Nimwambie Ukweli?

Nimwambie Ukweli?

Na hata kama unapenda mtu hadi unakua huoni unaangalia na hapo unapopenda

Alipaswa ajifunze kumuacha aende

Madame S
Watu wauachie moyo usukume damu, kupenda siku hizi yapaswa mtu aihusishe akili...
 
Ngoja upate ulemavu kwa ajili ya kipigo ndio akili zitakurudi.

Unaonekana unapenda vitu vya bure sana wahenga wanasema vya bure vinaua.

Kuna mdada aliharibiwa kizazi alisimulia humu ndani kisa cha wanaume wenye gubu kama la huyo man" baadae akamuacha sasa na wewe ngoja yakukute ili upate ajili.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna watu wavumilivu wa uvundo ukisingizia mapenzi mie hata aombewe msamaha na Mzazi nikisema sitaki ni full stop huu ujinga kuendekeza sijui ananitia vizuri anajali ni ulimbukeni daraja la 1
Atakuvunja mbavu au aje akupige ukiwa na Mimba ukatolewe kizazi akukimbie akaoe kigori mwingine
 
Pole sana kama bado unampenda itabidi ukomae na msemo wa wahenga "ukipenda waridi shutu uvumilie miiba"

Utarudi atakudunda tena utaondoka atakuomba msamaha utarudi mchezo huu mpaka lini sababu unampenda tu?

Mwishowe akuvunje mahali upate kilema bure!!

Madame S
Nikilinganisha mapenzi anayonipa na yale niliyoyapata kwa X wangu namwona kama alitumwa anipe faraja ya mapenzi.Lakini hivi vipigo ndio vinanikimbiza.
Naogopa kumwacha moja kwa moja alafu nikakutana na mwanamme kitombi kama yule niliyeachana naye.
 
Pole na matatizo yaliyokukuta. Binafsi naona kuwa mtu huyo unamfahamu vizuri tabia yake maana alishaionyesha toka mara ya kwanza mlipokutana lakini ulimpenda na mkaenda mbele zaidi mpaka ukahamia kwake, amekuwa akikukosea kwa kukupiga na kukunyanyasa mara kwa mara kutokana na wivu wa kimapenzi.

Hivyo unatakiwa ujuwe kuwa hiyo ndiyo tabia yake halisi na tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili (hata kwa mkorogo). Sasa pamoja na yote hayo bado unakili kuwa UNAMPENDA na hujui la kufanya mpaka unatuomba ushauri. mimi nakushauri USIKILIZE MOYO WAKO MAANA UNACHOMPENDEA UNAKIJUA MWENYEWE ila ningekuwa mimi ningeachana naye bila kugeuka nyuma.

HUU NI USHAURI TU. MAAMUZI UNAYO MWENYEWE
Ahsante kwa ushauri wako.
 
Kosa kubwa ulilolifanya mara ya kwanza ni kukubali kurudiana nae baada ya kuwatumia ndugu zako kukushawishi.

Utabiri wangu: Kosa kubwa unakaribia kulifanya baada ya kusikiliza moyo wako unataka nini bila kujali kwamba mwili utaumia (mateke na magumi)

Ushauri wangu: Usirudie lile kosa la mwanzo.
Niliamini atabadilika
 
Duh! Nenda police haraka mapenzi hayawi hivi ya vipigo vya kufa mtu kila mara. Nina hakika umeficha kuhusu kuumizwa kwa vipigo mara nyingi na kuishia kujiuguza au kwenda hospital na kudanganya madaktari. Waambie ndugu zako kisha kamripoti polisi vinginevyo anaweza kukuua huyu. Wivu kwenye penzi ni kitu muhimu lakini si wivu wa kiasi hiki. Kwa faida ya wengine ni vizuri huyu ukaweka ID yake hadharani hayo ni mawazo yangu ambayo wengine wanaweza kutoyaafiki.


Habari zenu?
Mimi ni member mkongwe humu.Nimebadili ID baada ya Id yangu ya zamani kubadilishwa password na 'kutekwa' na mwanamme alokuwa Mpenzi wangu.

Sitopenda kuitaja kwa kuwa ameshabadilisha user name na sihitaji kujitafutia matatizo kwa Kuwa hata huu uzi atausoma.Najua dude ninaloliamsha sio la dunia hii lakini nimeamua kama mbwai na iwe mbwai!

Nije moja kwa moja kwenye mada.Nimekuwa na mpenzi wangu huyu kwa muda wa miaka miwili.Kwa kweli mapenzi yetu yalianza kama utani tu humu jukwaani.Nakumbuka ilikuwa mada nachangia.Akani' quote' aisee mwanamme mkorofi huyu,alinitukana matusi ambayo sikujua chanzo chake.Kisa nilitetea mwanamke kuomba hela kwa mpenzi wake.
Sikumjibu mkurya yule.

