Nimfanye nini huyu office-mate?

Nimfanye nini huyu office-mate?

The truth will set u free,mwambie huyo office mate kwamba what she is doing isnt right and kama she doesnt behave or change ni bora uvunje huo urafiki...,itsn't worthy kabisa cheating n destroying ur marriage over something which u might regret entirely for the rest of ur life.

Thanx a lot! advice appreciated
 
anza mtindo wa kumsifia sana mkeo na kumpigia simu kwa kumbembeleza mkeo maneno matamu.na hata mkeo anapopata nafasi mkaribishe akutembelee ofsn. huyo bidada atakata mazoea na kitamuumiza sana..
 
anza mtindo wa kumsifia sana mkeo na kumpigia simu kwa kumbembeleza mkeo maneno matamu.na hata mkeo anapopata nafasi mkaribishe akutembelee ofsn. huyo bidada atakata mazoea na kitamuumiza sana..

nishamleta ofisini si mara 1, ni zaidi ya mara 3 lkn haijasaidia! labda nikuulize situation kama hii inafaa kuisimulia hm kwa yf ama?
mimi mke wangu
 
anza mtindo wa kumsifia sana mkeo na kumpigia simu kwa kumbembeleza mkeo maneno matamu.na hata mkeo anapopata nafasi mkaribishe akutembelee ofsn. huyo bidada atakata mazoea na kitamuumiza sana..

Code:
mimi mke wangu nishamleta ofisini si mara 1, ni zaidi ya mara 3 lkn haijasaidia! labda  nikuulize situation kama hii inafaa kuisimulia hm kwa yf ama?
 
.............tena UNAENDELEA huku unalia kwa uchungu, na ukimtaja jina lake..mfano kama anaitwa Fausta.......basi unalia huku unalalama kwa machungu.............kweli Fausta siku zote nakuheshimu kama dada yangu lakini unathubutu kunifanyia hivi...kweli..kweli Fausta.....sio vizuri ujue....shindwa Fausta....shindwa Fausta...shindwa Faaaaaaa....aaa....aah...aaah......aaahhh.......pfuuuuuuuh......na baada ya kumaliza endelea kulia kwa machungu kwa dakika kadhaa.....

.....nakuhakikishia baada ya hapo atakukoma.
PHP:
daah, itabidi nianze na reahearsals za kutosha
 
ndio video ya aina gani hiyo? nataka kufahamu

hii inaoyesha ni jinsi gani pilau inavyopikwa...labda slim5 atueleweshe zaidi maana hata mimi sielewi!!
 
Last edited by a moderator:
Na ukichelewa anakubaka ofcn ndio ukome...maana ishara zote keshamaliza.
 
Tunga stori ya dem mtaani anayekutega then muelezee huyo ofc mate. Wakati unamuelezea ponda mbaya tabia ya wadada kukutega na jinsi ambavyo huna mpango wa kumcheat mkeo na msifie mkeo sana... yani full kufagilia ataupata ujumbe. Elezea jinsi ambavyo unawadharau wanawake wanaojileta kwako huku wanajua umeoa yaani haribu. Asipoelewa tena basi katumwa!
 
Mpotezee tu akakuuliza kunanini hapo mwambie ukweli jinsi anavyokukera.
 
Kwani mkuu huyo Dada kaolewa? Km ajaolewa mfanye ile nyumba ukiingia lzm uiname
 
Nimecheka pale kwenye tabia za watu wa mkoa ambao hautakiwi kutoa "mkulu" wa kaya, kwani tabia zao zikoje?
 
Wana - JF nawasalimu sana!

Mwenzenu nina mtihani! Hapa ofini kwangu ni na bidada mmoja (ni mrembo wa haja tu, anatoka ule mkoa karibu na Dodoma na wadada wa mkoa huo wana ile sifa kama ya ule mkoa wa kanda ile isiotakiwa kutoa Mkulu). Ni mfanyakazi mwenzangu, tuliajiriwa mwezi mmoja, tumeishi kwa miaka mi3 kama kaka na dada, huku tukiheshimiana sana! Kama mnavyojua ofisi za serikali, huwa tunashirikiana sana katika mambo mengi sana ya kiofisi kuanzia kushare stories mpaka kupeana ushauri, asipokuwepo nafanya kazi zake, nisipokuwepo anafanya kazi zangu! Tunashirikiana ktk NIDO, majani ya chai, maji ya kunywa, vitafunio - hivi huwa tunapewa na ofisi, mpaka nauli!

