Ninachukizwa sana.....

Ninachukizwa sana.....

Hmaster

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
346
Reaction score
86
Ninachukizwa sana na taarifa juu ya OCD Arusha kuwaita wananchi wenzie panya,
Ninachukizwa sana na jinsi serikali inavyoufanyia mzaha muswada wa katiba mpya,
Ninachukizwa sana na tabia ya baadhi ya wabunge kulala bungeni wakati vikao vikiendelea,
je wewe unachukia nn?
 
Nachukizwa sana na tabia ya wahaya kusogeza mipaka.
 
Nachukizwa sana na tabia ya polisi kufanya kazi kwa maelekezo ya wanasiasa...
 
nachukizwa na viongozi wanaojali matumbo yao na sio matatizo ya wananchi.
 
tehe, hii nzuri.

Nachukizwaaa..nachukizwaa...aaaargh! nimesahau, wacha nkachungulie kwenye diary, huwa naziandika kero zoote, niipate iliyojirudia mara nyingi niibwage bwaaaa.
 
Nachukizwa sana na tabia ya viongozi kwenda kutibiwa nje ya nchi badala ya kuboresha hospitali zetu hapa.
 
Nachukizwa sana na tabia ya viongozi kuendelea kukumbatia uongo wa wawekezaji huku wananchi wakiishi katika lindi la umasikini.
 
Kweli si vizuri kabisa kuwaita binadamu wenzako panya.
Jamaa yule OCD si mzima kabisa. Kalaaniwa itakuwa.
 
nimechukizwa na kauli ya waziri mkuu wa Uingereza.
 
Nachukizwa na...... (Ngoja kwanza niangalie nianze na lipi)
 
Nachukizwa sana na tabia ya soksi zangu kuanza kunuka hata kabla hazijamaliza wiki mbili.
 
Nachukizwa na hali ya nafasi za mhimu kama viti maalum vya ubunge kukaimiwa na wadada wenye sifa moja tu! "nyumba ndogo za viongozi wa juu"
 
Nachukizwa na hali ya nafasi za mhimu kama viti maalum vya ubunge kukaimiwa na wadada wenye sifa moja tu! "nyumba ndogo za viongozi wa juu"

Mwee, wivu tu umekujaa.
 
Nachukizwa na tabia za wapinzani kupinga kila kitu serikali inachofanya.
 
Back
Top Bottom