Nina stress sana, ushauri unahitajika

Nina stress sana, ushauri unahitajika

Habari za wakati huu.

Ninaandika hapa nikiwa na msongamano wa mawazo mengi, huyu mwanamke ambaye ni mpenzi amekuwa akinipasua kichwa sana, ni mwepesi wa kubadili maamuzi bila kufikiria kuwa ni kiasi gani inaweza kutugharimu.

Ana ujauzito wangu ila kila tutakapokwaruzana anakimbilia kusema atalea mwenyewe hahitaji msaada wangu wala hanitegemei sana, nikitaka nijitoe tu, sasa nabaki na maswali, mwanangu nahitaji tumlee pamoja wazazi wake wawili, ikiwa nina mpango wa kumuoa nije kuishi naye, ila najiuliza sana kama tutafika mwisho wa safari, ili yeye aendelee kuwa na mimi inanilazimu nimnyenyekee sana, hebu nishaurini wakuu nifanyaje maana nahisi kuchanganyikiwa.

UPDATE; Comment number 5 nimeweka screenshot ya maongezi.


Sent using Jamii Forums mobile app
Bora wewe umeambiwa atalea mtoto pekeake maana yake utamuona huyo mtoto, mimi leoleo nimeambiwa mimba yangu itatolewa.
 
Kwanza nikupongeze wew ni kijana shupavu ambaye upo tayari kulea kiumbe Mungu atachokuletea dunian!. hongera sana
Pili unajua watoto wakike hawa saa nyingine huwa wanaleta shida.sasa cheza na saikolojia yake wewe naomba ukae kimya kama wiki au mwezi lazima akutafute.Usioneshe kunyenyekea sana. Damu nzito kuliko maji Usiohofu juu ya mtoto wako.
 
Huu ndiyo uchafu wa zinaa.

Mnapoambiwa msifanye uzinzi na uasherati nyie mnajifanya mnajuwa zaidi kuliko aliyewaumba.

Kwetu tunasema, kiranga komo.
 
Kwanza nikupongeze wew ni kijana shupavu ambaye upo tayari kulea kiumbe Mungu atachokuletea dunian!. hongera sana
Pili unajua watoto wakike hawa saa nyingine huwa wanaleta shida.sasa cheza na saikolojia yake wewe naomba ukae kimya kama wiki au mwezi lazima akutafute.Usioneshe kunyenyekea sana. Damu nzito kuliko maji Usiohofu juu ya mtoto wako.
Thanks mkuu ngoja nimpotezee kwanza kama miezi sita tumbo lijae akae sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
awali ya yote mkuu pole kwa hayo,
naomba historia fupi ya mchumba wako, kabla ya mimba ali kuwa na tabia za namna hiyo na mabo mengine ya tabia maana tunaweza sema hakufai kumbe hasira anapata kutokana na ujauzito huo, historia itasaidia mkuu
 
It must have been love, but it`s over now! Huyu binti anakuchezea akili tu, actually ana enjoy sana reactions zako. Funga virago mkuu.
 
Asee mkuu huyu simuelewi nia yake, alianza kusumbua muda!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka kakubali kukubebea mimba, anakupenda. Namna utakavyo react kutokana na action zake, kunaweza kukapelekea mkaachana. Namna nzuri ya kuachana nae, subiri akishajifungua, hudumia kachanga, pima uelekeo. Ikiwa hali bado tete, tafuta mpango wa kando. Ukiona huko kuna afadhali, hamishia majeshi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom