Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Acha kunyonyesha haraka sana bila hvyo utamuaharibu mtt anza kumpa mtt maziwa ya lactogen 1 na akifikisha miez 6 anza kumpa vyakula lain lain
Wee unamshaurije MTU aache kunyonyesha? Nani kakwambia MTU akiwa mjamzito kunyonyesha ndo basi? Mafunzo ya wapi hayo? Acha kukurupuka na kutoa mafundisho dhoofu na potofu.

Mjamzito anaruhusiwa kunyonyesha mpaka mtoto mwenyewe akatae. Virutubisho vya maziwa viko pale pale na havina madhara yoyote .
 
Kwa hiyo nimuachishe kumnyonyesha? Maana bado namnyonyesha na sijawahi kumpa chochote tofauti na maziwa yangu

Hivi clinic wamewekewa nyau waende.
Si uende ukaulize hayo yote huko why unataka myths za jf wakati vituo vya afya kila mahali!!!
Umwachishe umeshauriwa na Doctor? Anaharisha pengine nyonyo yako chafu ... go to the doctor!
 
Unazaa kama ulivyomzaa aliyezaliwa kabla, mbina kuna waozaa watoto hata mlkupishana miezi 10, 11 au 12.

Usifikirie kutoq wala kuishi kufikiria wengine watasemaje, siku ukikosa mimba tena hao hao ndio watakusema.

Na usiulize tena haya mambo, bali mshukuru Mola kwa baraka ulizopewa.

Ni mimi mzazi.
 
Naelewa huo ugumu Mkuu lakini zipo njia mbali mbali za kuweza kuzuia mimba nyingine kabla ya wakati muafaka na mkiwa makini hili linawezekana kabisa vinginevyo mimba kama hizi kwa Watanzania zingekuwa nyingi mno.

Mkuu tufurahie mtanzania mwenzetu yuko njiani anakuja, hayo yameshapita, hata hivyo ukiwa na mtu wako condom ni vigumu sana kukumbuka.
 
Kwa hiyo nimuachishe kumnyonyesha? Maana bado namnyonyesha na sijawahi kumpa chochote tofauti na maziwa yangu
The BabyCentre editorial team. Yes, your body will carry on making milk while you're pregnant, so you will be able to breastfeed. And after the birth you can breastfeed both your babies (tandem feeding), if you'd like to. Breastfeeding during pregnancy is fine if your pregnancy is going well, and you are healthy.

Hivi ndivyo wazungu wanavyoshauri, lakini kiafrika afrika wanasema uache kumnyonyesha mtoto ukiwa na mimba, kama unaona diarrhoea kwa mtoto inaweza kusababishwa na maziwa yako, ni kheri umwanzishie SMA gold ni mazuri tu kama maziwa mbadala ya breast feeding. Miezi sita ndiyo wanashauri kuanza vyakula kama uji na puree lakini watoto wengine wanaanza mapema.
 
Mtoto hawez kudhulika na chochote mi iliwahi nitokea hiyo na sikuacha kunyonyesha nilimnyonyesha mtoto hadi mimba ilipofika miez saba nikaacha kwa kuwa daktar alinambia ikifika wakat huo kuna yale maziwa muhimu kwa mtoto mtarajiwa yanatengenezwa hivyo akiendelea kunyonya atanyonya virutubisho vyote nilipo muachisha mtoto hakupata shida hata akaendelea kuwa na afya bora mpaka nilipo jifungua
 
Acha kunyonyesha haraka sana bila hvyo utamuaharibu mtt anza kumpa mtt maziwa ya lactogen 1 na akifikisha miez 6 anza kumpa vyakula lain lain
Mtoto hawez haribika mi ilisha nitokea nilibeba ujauzito mtoto akiwa na miez mitano nikashauriwa na daktar kuwa ninyonyeshe hadi mimba ikifika miez saba nimuachishe na wala mtoto hakuharibika nilimnyonyesha mimba ilipofikisha miez saba nikamuachisha
 
Dooo!, kazi kweli kweli. Ni vizuri ukawaona wataalamu wa mambo ya afya ya uzazi kwa ushauri
 
Mkuu kama hauna mshono basi usihofu kabisa maana hata kule hospital najua walikueleza kuwa uanze kufanya mapenzi baada ya miezi 4 toka ulipojifungua maana yake una uwezo wa kuwa mjamzito baada ya hiyo miezi 4.Acha hofu zisizo na msingi shida labda uwe una uwezo wa kuwahudumia hao watoto kama uwezo unao hakuna shida yoyote! pia achana na mambo ya wazungu sijui uzazi wa mpango emu jaribu kuangalia katika ukoo wenu au familia yenu unakuta mumepishana mwaka 1 na wote mmekuwa vzr tu mpaka sasa
mie ckujui hli mtapga show afta 4months! mie nljua aktoka 40 mpira unawekwa kati uwanjani,
 
Hongera sana..Binafsi mke wangu alikuwa na case kama yako..alikuwa stressful sana ila baada ya mda akazoea.akajifungua salama kwa oparation maana mtoto wa kwanza ilikuwa oparation na wa pili hivyo..

Watoto wakifuatana raha sana kwa sasa hauwezi kuona ila baadaye itaoana baraka ya ajabu sana..na huwezi kuwa na stress hata siku moja!
 
Hapo ni shida kama mtoto ameanza kuharisha it mins hayo maziwa yamekuwa machafu coz ya hyo mimba ingine mwachishe nyonyo mpe ya kopo tafuta mtu akusaidie kumlea asiwe karibu na wew mda wote joto lako litamwaribu unajua kubemenda mtoto wew?
 
Hakuna kitu kinachoitwa maziwa machafu, hiyo ni imani ya kimila, mama mjamzito anaweza kumnyonyesha mtoto wake mchanga hadi siku yakujifungua na ikiwezekana na hata baada yakujifungua (kumnyonyesha wote wawili) na yasitokee madhara yoyote na ukioona mtoto akinyonya anaharisha, inawezekana usafi wa matiti ya mama hauja zingwatiwa au tayari mtoto kashapatwa na utapiamlo
 
Do ile theory ya kuwa ukiwa unanyonyesha mimba haiwezi kushika si kwa wote, wengine wakijaribu tu ni kitu na box. Kula vizuri na kufanya mazoezi, jitahidi kutembea hata kwa nusu saa kila siku kama utaweza.

Jitahidi kubalance mapenzi kati ya hawa watoto wote, kwasababu wako karibu huyu aliyetangulia pia atahitaji kupendwa kama mwenzake. Wazazi wengi wanajisahau na attention yote inahamia kwa mtoto mchanga.
Rafiki hiyo theory inaapply Kama unanyonyesha usiku angalau mara tatu. Nimependa ushauri wako
 
Dada mnyonyeshe tu mtoto mpaka mimba itakapofikisha miezi saba na Baada ya hapo anza kumpa lishe nzuri yenye virutubisho mpende sana mwanao muweke karibu.

Mtoto ni Neema amini Mungu amemleta sasa iko sababu usichanganyikiwe hata jitie nguvu jitie Moyo utavuka na utawafurahia wanao.
 
Bado sijaenda hospitali , nimeolewa, nina mtoto mmoja tu, umri wangu ni 29 yr,
Hapa umepata ushauri mwingi wa kitaalamu,fanyia kazi,wala usiwe na hofu,maana hapa jamvini kila sampuli ya mawazo ya kitaalamu yapo.
 
Back
Top Bottom