Napenda sana mtoto, lakini najua mtoto si wangu. Ila mdada analeta ghasia. Nifanyeje? Nipo Marekani kwa sasa. Naomba ushauri

DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,654
3,327
Wadau Yamenikuta. Sitaki kuandika story ndefu sana. Lakini huyu mdada nilikutana naye nilivyokuja Tanzania na alinifanyia vituko ambavyo kwa kweli siwezi kuviandika hapa. Tokea nimwache amekuwa ni ghasia kweli. Nilishapima mimba naye na nikamkuta ameficha mkojo kwenye nguo ya ndani sababu matokeo yalikuwa negative kwa mimba mara positive ndio nikapata wazo la kumsachi na mtu hapo maabara pia akasema nimsachi. Sasa anatuma picha kwa ndugu zangu anasema nimemtekeza mtoto. Mimi kwa sasa sipo Tanzania niko abroad kwa hio hata DNA siwezi fanya.

Ila amekuwa ghasia sana. Kuna picha amenitumia NAOMBA KAMA KUNA ANYEJUA HUYO NI MTOTO WA NANI ANIAMBIE SABABU MIMI NAJUA HUYO mdada amechukua tu mtoto wa mtu anapiga picha naye. Muda aliosema amezaa mahesabu yanakataa. Na kama nilivyosema, nilipima mwezi mmoja baada ya kuwa naye mara ya mwisho akakutwa hana, akalalamika akaomba warudie vipimo, akakutwa ana mimba. Basi ndio nilivyomsachi, nikakuta ana hicho kichupa amekificha kilichokua na mkojo. Ni mdada mrembo, lakini urembo bila roho ni kazi bure.

Picha zake na ya mtoto hizi hapa. Najua huyu ni mtoto wa mtu Fulani. Naomba mnisaidie sababu ghasia zake zimezidi kwa kweli na mimi mwaka jana niliacha kazi zangu USA nikanunua tiketi ya mamilioni nikaacha shughuli zangu nikarudi Tz kushughulikia ghasia zake za mimba za uongo, na sasa sitaki KUFANYA HIVYO tena. Naomba msaada wenu wadau.

PS: Napenda sana mtoto. Ila sijajaliwa bado sababu sijapata mke bado. Ndio wadada nakutana nao kama huyu ni utapeli mtupu. Ila hata sasa hivi nasomesha Watoto watatu wa marafiki tu, kwa hio sio kwamba sina uwezo wa kumsaidia. Lakini sitaki kumsaidia mtu tapeli. Na kama nilivyosema najua hata huyo mtoto sio wake. Namba hazikubali kabisa.


NOTE: PICHA NA VIDEO ZIMEFUTWA BAADA YA KUSHAURIWA NA MDAU

Wadau: Asanteni wote kwa Ushauri Wenu. Nimejifunza mengi sana leo. Na nitafanyia kazi ushauri wa kila mtu. Naomba mniruhusu nifunge mada hii sasa. Siku njema kwenu waTz wenzangu.
 
Naweka beti kwamba kama ni mtoto wake, na hata kama ni wa jamaa mwingine. Kama ni mtoto wake tu yeye wa kumzaa NITAMLIPA YEYE MILIONI 5, NA FAMILIA YAKE MILIONI 5. Naweka bet hii sababu najua sio mtoto wake, na pia najua mimi na yeye hatuna mtoto.
 
Subiri kwanza; shida ni mtoto (kuto)kuwa wako, ndugu zako kusumbuliwa au wewe kuwa Marekani?
Shida ni huyu msichana ghasia zake. Anasumbua ndugu, anasumbua wafanya kazi wanaonisaidia Tz. Analeta ghasia ili kuharibu mambo yangu kwa kumtumia mtoto ambaye najua hata yeye hana.
 
Halafu, wewe unasema mimba ilikuwa negative, mara uliporudia ikawa postive na ulipom-search ukamkuta na kikopo.

Kwahiyo ukaridhika na majibu yapi? Kwanini msingepima damu ili waone hormonal levels?

Wewe mtu wa Marekani mwenye uwezo wa mamilioni ulienda Hospital au Zahanati?
 
Shida ni huyu msichana ghasia zake. Anasumbua ndugu, anasumbua wafanya kazi wanaonisaidia Tz. Analeta ghasia ili kuharibu mambo yangu kwa kumtumia mtoto ambaye najua hata yeye hana.
Mkuu, wewe achana naye. Hao ndugu waeleze kuwa sio mtoto wako wasisumbuke, endelea na maisha yako. Mambo madogo kama haya unayaleta JF kweli?
 
Halafu, wewe unasema mimba ilikuwa negative, mara uliporudia ikawa postive na ulipom-search ukamkuta na kikopo.

Kwahiyo ukaridhika na majibu yapi? Kwanini msingepima damu ili waone hormonal levels?

Wewe mtu wa Marekani mwenye uwezo wa mamilioni ulienda Hospital au Zahanati?
Tulipima mkojo mara ya kwanza akakutwa hana mimba. Akalalamika kwamba jamani mbona juzi tu nilikuwa na mimba nimepimwa, Basi wakarudia. Ndio ikaonekana ana mimba. Basi nikaenda laboratory ya uhakika kabisa arusha. Wakasema kabla ya damu, tufanye mkojo, ndio akawa anazingua hataki kutoa sample. Baada ya kuzingua sana nikamsachi nikakuta ameficha hicho kichupa. Na yeye kipindi hicho alikubali kwamba amedanganya na kuomba msamaha. Baada ya muda ndio akaja na hio gear nyingine. Damu ilikuwa tupime lakini baada ya kumwona ana kichupa nikaona hakuna sababu.
 
Mkuu, wewe achana naye. Hao ndugu waeleze kuwa sio mtoto wako wasisumbuke, endelea na maisha yako. Mambo madogo kama haya unayaleta JF kweli?
Nimem-ignore kwa muda mrefu sana. Lakini haachi usumbufu na ghasia aisee.
 
Just ignore her and mind your own f*cking businesses. Akiona haujali hatakusumbua tena.
Yani nimem-ignore. Na kublock namba etc. 2 years sasa tokea nimwache ila hata kwangu anakuja nk. Inaudhi sana sana. Ni tapeli mkubwa kweli yani.
 
Kumbe wewe ni muelewa ukikosolewa.
Sasa fanya hivi mtafute ndugu yoyote unae shirikiana nae mama mmoja aende akapimwe DNA na huyo mtoto.
Unae shirikiana baba inaweza kuleta shida huenda wazazi nao ndio vile ....
Kuna laboratory zipi arusha wanafanya DNA? Kama una information nitashukuru sana. Naamini Lancet laboratories wanafanya, ila ningependa kuwa na options kadha wa kadha.
 
Kuna laboratory zipi arusha wanafanya DNA? Kama una information nitashukuru sana. Naamini Lancet laboratories wanafanya, ila ningependa kuwa na options kadha wa kadha.
Hilo suala la kisheria nadhani unatakiwa mfungue shauri mahakamani au ustawi wa jamii wanaweza kutoa msaada.
Kwa wenzetu watakuwa wanapima popote bila ya kibali cha mahakama mradi ulipie pesa tu.

Kama vipi tafuta mwanasheria wa huku Bongo afungue kesi kwa niaba yako ashirikiane na nduguyo kufuatilia hili suala. Sio pesa nyingi.
 
Back
Top Bottom