Ikawa tabia yake akikuta hata like tu lazima ani harass!Nikawa namu ignore.Kitabia mimi ni mpole sana siwezi kujibishana.Nakumbuka mara ya mwisho yalinishinda nikamvaa na mimi hapa,libeneke lilichezwa nikaambulia ban ya mwezi.
Ban yangu ilivyoisha akanifuata Pm kwa upole akaniomba msamaha.Nikajikuta tu namsamehe.Mawasiliano yalianza na kupamba kasi kwa mwendo wa farasi.
Tukawa karibu mno mpaka baada kama ya mwaka hivi ndio nikawa huru japo kutoa namba yangu maana kwa kipindi hiko nilikuwa nimetoka kuachana na mtu sikutaka ukaribu wa haraka.
Baada ya kuonana na mawasiliano ya karibu sana tukajikuta tunapendana.Kwa kweli sikuwahi kujua kama kuna wanaume wakarimu kama huyu kaka nimwite 'Y'.

Yani He was so romantic,charming and loving.Alinipa madeko,alinipa mapenzi ya hali ya juu.Muda wa libeneke nilikuwa naomba 'po'.
Alikuwa mshauri wangu,rafiki yangu.
Nitake nini nisipewe,tofauti kabisa na nilivyomchukulia.Alinihamisha Sinza akanipeleka Mbezi karibu na kwake na kodi juu yake.Zaidi aliwapenda ndugu zangu wote alopata bahati ya kuwafahamu.Alikuwa sio bahili juu yangu kabisa.

Sikuwa mwepesi kutaka kumpeleka kwetu wala mimi sikukubali anipeleke kwao kwani niliwahi mpaka kutolewa barua ya uchumba alafu uchumba ukaisha baada ya mwanamme nilokuwa naye kuzaa na rafiki yangu kipenzi.

Jamani nilipohamia karibu na 'Y' ndio nilijua kama maharage ni mboga au kiungo cha makande.
Alinipiga marufuku kupitia kokote nikitoka kazini.Hataki marafiki wala jamaa.
Nikae ndani nipike nile nilale.Kazi yake ilikuwa inamkeep bussy mpaka saa tatu usiku basi lazima aje,aniangalie mara nyingi alikula.
Nikasema ngoja nitii.Nikaachana na marafiki nikawa mtu adimu hata kwenye masherehe ya watu sitokei tena.
Akija atakagua simu,emails tena akiwa very calm.
Jamani akikuta namba ngeni nitawekwa kikaangoni!Nilimweleza mimi sio mtu wa namna hiyo wala siwezi kumsaliti.
Jamani akawa anafanya ambush sasa,mara aje kimya kimya kama jambazi,mara aje dirishani mpaka akawa ananistua.Alivyoona haitoshi akaniomba nihamie kwake.Sikukubali nikawa nalala kwake mara nyingi kwangu nafunga.Mpaka siku nikavunjiwa mlango wa mbele na kusombewa kila kitu.

Hapo ndio akapata kisingizio cha kunihamishia kwake.Nilivyohamia kwake akazidisha wivu.Akipiga simu mchana kama inatumika nikirudi jioni nazabuliwa kama mtoto.Kitu kidogo mpaka anipige vibao.Nilikaa naye chini mara nyingi na kumweleza kutoridhishwa kwangu na ile tabia.Lakini hakuacha,nisipojisikia sex ngumi.Nikipigiwa na mwanamme ngumi.Nikapoteza furaha na nuru kabisa.Nikaamua kumuacha.
Nikaendelea na maisha yangu.Nikamblock kila mahali.Akija sifungui aisee mlango utapigwa mateke mpaka nafungua akiingia anaomba msamaha.Nikaamua kuhama baada ya usumbufu kuzidi.Sio kwamba nilikuwa simpendi ila mateso yake yalizidi.Kipigo jamani.

Akawatumia ndugu na rafiki zangu.Nikakubali turudiane ila sikutaka kurudi kwake.Sasa akahack kila kitu changu.Akadai anataka kuwaona wazazi.Moyo ukasita.Jamani Y alizidisha wivu hadi message za kuforward anakasirika.Ananipiga na bado sex anataka.
Nilishindwa kwa kweli.Namiss treatments na sex lakini nikikumbuka yale mateke na mangumi nashindwa.
Sijui nifanyeje ananistalk kila mahali mpaka kazin muda wa kutoka unamkuta Getini.Sina raha bila yeye nampenda lakini naogopa kumrudia hawezi kuacha kunipiga kabisa.
Naomba ushauri wenu.
 
Naam nakumbuka ule uzi katichi alikuwa na bahati hakupoteza maisha lakini kupoteza kizazi nalo ni jambo kubwa sana.


Ngoja upate ulemavu kwa ajili ya kipigo ndio akili zitakurudi.

Unaonekana unapenda vitu vya bure sana wahenga wanasema vya bure vinaua.

Kuna mdada aliharibiwa kizazi alisimulia humu ndani kisa cha wanaume wenye gubu kama la huyo man" baadae akamuacha sasa na wewe ngoja yakukute ili upate ajili.
 
Back
Top Bottom