Kwa hesma kubwa na taadhima, nawasalimu nyote wana-jf.
Mimi ni mwalimu wa sekondari niliesomea uwalimu kwa opportunity tu, na siyo "inness" yangu.
Nilitamani sana baada ya six niende kusomea muziki Bagamoyo ila Ndugu zangu walinikataza. Ninayo BA(Ed) kutoka UDSM-DUCE(2011).
NINAWEZA KUTUNGA NYIMBO KWA KUTUMIA VINA KWA MUDA MFUPI , NA IKAPENDEZA.
Naombeni msaada Ndugu zangu wa JF huenda nikatoka ki maisha, na hasa ikizingatia nina miaka 26 sasa.
Hata mawazo ni msaada.

although cwez jua unaandka nyimbo za aina gan bt nna rafk yang ni msanii if pocbl ntakuungansha nae mjue mnafanyaje. Wabongo bwana kaz kukatishana tamaa mwanzo wa safari then ikiwa poa mara ooooohh jamaa tunamjua acheni hivo
Poa sana! ila yeye anaimba nyimbo za namnagani?
tupe mistari kuhusu jamiiforum kidogo tukupime eleza chochote kuhusu jf
Kwanza kabisa
nakufunulia kurasa bila pesa.
Eti kisa natafuta nafasi , sina wasi
weupe huita chance.
Waonekana unahamu
kunifahamu
kamanawezapaa
najamii foramu.
Ujuzi wamwagika kwenye sinia
JF miii ni siniour.
Lijiunga 20 kumi na moja
na wana-like zangu hoja
ucheshi nimejaa vioja.
Nashukuru viongozi JF
sina senti
ningezawadi ka-elfu.
JF kwangu ni tukufu.
Mpenda Nchi atatoa tano
hata Mungu huunga mkono
Yangu macho kutazama MA-MODS
hawazidiwi na-loads
Kumejawa na watu makini
lakini
waajabu hawakosekani
Waletao utani jamvini
Wengine hutukana
wakihojiwa wanakana.
Wengine -super star
kutusi kwao sawa
kwenye tusi wanaweka-star
kuepuka kulamba Bann
kicheza JF unaikosa.
Makini hawato vurunda
hata wamseme nani,
Mnyika mpaka Makinda
sheria ya jamvi haitopinda.
Labda nije kilatini
"inoverata inoverunda"
Majukwaa nimengi hasa
utakosa ilipokasa
Inaongozwa na siasa.
Sijui niache hapa,
nikisema mengi tatoka kapa.
Nauliza taipata nafasi???
Weupe huta chance
kucharaza mistari
Yenye vina
nitengeneze Nina!!!!!!!