Wataalamu wa Mikopo, Uchumi, Hesabu naomba Mnieleweshe hapa

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Ukikopa Bank 20M kwa riba 16% kwa muda wa miaka 9(miezi 108) unalipa 37,854,541.16, kwa ufupi ni kama M38 hivi,(KAUSHA DAMU P2)

Hii ni kutokana na kikokotoo cha loan calculator,
Screenshot_20240101_141852_Loan Calculator.jpg


Sasa nataka nijue hii kimahesabu inakujaje?
Maana wao automatic tuu wanakuletea hivyo.

Hata ukijaribu ile hesabu ya kawaida ya

I = PRT/100,
Hupati hilo jibu..

Mikopo ni Janga.
Nikope 20M nipate 17M, nirudishe 38M?
 
Hiyo formula ya primary iache kwenye straight method.


Kwenye reducing balance na compounding and discounting interest mambo ni mengi, kiufupi wewe chukua pesa fanyia mambo yako. Maana saving ya peke yako ni mtihani kwa waafrica walio wengi.

Monthly Repaymant = P (r(1+r)^n)/((1+r)^n-1).

P = principal amount.
r = rate of interest.
n = number of period.
 
Ukikopa Bank 20M kwa riba 16% kwa muda wa miaka 9(miezi 108) unalipa 37,854,541.16, kwa ufupi ni kama M38 hivi..

Hii ni kutokana na kikokotoo cha loan calculator, View attachment 2859258

Sasa nataka nijue hii kimahesabu inakujaje?
Maana wao automatic tuu wanakuletea hivyo.

Hata ukijaribu ile hesabu ya kawaida ya

I = PRT/100,
Hupati hilo jibu..

Mikopo ni Janga.
Hiyo 16% ni riba ya mwaka mmoja.

Ukikopa miaka 9 maana yake chukua 16 zidisha Mara 9.

Riba ni 144%.

Na bank ni wezi.

Kwenye pesa uliyokopa, ujue itakatwa BIMA na PROCESSING FEE.

Halafu Riba itafanyika kabla hawakata hizo Bima na processing fee.

Kwa lugha rahisi UTALIPA riba ya Pesa ambayo hutachukua
 
Kausha Damu Iliyopewa Nyaraka Zote Na Serikali
Ukisikia Maji Tunaita Mmaa Ndiyo Hapo SasA
Ma~Bank Yanawasumbua Sana Wasomi, Watumishi Wanajikuta Wamekanyaga Kaa La Moto



Hamna Hamna Ndimo Mlimwamo!!
Unataka Kujenga, Ununue Gari, Upate Suit, Oops Lazima Baadaye Ujione Garasa La Mavi Ya Mbuzi Kwenye Mchezo Wa Karata
 
Unataka hesabu?
Tufanye hesabu,
Chukua hii formula

R = M r [ (1 + r) ^d ] / [ (1 + r)^ d -1]

Let
R = Rejesho lako kwa mwezi = ?
M = Mkopo uliokopa = 20,000,000
r = riba ya mkopo = 16%
d = muda wa mkopo kwa miezi = miak 9
^ = hio ni raise/power, ikimaanisha hio d iko raised

Twende kimahesabu..

r = 16% , hii inabidi uiondoe kwenye asilimja halafu uigawanye kwa mwaka..
Hivyo
r = 16÷100 = 0.16/12 = 0.0133333333
d = 9, hii unachukua miaka 9 unazidisha kwa miezi(9×12=108)


R = 20,000,000 × 0.0133333333 (1+0.0133333333)^108 ÷ (1+0.0133333333)^108 - 1


= 350,505.016
, ukiikadiria ndio inakuja 350,505.02 unayoiona hapo kwenye chart yako.
Hio sasa ndio rejesho lako la kila mwezi..
Ukilizidisha kwa Muda wote wa mkopo

350,505.016 × 108 = 37,854,541.728
ndio hio unayoiona hapo mzee baba.

Shida hapa ukiandika hesabu uki upload inakaa shaghala baghala,
Ukihitaji zaidi niambie nikuandikie niweke picha.
 
Unataka hesabu?
Tufanye hesabu,
Chukua hii formula

r [ (1 + r) ^d ]
R = M ————————
[ (1 + r)^ d -1]


Let
R = Rejesho lako kwa mwezi = ?
M = Mkopo uliokopa = 20,000,000
r = riba ya mkopo = 16%
d = muda wa mkopo kwa miezi = miak 9
^ = hio ni raise/power, ikimaanisha hio d iko raised

Twende kimahesabu..

r = 16% , hii inabidi uiondoe kwenye asilimja halafu uigawanye kwa mwaka..
Hivyo
r = 16÷100 = 0.16/12 = 0.0133333333
d = 9, hii unachukua miaka 9 unazidisha kwa miezi(9×12=108)


R = 20,000,000 × 0.0133333333 (1+0.0133333333)^108 ÷ (1+0.0133333333)^108 - 1


= 350,505.016
, ukiikadiria ndio inakuja 350,505.02 unayoiona hapo kwenye chart yako.
Hio sasa ndio rejesho lako la kila mwezi..
Ukilizidisha kwa Muda wote wa mkopo

350,505.016 × 108 = 37,854,541.728
ndio hio unayoiona hapo mzee baba.
Shukrani Sana Hapo Uamuzi Afanye Yeye
 
Hivi kibihashara Milioni 20 inaweza zalisha 500k kwa mwezi??
Hio inazalisha vizuri kabisa, labda kama ilivunywa vunjwa sana, yaani namaanisha ilitumika labda kwenye ukarabati, kodi, matengenezo na maandalizi ya biashara hio ila kama yote imeingia kwenye mzunguko..
 
Back
Top Bottom