu hii hapa

Ngoja tunaojua haya makitu ya namba tuwadadavulie maana wengi mnachanganya sana mambo.....na huo ndio muelekeo wa elimu yetu hadi mnaletewa div 5 sasa.

Kwa wale wanaosema jibu ni 9, wanakosea kuifananisha hiyo hesabu na hii hapa;

6/2(1+2) >>>> (6/2)(1+2) >>> 3x3=9

Wanaosema jibu ni 1; wanafanya hiyo hesabu sawa na hivi:

6/2(1+2) >>>> 6/{2(1+2)} >>> 6/(2x3) >>> 6/6=1

Kwasisi Mathematicians, hiyo hesabu ni sawa na kusema;

chukua 6, igawanye kwa mara 2 ya 1 kujumlisha 2:

Ambayo kwa kutumia maneno hayo; 1 jumlisha 2 ni 3, kisha zidisha mara 2 ni 6.

Kwahiyo tukirudi kwenye swali letu ni sawa na kusema;
chukua 6 igawanye kwa 6, jibu itakua 1:

Kimahesabu yenyewe sasa ni hivi;

6/2(1+2); ukitumia MAGAZIJUTO ni sawa kusema;
6/...2x...1+2 >>> 6/...2x3 >>>> 6/6=1.

Mpoooo???!!!

Aiseee...!!! Hakika ualimu ni kazi ngumu...kwa nini uzidishe kabla ya kugawanya? Ile kujumlisha namba za ndani unakuwa umeondoa mabano inabaki 6/2*3. Hapo lazima ugawanye kwanza ndo uzidishe!
 
Bana jibu ni 9....halaf hao ma PCM ndo hua wanachanganya wadudu hapa kahesabu kadarasa la saba kukisolve kwa sheria za advance! !
 
Attachments

  • 1402817281099.jpg
    1402817281099.jpg
    18.5 KB · Views: 91
Yan nimeona argument zako huko juu, bila kutoa msimamo wako nikadhani unajua kumbe hata kujua hujui na wewe jibu ni moja.

Hizo base hapa zinatoka wapi, mbona kuna watu hapa wameeleza vizuri, bado hamuelewi? Tatizo hapa wengi nikujifanya wajuaji wakati hujui.
Sijajifanya kuwa najua mkuu ila usikariri hesabu....hesabu ina misingi yake,na mojawapo ni kama hiyo,me nlikuwa naweka ulinganifu katika hoja yako kuwa mbona hata log ina base ten...si kweli kuwa log ina base ten pakee,ukweli ni kuwa log itakokotolewa kutegemeana na base iliyoanishwa,kama haijatajwa(kwa mfano log ya base two) unakokotoa katika base ten,kwa sababu tunachukulia kuwa namba zote ulizopewa zipo katika base ten...
 
Hiv hayo mambo ya log na base ten mnayatoa wapi kwenye hesabu ya la sita hiyo?
 
Aisee kumbe hata wewe unashabikia jibu la moja?? Mi nlijua tupo kwenye tisa wote....ntamshitaki mwalimu wangu wa hesabu kama hesabu hiyo jibu ni moja

Mkuu Khantwe, nitake radhi yan na bachelor yangu ya Ualimu niweke moja kwa Hesabu iyo?

Jibu kwangu ni 9
 
Back
Top Bottom