Nina Furaha kuu Rais kusaini Mswada-Ndugai

Nina Furaha kuu Rais kusaini Mswada-Ndugai

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Naibu Spika wa bunge Job Ndugai amesema ana furaha kubwa kusikia Rais ameshasaini mswada wa sheria uliokuwa unabishaniwa.

Akizungumza jana Ndugai amesema kwanza haelewi kinachobishaniwa kuhusu Mswada huo na bunge liliupitisha baada ya sheria na taratibu zote za kibunge kufuatwa.

Kuhusu kurejeshwa bungeni baada ya majadiliano ya wapinzani na Rais Kikwete Ndugai amesema kwanza wanaopigia debe suala hilo ni lazima wajiulize Je, kanuni zinaruhusu?

Kwanza sina uhakika kama mswada huu huu utarejeshwa ila ninachofurahi umeshasainiwa na Rais...'alisema Ndugai kwa Furaha.'

Source:Tanzania Daima.
 
Wameambulia aibu na fedheha tu!

Kikwete kasaini kwanza kama mwana CCM nwenzao na pili kuwaondolea aibu na tatu Kikwete nae anategemea hilo bunge kuibeba serikali yake bungeni.

Narudia wabunge wa CCM wametia aibu na wangekuwa waungwana wangeomba radhi.

Kufurahia Kikwete kusaini ni kujikosha na kujifariji tu ila ila ukweli nafsi zao zinawasuta.
 
'Mara baada ya kuwapokea Ikulu wapinzaniMh.Rais Jakaya Kikwete aliwapa Taarifa ya kusaini Muswaada huo Tarehe 10 October 2013 na wote waliafiki na ndipo majadiliano yakaanza'-Salva Rweyemamu
 
Huuu ungumbaro utaisha lini?tunataka katiba bora na sio katiba ya CCM au upinzani.
 
Kwa staili hii bora tungeendelea na utaratibu wa kuishonea viraka katiba yetu ya awali
 
'mara baada ya kuwapokea ikulu wapinzanimh.rais jakaya kikwete aliwapa taarifa ya kusaini muswaada huo tarehe 10 october 2013 na wote waliafiki na ndipo majadiliano yakaanza'-salva rweyemamu

ikulu siyo sehemu ya kutungia sheria rudini bungeni kama mnamapendekezo au hoja za msingi nendeni mkajadiliane huko.
 
Hivi hata Rais akiwaambia kijanja kwamba nimeshasaini muswada,kwa kuwa kawaambia ikulu, basi hiyo ni sawa?
 
Naibu Spika wa bunge Job Ndugai amesema ana furaha kubwa kusikia Rais ameshasaini mswada wa sheria uliokuwa unabishaniwa.

Akizungumza jana Ndugai amesema kwanza haelewi kinachobishaniwa kuhusu Mswada huo na bunge liliupitisha baada ya sheria na taratibu zote za kibunge kufuatwa.

Kuhusu kurejeshwa bungeni baada ya majadiliano ya wapinzani na Rais Kikwete Ndugai amesema kwanza wanaopigia debe suala hilo ni lazima wajiulize Je, kanuni zinaruhusu?

Kwanza sina uhakika kama mswada huu huu utarejeshwa ila ninachofurahi umeshasainiwa na Rais...'alisema Ndugai kwa Furaha.'

Source:Tanzania Daima.

Huyu ni mlevi anayeongea akiwa kwenye hang over. Ni mtu mpenda cheo na fedha asiyejali taifa lake. Huyu ni wa kupuuzwa.
 
msilete issues za mjinga huyu ni ujinga tuuu unamsumbua na ushamba wa kongwaaaaaaaa
 
Naona kuchanganyikiwa. Hii ni movie au naota. Sasa hawa ndugu zetu walifata nini huko Ufukweni Mwa bahari ya Hindi. Walikwenda kushangaa fery?.

Kwa hiyo huu MSAADA, umesainiwa tayari au Ndio umerejesha Bungeni a.k.a BUNGEWOOD, kufanyiwa script edit upya.
 
Back
Top Bottom