Nina mtu wangu...huo ndo ukweli wangu

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Wakuu habari za leo? Mara nyingi nimekuwa nikikumbana na hilo jibu "nina mtu"...
Hii hutokea baada ya kufanya juhudi nyinginezo za kumuweka mtu karibu, nimekuwa mtu wa kukata tamaa sana...licha ya ushauri niliowahi kuupata Msaada; Nahisi kuishiwa mbinu

Ninachojiuliza

1. Je inawezekana kuwa na mtu ambaye ana mtu kabisa?
2. Nifanyeje na wewe huwa unafanyeje ukutanapo na jibu kama hili?
3. Je watu wanaingia kwenye mahusiano kwasababu tu hawana watu?

Naombeni ushauri wenu, maana kuna mdada nampenda na nimejitahidi kumuweka karibu...lakini jana kaniambia anaouita ukweli wake "ana mtu"...nimeshindwa nifanyeje mpaka muda huu.
 
ni nadra kukuta hana mtu labda iwe katoka kwny mahusiano punde. pia inawezekana likatumika mbadala wa hapana.
 
wapo watu ambao wako free, tafuta hao... afterall kuna nafasi moja tu kumpenda mtu kwa mapenzi ya kweli ingawa unaweza kuwapanga watu kibao kwa sababu ya kuwachuna, kujionyesha kwamba wewe ni kidume etc
 
Wasio kwenye mahusiano wapo ila yahitaji utulivu kuwapata..afadhali huyo anaekwambia ukweli kuliko mwingine atakudanganya yupo single kumbe ana intention ya kukuongeza kwenye list..
 
Ulitaka vipi na habari ndio hiyo....mimi nahisi approach yako ilikuwa mbaya, kama ungeweka uhusiano au nia yako yeye awe mpenzi wako yasingefika huko, naona kama ulianzisha kama yawe ya platonic friendship na wewe ukachanganya kuwa demu anamekukubali.
 
Mkuu kuna ukweli ndani ya maneno yako...isitoshe sikuwa na malengo ya muda mfupi
 
Ulitaka vipi na habari ndio hiyo....mimi nahisi approach yako ilikuwa mbaya, kama ungeweka uhusiano au nia yako yeye awe mpenzi wako yasingefika huko, naona kama ulianzisha kama yawe ya platonic friendship na wewe ukachanganya kuwa demu anamekukubali.

mhhh lakini kama ana mtu si ingebaki kuwa hivyo....inawezekana pia nimekosea, ndo maana natafuta mbinu za kujisahihisha
 
Mkuu komaa alafu unaonekana ulikuwa serious mpaka noma.Wenzako tunaanzaga kimasiala halafu kitu messi babu.Ukishindwa omba kampani yake utaniambia mwenyewe
 
mhhh lakini kama ana mtu si ingebaki kuwa hivyo....inawezekana pia nimekosea, ndo maana natafuta mbinu za kujisahihisha

Huwezi kuforce someone to love you, kama anamtu chapa lapa, na kama alikuwatingisha kibiriti na akaona haupi attention, she will comeback!
 
hiyo ndo janja ya wasichana.
Akikwambia ana mtu utaona kweli mzuri ndo maana wenzio wamewahi kwa hiyo utaongeza nguvu na msichana ataongeza thaman yake.
Wakati naanza chuo wasichana walikuwa wanajivalisha pete za ingejiment wenyewe ili waonekane walishapendwa na wengine! ukimtokea mara anakuambia nipo singo mara hii alinivalisha akawa hajatulia nikampiga chini na sababu kibaooooo.

WW komaa nae alfu uangalie anavyorespond utagundua nae anakupenda au la, ukiona haeleweka sepa
 
poa mkuu...nilikuwa nafikiria kufanya hivyo..nashukuru kwa kunipa moyo,, anadai mtu wake anasoma Botswana na hajaja mwaka wa tatu sasa...
 
Wakuu habari za leo? Mara nyingi nimekuwa nikikumbana na hilo jibu "nina mtu"...
Hii hutokea baada ya kufanya juhudi nyinginezo za kumuweka mtu karibu, nimekuwa mtu wa kukata tamaa sana...licha ya ushauri niliowahi kuupata Msaada; Nahisi kuishiwa mbinu

Ninachojiuliza

1. Je inawezekana kuwa na mtu ambaye ana mtu kabisa?
2. Nifanyeje na wewe huwa unafanyeje ukutanapo na jibu kama hili?
3. Je watu wanaingia kwenye mahusiano kwasababu tu hawana watu?

Naombeni ushauri wenu, maana kuna mdada nampenda na nimejitahidi kumuweka karibu...lakini jana kaniambia anaouita ukweli wake "ana mtu"...nimeshindwa nifanyeje mpaka muda huu.

mkuu jibu kama hili lako nimelipata juzi-ila sijakata tamaa-leo nimefanya utaratibu tukutane tena ili nimwanzie maelezo marefu-kifupi nataka kumu-exploit kwa maelezo mengi-nione reaction yake
 
mh haya majibu ni common sana, ila sema wengine huwa hawamaanishi wanachokisema
 
Mkuu,kwan we unataka wa kuoa au wa kutafuna 2 then usepe?kama unataka wa kutafuna ni PM nikupe maujanja.
 
Back
Top Bottom