Nimnunulie mama zawadi gani?

Nimnunulie mama zawadi gani?

Mi mwenyewe mwanaume mwenye ivo vi baby walker anatembea amening'iniza ufunguo huwa namshangaa
Mungu akuongezee miaka mingi ya kuishi bibie.Mana unatupa hasira ya kuzidi kuzisaka.
 
Okay wacha nikujibu mkuu

Mzee wangu yupo..
Sawa,wapo pamoja (mke na mume) na wana maelewano mazuri? Kama ndiyo, ulishajaribu kuwapa zawadi ya pamoja au kwa wakati mmoja? Kama hawapo pamoja nieleze, niseme kitu,zingatia mimi ni umri wa kutosha wewe kuwa mwanangu.
 
Tusichotambua ni kuwa kwa mama zetu kila tunachowafanyia kwa upendo kwao kina thamani kubwa sana. Ndio maaana unaweza kumtumia mama yako sh.10000 akakushukuru na kukuombea sana, ila gf/mke anaweza hata asishukuru au akaona kama dharau.

Si unaona zawadi ulizomnunulia hazitumii wala kugawa!! Hiyo ni ishara kuwa anazithamini na anatamani kuziona kila wakati hivyo hataki viharibike. Sasa kaa nae mara kwa mara muwe mnazungumza, lazima utajua kuna kitu anatamani kuwa nacho au kukifanya ila hana huo uwezo. Then kama kipo kwenye uwezo wako mfanyie.

NB: zawadi yoyote utakayompa kwake inathamani kubwa.
genius
 
mtafutie hafla maalumu ktk siku yake maalumu mfano siku yake ya kuzaliwa andaa sehemu patengeneze Kwa bashasha ya jina lake na ujumbe wa unaomuonyesha kiasi gani unamthamini tena hivi vyote unamfanyia kwa surprise Iyo siku. Mkuu iyo siku ukimpa ata zawadi ya kitenge hatoisahau katika maisha yake hasa ikifika siku ya tarehe kama hiyo kila mwaka. Na iyo siku kumkumbusha sana moments za kitambo alizowahi kukufanyia za kudhiirisha upendo wake kwako.
 
umenikumbusha[emoji1787] kuna siku nilikua naangalia Mieleka na mama Mtu akimpiga mwenzie , utaskia wewe inuka mbonde huyo[emoji23][emoji23][emoji23] akiinua akimpiga utaskia eeh safi kabisa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]such a beautful moment ever
Nilikua nikienda kumsalimia mama siku za weekend nikagundua anapenda sana kuangalia mieleka.

Hata kama tulikua tunaongea mambo ya maana mieleka ikianza maongezi inabidi yaishe tu maana focus yote anaihamishia kwenye mieleka.

Nikagundua king'amuzi anachotumia ni cha hovyo sana maana walikua wanaweka mieleka ya zamani sana.

Siku moja nikajichanga nikamnunulia dstv na kifurushi cha miezi mitatu. Kwakweli mama alifurahi maana alikua anaangalia mieleka live.

Kuna ndugu yangu anakaa nae huwa ananipigia simu ananiambia nimemuweza mama maana siku hizi yupo bize na mieleka na anawajua wapiganaji wote. Mimi huwa nafurahi tu nasema acha mama afurahi.
 
Sawa,wapo pamoja (mke na mume) na wana maelewano mazuri? Kama ndiyo, ulishajaribu kuwapa zawadi ya pamoja au kwa wakati mmoja? Kama hawapo pamoja nieleze, niseme kitu,zingatia mimi ni umri wa kutosha wewe kuwa mwanangu.
Wako pamoja.Mzee ni mtu wa kusafiri sana.
 
Back
Top Bottom