Nina Ekari 30, maji yapo, naomba ushauri nifanye nini nitoke?

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
982
1,546
Wakuu naombeni mawazo na ushauri wenu, mimi sio mtaalam wa kilimo nimekuwa nalima kienyeji kwa muda sasa, lakini sijapata faida ya kilimo kama ninavyosikia kwamba kilimo kinalipa kama wengi wanavyodai kwamba wametoka kutokana na kilimo.

Nina eneo, lina ekari 30, nina kisima cha maji kinanipatia maji ya uhakika, nina jenereta na pampu ya kusukumia maji katika matangi ya maji, eneo lina mazao kadhaa ya kawaida, kuna kibanda cha mlinzi muda wote yupo anayeangalia mazingira.

Eneo liko nje kidogo ya mji, wastani wa km 35 kutokea katikati ya jiji (Dar) kuelekea Mkuranga.

Nimetoa hela hadi sasa naona mfuko unaanza kutopoka, nifanyeje nirudishe hela yangu na nianze kufaidi matunda ya kilimo?

Ushauri, mawazo yoyote yanakaribiswha
 
Nakushauri ujikite zaidi kwenye "horticulture farming" yaani kilimo cha mboga mboga.

Sifa za kilimo hiki ni kwamba hakichukui eneo kubwa lakini matokeo yake ni makubwa kama utakua makini katika usimamizi.

Lakini pia unaweza ukaliweka eneo lako vizuri na kufanya kama eneo la kukodi kwa yeyote atakayetaka kulima. Kwasababu umesema lina maji.

PM kwa mazungumzo zaidi.
 
Asante kwa ushauri, unaweza kufafanua zaidi kuhusu 'horticulture farming' unamaanisha nini? Kama kuna mifano ingekuwa bora zaidi
 
Horticulture farming ni kilimo cha mboga mboga na matunda. Mifano ni kama kilimo cha matikiti, matango, mboga za majani, nyanya, hoho, n.k

Kilimo hiki kina sifa kuu moja; Hutumia eneo dogo kwa faida kubwa. Nikimaanisha kiasi utakachowekeza katika heka moja unaweza kupata zaidi ya mara tatu kama mapato.

Vile vile kilimo hiki kwa mazao mengi ni cha miezi 3-4.
 
Lima matikiti mkuu yanalipa Sana ......tena watu wananunua maeneo huko mkuranga wengi wanalima matikiti
 
hekari 35 ni nyingi sana nenda SUA Morogoro wanaweza kukupa ushauri nn cha kufanya na pia ujifunze kuhusu kilimo hata kwa kuwatembelea wakulima wenzako waliofanikiwa ambao watakupa practical experiences. Cha muhimu ni kujifunza na kufanyia kazi utatoka tu na pia usiwe mtu wa kukata tamaa

SOMA HII

KILIMO CHA NYANYA

Awamu ya Kwanza: Septemba 2015

S/No Mahitaji Idadi/Kiasi Gharama Jumla

1. Kulima shamba Ekari 1 40,000/=

2. Kuandaa matuta Ekari 1 50,000/=

Jumla ya gharama zote za kuandaa shamba 90,000/=

3. Kununua mbegu Packet 4 28,000/=

4. Kuandaa kitalu cha kusia

mbegu na kumwagilia

mbegu 5m2 10,000/=

Jumla ya maandalizi ya mbegu 28,000/=

5. Kupanda miche shambani Ekari 1 50,000/=

6. Mbolea ya samadi Trip 5 25,000/=

7. Kununua jenereta 1 500,000/=

8. Kumwagilia (mafuta) Mara 10 250,000/=

9. Kupalilia Mara 2 20,000/=

Jumla ndogo 845,000/=

10. Mbolea ya kuzalishia (CAN) Kilo 10 50,000/=

11. Madawa ya kutibu magonjwa ya nyanya 40,000/=

12. Kuvuna mara 4 100,000/=

Jumla ndogo 190,000/=

JUMLA YA GHARAMA ZOTE 1,163,000/=

Mavuno ya nyanya kwa ekari moja ikitunzwa vizuri yanaweza kufikia tani arobaini (40) sawa na madebe 2,200 ya lita ishirini. Lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, magonjwa na sababu nyingine, kiwango cha chini cha kuvuna nimeweka tani kumi na nane (18) sawa na madebe 1000 ya lita ishirini.

Debe moja la nyanya hapa Bariadi linauzwa kwa Tsh 10,000/=. Labda kutokana na mabadiliko ya bei sokoni, bei ya chini ninayoweza kuuzia iwe Tsh 8,000/= kwa debe.

Nitavuna jumla ya madebe 1,000 na kila debe nitauza kwa Tsh 8,000/=, nitapata jumla ya Tsh milioni nane 8,000,000/=.

