Nilizaa na mwanamke mtoto wangu kapewa mume mwingine, nifanyeje?

ben brancoII

Member
Mar 19, 2017
40
27
Wakuu habari za usiku,

Nahitaji msaada wenu wa ushauri,

Miaka minne iliyopita nilimpa mwanamke fulani ujauzito mkoani Tanga, kutokana na pilikapilika zangu utafutaji kipindi hicho sikuweza kumhudumia kwa chochote maana nilikuwa mbali nje ya nchi na hatukuwa na mawasiliano na nilimuacha na mimba ya miezi 4.

Kuna siku moja baada ya miezi 2 kupita alikutana na rafiki yangu akamuambia "mwambie rafiki yako huyu mtoto nitampa mtu mwingine yeye kama ameamua kunikimbia atakuja kujuta"

Baada ya rafiki yangu kuniambia yale ndyo nikapata namba ya mwanamke huyu lakini nilipokuja kuongea nae akaniambia eti mtoto amempa mume wake waliyeachana kabla ya kukutana na mimi, akadai alipoona maisha magumu akamfuata jamaa akamkazia alipomuacha alimuacha na ujauzito na jamaa akakubali kwahiyo mimi nitulie nisimletee vurugu kwani damu yangu haipotei mtoto atanitafuta hata ukubwani na akabadilisha namba ya simu sikumpata tena.

Now nimerudi home Tz na ninamtaka mwanangu, Mwanza nimeamua kujenga katika mji ambao ndipo tulipokutana na akapata mimba hiyo, nimenunua eneo kwa watu ambao wanatujua vyema mimi na yeye nikajenga kakibanda, yule mtoto sasa ni mkubwa wa kuanza hata chekechea akajua a e i o u lakini anaishi mazingira magumu sana, mtoto ni copy yangu kabisa hata watu waliponiona tu naingia siku ya kwanza walisema daah jamaa kama umebandika sura yako kwa yule mtoto kuonesha jinsi gani anafanana nami.

Nikaenda kwa wazazi wa mwanamke huyu baba na mama yake wakaniambia kuwa ni kweli hayo wanayafahamu lakini wakaniomba sana kuwa haya mambo niyaache kwani wao wanaogopa aibu kijjini maana mtoto wao kashaolewa na mtu mwingine na anajua yule ni mwanae mpaka kadi ya clinic ina jina lake huyo mwanaume hivyo itakuwa ni aibu kwao kama wazazi na mtoto wao ataachwa, mwishowe wakaniambia kama nikitaka kufanya hivyo basi niwe tayari kumuoa mtoto wao, bahati mbaya nimeshaoa tayari.

Wakuu nimekuwa naumizwa sana na hali ya mtoto, bila shaka najua ni wangu, amefikia umri wa kusoma lakini hakuna mwenye habari na umuhimu wa elimu, mtoto ana mazingira magumu maisha yao ni ya dhiki sana hufikia wakati hata msosi hawapati, nguo zake zimechakaa sana na za ovyovyo, nimejaribu japo niwe namuhudumia kwa siri kupitia wao babu na bibi yake wamekataa wanadai mkwe wao atahojihoji sana na atajua.

Katika maisha yangu nina kila kitu kinachonipa furaha maishani mwangu lakini hili la mtoto linanifanya kila siku nalia machozi na hata nikifurahi nikilikumbuka hili amani ya moyo hukosekana.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu, je kuna hatua zozote za kisheria naweza chukua kumpata mtoto yule? Wakati mwingine nafikiria nimwite yule mume wake aliyempa mtoto wangu nimchane live lakini napata moyo wa huruma nitamuharibia ndoa yake. Wakati mwingine nafikiria kumuiba mtoto, lakini naogopa kuvunja sheria ila mwanamke huyu niliyezaa nae karibu asilimia90 ya ndugu zake wa kike wananitambua kama mimi ndiye baba halisi.

Nifanyeje jamani niweze kumpata mwanangu na nimsaidie aweze kusoma na kuishi kwenye mazingira ninayotamani?

USHAURI WAKO NI MUHIMU SANA KWANGU MKUU USIPITE TU TAFADHALI.
 
Je mama yake akiachika utakuwa tayari kumpatia matunzo!? Mkeo umeshamwambia kama una mtoto wa nje unataka kumchukua ili uishi naye!? Kama majibu ya maswali yangu haya mawili ni ndiyo basi andaa utaratibu wa kuchukua mwanao bila kuleta kizaazaa kikubwa. Kila la heri na baraka katika juhudi zako. Ukiweza kumchukua baada ya kufuata ushauri utakaopewa hapa lete mrejesho.
 
Duh pole sana. Kama upo tayari kumlea mtoto, pamoja mama yake punde ukweli utapowekwa wazi then go ahead udai mtoto wako, maana;
  • Si vyema kumuacha mtoto anaishi kwa mateso na probably aje kuwa wa mitaa kwa kukosa elimu na ilhali wewe unajiweza.
  • Itakuwa laana pale utakapo muingiza mama yake matatizoni na kumtelekeza. Since you did leave her to deal with what was both your mistake all alone, she surely deserves to reap the rewards of your success!
Ila mkuu duh,sasa na wewe kwanini ukaenda kujenga na kuhamia sehemu hiyo hiyo ambayo yeye na mumewe wapo?Did you not think this will complicate things even further?
 
Je mama yake akiachika utakuwa tayari kumpatia matunzo!? Mkeo umeshamwambia kama una mtoto wa nje unataka kumchukua ili uishi naye!? Kama majibu ya maswali yangu haya mawili ni ndiyo basi andaa utaratibu wa kuchukua mwanao bila kuleta kizaazaa kikubwa. Kila la heri na baraka katika juhudi zako. Ukiweza kumchukua baada ya kufuata ushauri utakaopewa hapa lete mrejesho.
nipo tayari na mke wangu yupo pamoja nami katika hili.asante sana mkuu
 
Duh pole sana. Kama upo tayari kumlea mtoto, pamoja mama yake punde ukweli utapowekwa wazi then go ahead udai mtoto wako, maana;
  • Si vyema kumuacha mtoto anaishi kwa mateso na probably aje kuwa wa mitaa kwa kukosa elimu na ilhali wewe unajiweza.
  • Itakuwa laana pale utakapo muingiza mama yake matatizoni na kumtelekeza. Since you did leave her to deal with what was both your mistake all alone, she surely deserves to reap the rewards of your success!
Ila mkuu duh,sasa na wewe kwanini ukaenda kujenga na kuhamia sehemu hiyo hiyo ambayo yeye na mumewe wapo?Did you not think this will complicate things even further?
asante kwa ushauri wako mkuu,hapo nilipojenga na wanapoishi wao ni kijiji cha pili,pia mimi siishi huko ila kuna vijana wanaishi na huwa naenda kwa wiki hata zaidi ya mara 4.

wewe unanishauri huo ukweli niuanze vipi kuuweka wazi maana wao hawataki ijulikane,au nimwite yule mume nimchane live kuwa mtoto si wake?mke akimuacha nitamsaidia sababu kosa nilianza kufanya mimi.au ungekuwa ungefanyaje
 
Ukiona hivyooo ujuee either mtonyo tatizo au siyooo wakoooo we unadhani ni wakoo si unajuaa mwanamkee ndo anamjuaa baba wa mtoto ni nan!
 
Mkuu kama una uhakika ni mtoto ni wako fanya jitihada za kumchukua.Siwezi ona mtoto wangu anaishi katika mazingira magumu kisha nikakaa kimya. Kosa alishalifanya huyo mama mtoto kumpa mwanaume mwengine mtoto na hali akijua kiwa si wa kwake.
Dai mtoto fanya taratibu za kupima DNA.Ni wazi humtendei haki mtoto na baba anayemlea ukiamua kunyamaza kimya.
 
Alikuwa na mimba ya miezi 4.

Baada ya miezi 2 ukapata contacts zake, so hapo alikuwa kama 6 minths pregnant, ok..

Ukadai mtoto akasema kampa mwingine

umeruka kitu hapo kusema ulichukuq muda gani tangu umuachw akiwa na mimba ya miezi 4 hadi ulipotaka

Kuna kitu hujaandika kueleweka, inaelekea ulifurahia ya ulipoenda na haukumtunza mtoto

Now ndio umemkumbuka, na hakuwa mke.wao so why unaandika "mume mwingine"
 
Umeshatimua mavumbi sasa unatafuta pa kuhemea,huyo mtoto kula mlo mmoja na maisha ya dhiki alishazoea tangu ulipo muacha na angali tumboni na miezi mi 4, usiwe mbinafsi wewe ulishamtelekeza tangu mimba waache na maisha yao usijitie bwana huruma kwa kuonyesha huruma na hudhuni za kinafiki,kusingizia nje ya nchi kua ni chanzo cha kuto hudumia mimba na baadae mtoto wako ni ujuha wa hali ya juu,kwani nje ya nchi ni akhera? Si ni duniani hapa hapa!? Ulikua ukifahamu kuna watu wa karibu including huyo unayemtaja kama rafiki yako je kwanini hukuchukua hatua mapemaa kupitia hao wakati wewe upo huko nje ya nchi!? Huyo mwanao believe me or not ni Diamond ajaye, ni future successful man/woman na Mungu anampitisha kwenye hayo magumu ili baadae amuinue,mwache Dada wa watu na mumewe na mtoto wao ambae wewe hukumthamini
 
Mkuu tulia tu anza maisha yako kama kweli mtoto ni wa kwako damu huwa haipotei.

Usije ukamuharibia huyo dada na ilihali wewe tayali una mwenza ila mwambie kabisa Akae akijua wewe ndio baba wa mtoto na pia uwe unachangia hata kidogo tu kwa ajili ya mahusiano mema wewe na mwanao hapo baadaye atakapokuja kutambua kuwa wewe ndio baba yake.

Huwa naamini kabisa Mwanamke hata ambambikizie mwanaume mimba ila ipo siku atakuja kumwambia mtoto wake baba yake halisi ni nani. Hata kama baba Mbambikiwa alimtunza katika viwango vyote vya Ubaba.

Kikubwa hapo Endelea na Maisha yako. Ila usikatishe mawasiliano na huyo dada ili kumjulia hali mtoto.
 
Kuna vitu vingi sana unaficha,hapa tunasikiliza ya upande mmoja ila maneno yako yanaonyesha ulimkimbia mwanamke baada ya kumpa mimba,ulimuona hafai kuwa mkeo,hafai kuzaa na wewe. Hapa unasema umeoa ina maana ulioa kabla ya kumpa mimba au baada? Umejichanganya kuwa amempa mtoto aliekua mumewe,kwan huyo mdada aliolewa akaachika kisha akaolewa tena na huyo huyo jamaa?
 
jaribu kumtafuta baba wa kufikia wa huyo mtoto mkakae naye kitako pamoja na Rafik yako na Rafik yako na huyo baba wa kambo. Kisha muongee kiume kiume Zaid na Zaid na uandae fidia km million tano hivi uumpe huyo baba wa kambo na Rafik yk umpe Laki tano. mimi Nina hakika utafanikiwa.
 
Unajifaragua mpaka unaenda kupima DNA unakuta hata wewe siyo wa kwako sijui utafanyaje!!
 
Kwani mke uliyenae amekosa mtoto? Vumilia hivyo hivyo, madhara ya kujitokeza ukidhani wewe ni jasiri kunaweza kumpoteza hata mtoto! Unajua ukweli unavyouma? Usimponze mwenzio, hasira sometimes hazizuiliki!
huyu atakuwa amekosa mtoto sasa anakumbuka kuwa kuna mtu alimwachaga na mimba, eeeh alidhani mtoto ni tv akienda dukani ananunua tu.
 
jaribu kumtafuta baba wa kufikia wa huyo mtoto mkakae naye kitako pamoja na Rafik yako na Rafik yako na huyo baba wa kambo. Kisha muongee kiume kiume Zaid na Zaid na uandae fidia km million tano hivi uumpe huyo baba wa kambo na Rafik yk umpe Laki tano. mimi Nina hakika utafanikiwa.
Milioni tano ni pesa ya ice cream haiwezi kufuta maumivu alosababisha na atakayosababisha huyu kaka.
 
I suggest, either m-face huyo mwanaume mwenzako kama ana dalli za uelewa. Kama ni ngumu, nenda ustawi wa jamii wamuite huyo mama na huyo baba wa kambo. Usitumie hasira. Maana mwisho wa siku tunaangalia maslahi ya mtoto. Kikubwa wewe usiwe mkali. Just ongea na mzazi mwenzako na ukiona hataki katu katu.. basi kajisalimishe ustawi wa jamii. Na uwaelezee kabisa wewe haja yako ni kuona mtoto anahudumiwa vizuri. Na kwa vile uwezo unao na nguvu unazo..sioni tatizo.

Hli swala halihitaji papara linaweza kutatuliwa kwa busara.
 
Back
Top Bottom