Nimkwepe vipi huyu mama ntilie?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,879
15,459
Wakuu,

Kuna mama ntilie flani hapa Arusha kaniganda hatari,nilikuwa na lengo la kuchapa tu na kuingia mitini,lakini naona kaniganda na hana mpango hata wa kuachana na mie.

Kiumri kanizidi kama miaka mitano,ana mtoto mmoja wa miaka 7,elimu kaishia la saba,sasa mimi mtu wa hivyo nimpeleke wapi wakuu.

Nipeni mbinu za kumkwepa kisayansi.
 
Wakuu,kuna mama ntilie flani hapa arusha kaniganda hatari,nilikua na lengo la kuchapa tu na kuingia mitini,lakin naona kaniganda na hana mpango hata wa kuachana na mie.kiumri kanizidi kama miaka mitano,ana mtoto mmoja wa miaka 7,elimu kaishia la saba,sasa me mtu wa hvyo nimpeleke wapi wakuu.nipeni mbinu za kumkwepa kisayansi.
Wewe una PHD mpaka unamuona huyo wa darasa la 7 huna pakumpeleke? mbona kabla hujamvua nguo hukuangalia umri wala darasa wala mtoto alokua nae later ndio umejua yote hayo? wacha kujifanya ukoo juu kuliko mwengine,type yako ndio hizo za mama ntilie sasa kama umepata mwengine nenda usije ukachelewa lakini usimfanye huyo mwanamke kama anakuhitaji sanaaa,ebu mwambie sikutaki na mpe sababu kama ulosema halafu uone mziki wake...
 
Wewe mwenye elimu kubwa kutwa upo mitandaoni kutunga vijistory vya uongo. Unadharau darasa la saba wakati wewe umemjua kupitia hiyo kazi yake. Kwani hiyo sio kazi halali?. Pia yeye kua darasa la saba hakuondoi ubinadamu wake, mbona kwenye mitandao tumemuona msomi wa PHD analalamika maisha ya mtaani yalivyo magumu?
 
Back
Top Bottom