Ambition plus
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 7,090
- 13,527
Habari za midaa hii wana jamvi,
Nitangulie kwa kuwapa pole ambao mama zao wametangulia mbele za haki (wapumzike kwa amani). Pia, wasio na mama ama wamelelewa na mama wa kufika (pia ni mama) haijalishi wamekulea kwa namna gani.
Nimekaa leo ni siku ya tatu natafakari "nimnunulie mama zawadi gani". Mimi na mama yangu tumepishana miaka 22. Mimi niko 30 early. Ni kwamba ukiangalia siyo mkubwa wakutisha (nikiwa kama mtoto wake pekee). Mama yangu ni mpambanaji sana, na hapo alipo hanitegemei kwa chochote. Kama nikimpa "pesa"ni kwa mapenzi yangu na lazima ataniuliza ni ya nini.
Kama zawadi nimewahi mnunulia nyingi kama viatu, pochi, nguo, saa, vikoi, tiketi za matembezi na vingine vingi. Baadhi ya nilivovinunua havai, hatumii wala hagawi. Viko tu anaviangalia ndani kwake.
Sasa nawaza nimnunulie nini kama zawadi nimfurahishe mama yangu, niuguse moyo wake. Tafadhali nishauri sifikirii kitu kikubwa.
Tafadhali nishauri.