Nina mtaji wa milioni 1.5 nataka kufungua biashara hii, wazoefu nahitaji mawazo yenu

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
1,448
2,289
Salute wakuu,

Baada ya kutulia na kufikiri sana, nikapata wazo la kufungua biashara ya vitu vya electronics sijui kama nipo sahihi. Vitu hivyo ni kama:
  • Flash drive
  • Memory card
  • USB wire
  • Charger
  • Card reader
  • Power bank
  • Min speaker
  • Bluetooth earphone
  • Hair cutting machine
  • External and Internal hard disk
  • Protector za simu pamoja na cover
  • Battery za simu na vioo
  • Gaming pad, na vitu kama hivyo
Mimi nipo mkoani nimepata uzoefu wa kuagiza hii mizigo kutoka Ali Express na mizigo yote imefika salama.

Sasa mpangilio upo hivi, mfano flash ya Toshiba GB 32 Ali Express unapata kwa 13,900 yenyewe 11,000 na usafiri (shipping) 2,900 mimi nitauza kwa elfu 25, maelewano pia yapo.

San Disk GB 16 Express inauzwa elfu 6 hadi 7 mimi nitaanza na elfu 15. Maelewano ya kushuka yapo kiasi.

Hapo hapo huku nilipo flash ya 2GB bei ni elfu 12.

Memory hapa nachukua pieces 20 zinakuwa (100) 8GB na 4GB jumla bei inakaa laki na 20 na kitu hivi.

Then 8GB elfu 10 pungufu ni mpaka elfu 8 then 4GB elfu 5.

Bluetooth ear phones hizi ni elfu 3900 mimi nitaanza na elfu 8, bei ya punguzo ipo.

USB wire hizi 1500 nitaanza na elfu 4
Card reader izi zipo za 800 ad 900 mi ntaanza na elfu 2500.

Hivyo ni vichache na mpangilio wake wa bei ni huo kwa utafiti mdogo niliofanya.

Mfano:

Flash GB 32 huku mkoani unaanza na 45,000 elfu mimi nitaanza na 25.

Kutokana na ninakotoa yapo mengi ya kuandika, ila huo ni mpangilio wa vichache.

Naomba mnishauri hapo nitatoboa kwa bei hizo lakini pia nitaweka vipeperushi kutangaza bidhaa hizi ili wengi waone hapo vipi mawazo yenu jamani.

Poleni kama uandishi hautakuwa poa.

IMG_20191119_163626.jpg
Screenshot_2019-11-24-00-43-31.png
Screenshot_2019-11-24-00-43-25.png
Screenshot_2019-11-24-00-43-18.png
IMG_20191124_004817_276.JPG
IMG_20191124_004835_003.JPG
IMG_20191124_004844_964.JPG


NB: Utani na dharau hazifai. Ukikosa cha kuchangia pita kimya wapo wenye busara watatoa mawazo yao na sio kuvunjana moyo.

Muwe na siku njema wapendwa.
 
mkuu mimi, Mkuu kabla ya kuanza kufanya hyo biashara.. umejaribu kufanya research kwenye eneo unalotaka kuiweka kuwa lina mzunguko mzuri (Yaani wateja wapya) kwa sababu hyo biashara haitegemei sanaa wateja walewale (wanaojirudia)..

Think deep before act...! Naiman umenielewa japo mwandiko wangu mbaya
 
Kabla sijaagiza ntaanza kuuliza makato yapoje kwanza
We omba tu TRA wasikuotee, na kwa njia ya Posta wanaweza wasikuotee lakini wakikuotea, TRA hawana aibu!! Hata hivyo, jaribu kununua kwa buyers tofauti (about 2 buyers kwa same product) ili kupunguza risk ya kuchelewa mzigo na kucheleza zaidi! Mimi si mara moja wala mara 2, nimeshawahi kupata mizigo within 2 weeks, lakini pia si mara moja wala mara mbili, nimeshawahi kupata mzigo kwa zaidi ya mwezi!

Aidha, jaribu pia kutafuta supplier wa same product aliye Alibaba kwa sababu kwavile wanauza jumla, hawa ni more cheap though mtihani upo kwenye kupata supplier anaye-ship to Tanzania!
 
Si umesema usha agiza tiyari? Hahaaa kwa kuongea unawexa ona ni kitu rahisi sana. Watu Mikoani wenye Maduka ya mitahi ya milion hadi 100 wanachukua mzigo Dar sembuse wewe milion 1 mtaji wa kimachinga?

Kachukue kwa Maduka ya Jumla Dar. Kwa kuongea ni rahisi mno tena mno ila njoo kwenye practical ndo utaelewa ninacho manisha.
Kabla sijaagiza ntaanza kuuliza makato yapoje kwanza
 
Back
Top Bottom