Jumla ya mauzo yote 8,000,000/=

Jumla ya gharama zote 1,163,000/=

Jumla Ya Faida nitakayopata 6,837,000/=

JUMLA YA FAIDA NITAKAYOPATA KWENYE MRADI HUU AWAMU YA KWANZA NI TSH 6,837,000/=

Huna Milioni Moja, Utafanyaje Kupata Mtaji Wa Kuanzia?

Naomba nikutoe hofu juu ya hilo, ukiangalia kwa makini kwenye jedwali la mchanganuo hapo juu, utagundua kuwa gharama nyingi nilizozitaja ni za vibarua ukitoa gharama za jenereta, kununua mbegu, mbolea ya kuzalishia na dawa za kutibu magojwa. Gharama zingine unaweza kuziepuka kama utashiriki wewe mwenyewe kwenye shughuli hiyo bila kutegemea vibarua.

Njia Nzuri Ya Kupata Shamba Na Mahitaji Mengine

Mimi wakati naamua kulima nyanya sikuwa na shamba la kulima, nilizunguka zunguka huko kijijini nafuta shamba la kulima angalau ekari moja. Haikuwa kazi rahisi wala sikufanikiwa kupata shamba kabisa. Baadaye nilimkuta mzee mmoja anashamba zuri sana lenye rutuba na liko karibu na bwawa la maji. Nikaongea na mzee huyo na kumwomba kama ataniruhusu niungane naye kulima nyanya, tuupanue mradi uwe mkubwa zaidi. Nikampa maelezo mengine mengi nikamweleza faida atakazo pata, hatimaye mzee akakubali. Kwa njia hiyo nikawa nimepata shamba bure na mbolea ya samadi ya bure maana mzee anafuga ng’ombe. Gharama pekee ni kuisafirisha mbolea kuipeleka shambani. Kupitia ushirika huo nilioupata japo sikuwa na mwenyeji hata mmoja, sasa ninauhakika kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa.

Njia Hii Aliitumia Rafiki Yangu Na Akafanikiwa.

Tumia Njia Hiyo Utafanikiwa Tu

Kama mimi nimetumia njia hiyo na nimefanikiwa, kama rafiki yangu alitumia njia hiyo na akafanikiwa na wewe tumia njia hiyo upate mahali pa kuanzia nina uhakika utafanikiwa. Kumbuka kutafuta pesa ni mchezo, cheza kwa furaha, bila hofu moyoni mwako hakika utashinda na kufanikiwa.

Mbegu Gani Ya Nyanya Nzuri?

Baada ya kuuliza uliza watu wengi na wataalamu wa kilimo, wamenishauri nilime aina yaMwanga. Wanasema ina mavuno mengi na ganda lake ni gumu na inavumilia magojwa mengi. Mahali unapoishi ulizia nyanya aina gani inakubalika sokoni, utapata jibu. Mbegu zingine nilizozikuta madukani ni Tanya, Cal J, Tengeru 97, Iffa, Mkulima, Maoney maker na nyingine nyingi. Fanya utafiti wako ujue ni ipi inafaa.

Tulime kwa pamoja

“Kama mimi nimetumia njia hiyo na nimefanikiwa, kama rafiki yangu alitumia njia hiyo na akafanikiwa na wewe tumia njia hiyo upate mahali pa kuanzia.
 
Nina imani utafanikiwa...mpaka hapa umekwishapata ushauri mzuri.....Horticulture.Usikubali kabisa lile zao la yule mbunge wa CCM .......na nyie ccm wafundisheni wabunge wenu huu ni wakati wa juwa seeious.
 
Naomba utupe mrejesho wa mauzo ,soko likoje?

shamba kubwa sana. tenga hata 20 acres upande michungwa na embe za kisasa zile kubwa na zenye nyama nyingi. mpe hi faizafoxy
 
Wakuu naombeni mawazo na ushauri wenu, mimi sio mtaalam wa kilimo nimekuwa nalima kienyeji kwa muda sasa, lakini sijapata faida ya kilimo kama ninavyosikia kwamba kilimo kinalipa kama wengi wanavyodai kwamba wametoka kutokana na kilimo.

Nina eneo, lina ekari 30, nina kisima cha maji kinanipatia maji ya uhakika, nina jenereta na pampu ya kusukumia maji katika matangi ya maji, eneo lina mazao kadhaa ya kawaida, kuna kibanda cha mlinzi muda wote yupo anayeangalia mazingira.

Eneo liko nje kidogo ya mji, wastani wa km 35 kutokea katikati ya jiji (Dar) kuelekea Mkuranga.

Nimetoa hela hadi sasa naona mfuko unaanza kutopoka, nifanyeje nirudishe hela yangu na nianze kufaidi matunda ya kilimo?

Ushauri, mawazo yoyote yanakaribiswha
Mkuu fuga samaki baada ya miezi utakua mtu mwingine kabisa
 
Ingia Kilimo Biashara Facebook page kuna wadau pale ni wakulima wazuri tu ongea na Sheigo atakuunganisha na wakulima wazoefu na ushauri mzuri tu free of charge
 
Back
Top Bottom