Katika lunch pia hivo hivo, nina hela namuagizia lunch box, na yy akiwa nazo hivo hivo! Yaani tumekuwa dada na kaka wapenzi mpk ofisi zingine wanatuonea wivu! Wakati ofisi zingine wanashindana umbea na majungu, sisi kwetu ni kupendana na kujaliana! wakati mwingine majungu yakiwazidia wenzetu huwa wanakuja ofisini kwetu kupata relief!

Mimi nimeoa na yeye ameolewa! Mwenzangu ndoa yake ina mtihani, hawajabahatika kupata mtoto! Bahati mbaya ni kuwa, bi dada umri umeenda! Mimi amenizidi 2 years! Mimi kwa upande wangu mungu amenijaalia watoto wawili! Mwanzoni kabla sijamsoma, ilikuwa rahisi mimi kumueleza ama kupiga story kuhusu watoto, reference kwa wanangu! Kumbe mwenzangu moyoni alikuwa anaumia sana! ktk story zote tunazopiga, hizi za watoto hazipendi! zinamchoma! Baada ya kujua na mimi nimeacha kumuelezea lolote lile kuhusu watoto wangu! Hata kama naenda hospital kupeleka mtoto, basi yeye nitamuambia naenda k'koo ama posta, ili tu nisimuumize!

Sasa balaa ni hili hapa! Kaja na mpya!
Alianza kwa kuntumia video ya PILAU whatsapp! kwa kuwa ni mtu ambae uhusiano wetu haukuwai kufikia ktk kutumiana vitu km hivo, nikashtuka! nikahisi kakosea wa kumtumia! mimi sikumjibu bali nikai-delete fasta kabla mama nanii hajaiona! nikasubiri sms yake ama call ya apology! kimyaaaa! Baada ya siku kama 3, akanambia samahani ile video haikuwa yako, nilikosea kukutumia, nikamuambia sawa ila kuwa makini!

Hapo kabla alikuwa ni mpenzi wa sketi ndefu na blauz za kuficha matiti, siku hz ni mwendo wa vimini na blauz za manyonyo nje! Mbona nakoma mwenzenu!Siamini kama ananivalia mimi ama mwengine, lkn kazi ninayo! Na pia kesi za kuitwa nikamsaidie kitu ktk computer yake sk hz zimekuwa kibao, hasa za kumwelekeza program mbali mbali, tena wkt mwingine anakuja kwangu kuniinamia nimuelekeze, nakomaje! manyonyo yote, tiiii kwangu!

Likaja la kuonyeshwa chachandu! mimi sijui kama tangu zamani anavaa ama ameanza kuvaa siku hz, na kama anavaa siku hz, ananivalia mimi ama mr wake, mm sijui! ila kila siku naonyeshwa chachandu, lazima nionyeshwe chachandu, kama si asubuhi basi mchana! na anajua style nzuri za kunionyesha chachandu zake! tena anajua kuchagua, zinamkaa vzr kweli kiunoni! (bahati mbaya hajui kama mimi ni ugonjwa wng, hii bidhaa mimi huwa naumwa nikiiona! daah kila m'me na madhaifu yake jamani)

Yote kwa yote mimi si mfuasi wa michepuko! Na bado tunaheshiana sana, japo nimeshaanza juhudi za kupunguza mapenzi ya udada-ukaka ili huko mbele yasije yakawa mazito! Shida yangu wanaJF, naomba mnisaidie njia sahihi ya kumuomba kama ananitega, basi mimi hapana, siko huko! anionee huruma, coz mateso ninayopata, kila siku nakuwa wa kwanza kusepa ofisini na wa mwisho kuingia, na hii inanipunguzia ufanisi kazini! Nambieni nitumie njia gani ili nimrekebishe na turudi ktk undugu wetu kama zamani, nia yangu ujumbe umfikie japo naogopa mashushu ya bimdada! Msaada jamani!

Mshirikishe hii thread akiisoma atakuwa kaelewa.
 
Back
Top Bottom