Nimfanyie Nini huyu Mwanamke?

Nimfanyie Nini huyu Mwanamke?

Hello,

Nimekuja kwenu ndugu zangu naomba mnipe mawazo yenu, naomba mnishauri kama ndugu au rafiki yenu. Sitaficha chochote.

Nilimaliza chuo miaka kama 5 iliyopita nkapata kazi private after two years kazi ikaisha.

Nilifungua bihashara ikadumu mwaka mmoja then ikafilisika, baada ya hapo nilipigika sana. Nilipigika Ile aswaaa, nilikonda Hadi mahitaji muhimu nilikosa.

Mwaka 2023 Kuna Binti tulikuwa tunafahamiana muda ila mwaka huo tukakoleza mawasiliano, huyu Binti tuliishi mikoa tofauti. Na nilimficha Hali yangu ya maisha.

Basi sijui uyui Binti alikuwa na upwiru au barehe, she was around 23yrd by that year. Yule Binti alinipenda hatari na sikuwahi mtumia Hela.

Kimbembe kikaja anataka niende mkoani kwake, hapo alikuwa kapata kazi private,,, basi mtoto alitaka sana niende mkoani kwake lakini sikuwa ata na mia. Nilikwepa nkakwepa ila mwisho nkaamua kusema ukweli kuwa sina ata mia.
Alipokuwa anaenda kikazi hakusita kumuachia Hela ya matumizi na zawadi kama zote

Mala paaa Binti akanitumia nauli, ikabidi niende mkoani kwake, nilipofika alinipokea vzr mnoo. Usiku ulipofika lah hau lah nilikuta Binti ni BIKRA hajawai fanya mapenzi.

Daa basi nkamtoa BIKRA yake nilikaa wiki then Binti akanipa nauli nkarudi mkoani, baada ya mwezi Binti alikuwa ameapply ajira za Tamisemi, akapangiwa kazi serikalini.

Kwa kua sikuwa na mia nkamshawishi Binti nimsindikize afu ntafute fulsa uko alikopangiwa. Kumbuka sikuwa na mia mfukono, tulivyofika uko alikopangiwa sikuwa na mishe yeyote,binti akawa anaenda kazini mie nabaki Ndani. Nilikaa na yule Binti silipi chochote sio Kodi, umeme,maji, chakula Kila kitu alikuwa analipa Binti.

Yule Binti alinistili sana, tulikuwa tunaishi kisera hatukutambulishana. Nikiri nilimpenda sana yule mwanamke. Baada ya miezi mitano yule Binti alipata mimba, aisee yule bidada alichanganyikiwa hatari.

Yaani alipata kazi akiwa mdogo na kwao wazazi wake ni viongozi wa dini, yule Binti alimanusra awe crazy,, alitaka kutoa nkagoma ,kazini kwao walikuwa wanampiga majungu kuwa atatokaje na jobless, Yaani alikuwa kama kachanganyikwa, lakini badae alitoa Ile mimba.

Then after nilipata kikazi private nkahama halmashauri nyingine,,baada ya kutoa mimba ni kama tulipata raana,, Yaani mahusiano yalikosa amani Kila siku ni ugomvi, ugomvi, ugomvi, baada ya miezi michache tukaachana

Baada ya kuachana niliumia hatari, nkaendelea ku fight,na mimi Mwenyezi Mungu akanibariki nkapata kazi nzuri tu.

Sasa Kila nkikumbuka fadhila,wema, na kunistrili Kwa yule Binti huwa natamani nilipe ata fadhila kidogo Kwa yule Binti. Yaani nilidate nae Hadi tukaachana sikuwai kumnunulia ata chupi, lakini sio kwamba nilitaka Bali ni umasikini niliokuwa nao.

Sahivi tunawasiliana fresh tu, anasisitiza bado yupo single.

Wakuu nilitamani nimnunulia zawadi yeyote huyu Binti Ili nilipe fadhila za wema alionitendea.

Je angekuwa ni wewe ungemfanyia Nini huyu Mwanamke? Au nivunge tu ihesabike alijitoa tu kwangu kama msaada hakuna aja ya shukrani.

Msaada jamani

N.B mie sio mwandishi mzuri.
Unaona, hata kuoa bikra si grantee ya kutoachana
 
Uyo rudiana nae oa ni mke uyo, hadi sild umetoa ww, unataka nini tena na yupo single kuishi nae km mume ukamtreat fresh ni zawadi kubwa kuliko zote
 
Naomba niwe kama Da mwadawa! WE KOMA WEWE KOMA KABISA!!!

Yani Ninja sikufichi kama huyo mwanamke humtaki tena kwenye maisha yako Tukipiga mahesabu ya kukutumia nauli mara 2 na kukulisha miezi 12 tukiweka na Riba mnunulie hata IST Used! Kwa jinsi wanawake tusivyo na hela! Aisee Chukua fungu hata milion 2 mpe na utakua umepoteza mke bora kwako na kwa mume mwingine atakaempata mana hatokaa amtende wema mwanaume mwingine!
Wanaume ndo mana skuizi mkioa tu mnakufa nawaambia kwa style hii.mtakufa sana!
 
Alikuwa mwanamke sahihi mwanzo kitendo cha kutoka mimba mkaanza ugomvi ngumu kuwa Sawa tena
 
FB_IMG_1755926504719.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom