Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

MUL

Member
Oct 5, 2016
67
125
Habar zenu wana jf!! Samahani sana kwa usumbufu, naombeni msaada wenu nifanyeje mwenzenu yamenikuta nipo njia panda sina cha kufanya.

Mwanangu bado mdogo miezi minne tu sasa na tayari nina ujauzito. Mtoto kashaanza kuhara kila siku na anazidi kunyong'onyea tuu. Hospitali walimpima hana tatizo, je nifanyeje? Nawaombeni sana mnisaidie ili niokoe afya ya mwanangu.

Najua kuna watu watanitukana ila yote sawa nastahili, ushari wako ni muhimu.

Asanteni.
 
eyamango

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
464
500
Umekimbilia huku jamvini, nikuulize maswali tafadhali. Je ulienda hospitali ukawaona wataalamu wa mambo ya uzazi? Je umeolewa? Je ni mimba ya mtoto wa ngapi? Je una umri wa miaka mingapi? Je unajua maana ya uzazi wa mpango? Je afya ya mtoto inaendeleaje kwa sasa?

Ukishajibu walau maswali haya, utawapa wataalamu mahali sahihi pa kuanzia kwani humu jamvini kuna waliobobea kuhusu mambo ya uzazi.
 
MUL

Member
Oct 5, 2016
67
125
Kwani shida ni nini akifikia kujifungua huyo atakuwa na mwaka 1 na miezi kadhaa. Shida kama huyo wa miezi 4 ulijifungua kwa operation yaani kama una mshono ila kama hauna wewe fyatua tu utimize kauli ya Magufuli.
Sina operation, Ila. Hofu yangu ni juu afya yangu mimi na mtoto, maana kiukweli kupata ujauzito saivi sikupanga kabisa,
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,041
2,000
Do ile theory ya kuwa ukiwa unanyonyesha mimba haiwezi kushika si kwa wote, wengine wakijaribu tu ni kitu na box. Kula vizuri na kufanya mazoezi, jitahidi kutembea hata kwa nusu saa kila siku kama utaweza.

Jitahidi kubalance mapenzi kati ya hawa watoto wote, kwasababu wako karibu huyu aliyetangulia pia atahitaji kupendwa kama mwenzake. Wazazi wengi wanajisahau na attention yote inahamia kwa mtoto mchanga.
 
MUL

Member
Oct 5, 2016
67
125
Umekimbilia huku jamvini, nikuulize maswali tafadhali. Je ulienda hospitali ukawaona wataalamu wa mambo ya uzazi? Je umeolewa? Je ni mimba ya mtoto wa ngapi? Je una umri wa miaka mingapi? Je unajua maana ya uzazi wa mpango? Je afya ya mtoto inaendeleaje kwa sasa?

Ukishajibu walau maswali haya, utawapa wataalamu mahali sahihi pa kuanzia kwani humu jamvini kuna waliobobea kuhusu mambo ya uzazi.
.
Bado sijaenda hospitali , nimeolewa, nina mtoto mmoja tu, umri wangu ni 29 yr,
 
MpiganiaUhuru

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
780
1,000
Nachohitaji ni nifanyeje ili mtoto asidhulike kipindi hiki cha ujauzito? Maana hofu yangu ni juu ya huyu mtoto niliyenaye
Kwani bado ananyonya? Kwanza, kitendo cha kupata mimba ndani ya muda mfupi hivyo inamaanisha ulikuwa hunyonyeshi mtoto mara kwa mara maana kunyonyesha ni njia mojawapo ya kuzuia mimba. Na kama hivyo ndivyo huna haja ya kuogopa, shida ni pale mtoto anaponyonya material isiyotakiwa kwenye mwili wake, fyatua tu!
 
Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,895
2,000
Duh.!
Miezi minne. Watu mmekosa huruma jamani mpaka mtoto wa miezi minne mmembemenda? Si mngetumia hata condom. Nashindwa hata nikushauri vipi basi nenda Hospital ukapate ushauri wa kitaalam.
 
Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,311
2,000
Sina operation, Ila. Hofu yangu ni juu afya yangu mimi na mtoto, maana kiukweli kupata ujauzito saivi sikupanga kabisa,
Mkuu kama hauna mshono basi usihofu kabisa maana hata kule hospital najua walikueleza kuwa uanze kufanya mapenzi baada ya miezi 4 toka ulipojifungua maana yake una uwezo wa kuwa mjamzito baada ya hiyo miezi 4.Acha hofu zisizo na msingi shida labda uwe una uwezo wa kuwahudumia hao watoto kama uwezo unao hakuna shida yoyote! pia achana na mambo ya wazungu sijui uzazi wa mpango emu jaribu kuangalia katika ukoo wenu au familia yenu unakuta mumepishana mwaka 1 na wote mmekuwa vzr tu mpaka sasa
 
MUL

Member
Oct 5, 2016
67
125
Kwani bado ananyonya? Kwanza, kitendo cha kupata mimba ndani ya muda mfupi hivyo inamaanisha ulikuwa hunyonyeshi mtoto mara kwa mara maana kunyonyesha ni njia mojawapo ya kuzuia mimba. Na kama hivyo ndivyo huna haja ya kuogopa, shida ni pale mtoto anaponyonya material isiyotakiwa kwenye mwili wake, fyatua tu!
Nanyonyesha, na hadi hivi leo sijawahi kumpa mtoto chochote kile tofauti na maziwa yangu mwenyewe, tatizo saivi naona anaharisha
 
Top Bottom