Nina malalamiko dhidi ya Human Resources Officer wa TRA

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Unajua TRA ni wazembe sana.

HR wa TRA alikua na doc za mama yangu toka amestaafu 24/5/2021 na amekaa nazo tuu hajazipeleka PSSSF hadi jana tarehe 01/10/2021.

Sasa hii ni haki kweli kwa mtu aliyestaafu akitegemea alipwe mafao.

Human Resource officer anakaa na documents mezani kwake to mwezi wa tano hadi mwezi wa kumi yaani five months anakaa na documents bila kuzifanyia kazi na kuzipeleka zinakotakiwa yaani PSSSF.

Miezi aliyokaa nayo ni muda wa pension yake kumature kwa maana now angeanza kupata pension yake. Hii ni halali kweli?

Au anatengeneza mazingira ya rushwa?

Naombeni msaada hili suala nianzie wapi ili Mama yangu atendewe haki na apate haki yake.

Mtanisamehe Sana Kama Sio Pahala Sahihi Pa Kuongelea Hili Jambo Wakuu
 
All in all Kwanini hyo hr nae akae na docs ya mtu 5 months bila kuzifanyia kazi?
 
Kwani ungemjibu documents zimeshapelekwa ungepungukiwa na nini? Unapomuuliza anataka mfanye nini, una maana gani? Uko juu ya kila kitu? Unaonekana sio mtumishi wa umma kwa kuwa huna ustaarabu.
Ndio Maana sijamjibu Maana akili yake Haina Akili
 
Vitendo hivi serikalini ni vya kawaida kabisa. Hili neno la "kufuatilia" serikalini, lazima liondolewe. Bila mtu kufuatilia hapati haki yake wala jibu. Tena unaambiwa, "Fuatilia" au kuulizwa "umefuatilia?"
 
Kwani ungemjibu documents zimeshapelekwa ungepungukiwa na nini? Unapomuuliza anataka mfanye nini, una maana gani? Uko juu ya kila kitu? Unaonekana sio mtumishi wa umma kwa kuwa huna ustaarabu.
Mimi sio mtumishi wa umma, ila sijaelewa lengo la uzi baada ya document kuwa zimeshapelekwa, angeleta hii mada kabla document hazijapelekwa ingeleta mantiki, sasa anataka zirudishwe au? Maana si zimepelekwa tayari?!
 
Ukifuatilia kwenye ofisi ya umma, afisa akikusumbua taka uonane na boss wake, manager ama mkurugenzi utasaidiwa haraka.

Mama alikua anafuatilia wapi hapo hadi akawa hapewi mrejesho? Ni kwenye ofisi ya kituo chake cha kazi?
 
Boss huoni kama ndiyo unaunguza picha? Huyo HR anaweza soma huu uzi,ndiyo akaamua kuongea na wenzake wa PSSSF, wakawa wanampiga tu chenga mother, ni bora kama angevuta kwanza mpunga,ndo uje utoe lalamiko lako! Ni ushauri wangu tu!
 
Back
Top Bottom