Ninachotaka kukisema mwakijua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninachotaka kukisema mwakijua?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mtanzanika, May 5, 2012.

 1. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,208
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Jamaa mmoja mwenyetabia ya kujifanya shekhe na hali elimu yake mgogoro alishtukizwa siku moja baada ya swala ya Ijumaa na kuombwa atoe mawaaidha,msikiti ulikua umejaa!
  Aliposimama alianza!
  'Ndugu zangu waislam ninachotaka kukisema mnakijua hamkijui?'
  Waislam(kwa pamoja):'Hatukijuiiii'
  Jamaa:'Basi kama hamkijui sina haja ya kuzungumza na watu wasiojua'
  Jamaa akenda zake!

  siku nyingine akapewa tena nafasi,aliposimama akauliza!
  'Ndugu zangu waislam ninachotaka kukisema mwakijua hamkijui?'
  Waislam(siku hiyo waliashakubaliana):'Tunakijuaaaa!'
  Jamaa:'Basi kama mwakijua sina haja ya kukisema kwa kuwa wote mwakijua'.Jamaa akenda zake.

  Waislam wakampania wakaweka mkakati,siku ya tatu ilikua sala ya Iddi waumini wamejaa ndani na nje pia!jamaa aliposimama kama kawa akauliza!
  'Ndugu zangu katika Imani,ninachotaka kukisema mwakijua hamkijuig?'
  Waislam (walioko ndani ya msikiti):'Tunakijuaaa'
  Waislam(walioko nje):'Hatukijuiii'
  Jamaa:'Basi nyinyi wa ndani mtawafundisha wa nje,wassalaam'
  jamaa akenda zake.
   
 2. h

  hamic mussa JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  teh teh teh nacheka kwa vina.
   
Loading...