Nina mtaji wa milioni 1.5 nataka kufungua biashara hii, wazoefu nahitaji mawazo yenu

Huo mtaji Wa kimachinga ni wangu Mimi na ndio nnapo anzia binafsi nimeamua kuchukua through Ali express sio kwamba sijui kama dar ipo nafahamu ata hao Wa dar nao wanatoa uko uko alibaba amazon n.k
Alafu mtaji wangu ni 1.5 ndio uwezo wangu sasa nitajilazimishaje niwe na M 10 pasipo uwezo kuruhusu bado ujanivunja moyo mkuu labda uje na lingine.
Ametumia lugha kali lakini ni ushauri mzuri. Lazima ujiulize wafanyabiashara waliotangulia wanatumia njia gani kupata mzigo? Je ni njia unayotaka kuitumia wewe? Kama sio kwanini hawaitumii? Unatakiwa usisahau kuwa hii mitandao inafahamika hivyo ni lazima ujiulize kama haitumiki sana na wafanyabiashara wa kati na wadogo ni kwanini?

Kama upo mkoani ukichukulia kwa Jumla dar utauza kwa faida bado, mtaji ukikua unaweza kusafiri mwenyewe na kwenda China.

Kwa mtaji ulio nao nakushauri kama ni lazima sana uagize mwenyewe basi tafuta vitu unique kimoja au viwili uuze kimachinga taratibu kwa faida. Kitu ambacho upatikanaji wake si rahisi' huku.

Ukitumia njia unayotaka kutumia utapata changamoto ya kodi' hata ukifanikiwa kukwepa Mara ya kwanza basi Mara ya pili au ya tatu utalipa tu' sasa hapo biashara inakuwa haina going concern.

Kila la heri mkuu.
 
Mkuu Kama umeona fursa hapo ulipo. Itumie. Unaweza kuagiza mizigo yako AliExpress na ikafika hayo masuala ya Kodi yasikutishe sana. Pia Aliexpress unapata uwanda Mpana wa kununua bidhaa unazotaka zaidi. Bila kuathiri shughuli zako. Cha msingi Una nunua mzigo tofauti tofauti Kwa wauzaji tofauti tofauti. Hivyo mzigo Inaweza kuja katika size ya kawaida na Tra wasijue kitu.

Pia unaweza kutangaza kwenye Mitandao. Una Anaanda Tangazo lako vizuri halafu unarusha katika eneo unalo ishi maana Instagram/Facebook wanakupa Uhuru wa kuchagua wapi Tangazo lako lifike.

Mimi nilianza na Kama laki 2, kununua vitu online halafu nauza online Ila nafanya delivery mwenyewe. Mambo si haba mtaji unakuwa na Maisha yanasonga. Hivyo hata wewe unaweza kufanya na kufanikiwa Zaidi la msingi ni malengo na mikakati yako.
 
Mkuu kikubwa kama feasibilty study imesoma positive.Shusha mzigo.Usitishwe na hao wanaosema 1.5m n ndogo kuagiza mzigo eti uchukulie dsm.In fact Bongo bado watu wengi wako nyuma kutumia masoko ya online.
Kabisa kama unatulia na online market unatusua
 
Ametumia lugha kali lakini ni ushauri mzuri. Lazima ujiulize wafanyabiashara waliotangulia wanatumia njia gani kupata mzigo? Je ni njia unayotaka kuitumia wewe? Kama sio kwanini hawaitumii? Unatakiwa usisahau kuwa hii mitandao inafahamika hivyo ni lazima ujiulize kama haitumiki sana na wafanyabiashara wa kati na wadogo ni kwanini?

Kama upo mkoani ukichukulia kwa Jumla dar utauza kwa faida bado, mtaji ukikua unaweza kusafiri mwenyewe na kwenda China.

Kwa mtaji ulio nao nakushauri kama ni lazima sana uagize mwenyewe basi tafuta vitu unique kimoja au viwili uuze kimachinga taratibu kwa faida. Kitu ambacho upatikanaji wake si rahisi' huku.

Ukitumia njia unayotaka kutumia utapata changamoto ya kodi' hata ukifanikiwa kukwepa Mara ya kwanza basi Mara ya pili au ya tatu utalipa tu' sasa hapo biashara inakuwa haina going concern.

Kila la heri mkuu.
Fact umeongea mkuu asante sana
 
Mkuu Kama umeona fursa hapo ulipo. Itumie. Unaweza kuagiza mizigo yako AliExpress na ikafika hayo masuala ya Kodi yasikutishe sana. Pia Aliexpress unapata uwanda Mpana wa kununua bidhaa unazotaka zaidi. Bila kuathiri shughuli zako. Cha msingi Una nunua mzigo tofauti tofauti Kwa wauzaji tofauti tofauti. Hivyo mzigo Inaweza kuja katika size ya kawaida na Tra wasijue kitu.

Pia unaweza kutangaza kwenye Mitandao. Una Anaanda Tangazo lako vizuri halafu unarusha katika eneo unalo ishi maana Instagram/Facebook wanakupa Uhuru wa kuchagua wapi Tangazo lako lifike.

Mimi nilianza na Kama laki 2, kununua vitu online halafu nauza online Ila nafanya delivery mwenyewe. Mambo si haba mtaji unakuwa na Maisha yanasonga. Hivyo hata wewe unaweza kufanya na kufanikiwa Zaidi la msingi ni malengo na mikakati yako.
Da ongera sana mkuu mungu akuzidishie
 
Back
Top Bottom