Nimfanye nini huyu office-mate?

Nimfanye nini huyu office-mate?

Si unataka asikusumbue tena? nakushauri sasa,chukua ushauri wa wadada wa humu jf coz wao wanajua mambo yanayowakatisha tamaa
wakifanyiwa na wapenzi wao au wale wanaotaka wawe wapenzi wa baadaye,
ukichukua ushauri wa ''me'' wenzio utakupeleka pabaya
kwa heri.
 
pole, naona kama ni mimi ninaekuandama vile, bac nitaacha kukutega!!!!!
 
Ukianza tu kuomba PO ujue ushaliwa. Mdada keshaklula head, tusubiri umaliziaji tu
 
kwa sababu umemzoea kama unavosema basi siku moja toka naye out ya lunch wakati wa kazi..mkifika huko muulize kwa nini amebadilika siku hizi? mwambie wazi kuwa hupendezwi na mavazi yake ya vimini na pia kuacha matiti wazi..
mwambie kuwa hayo yamekufanya umuogope na umkwepe kwa sababu yeye ni mke wa mtu na wewe ni mume wa mtu, na wewe kama mwanaume unaogopa vishawishi vitakavyoharibu urafiki wenu..mwambie wazi hupendezwi na tabia yake na umuombe abadilike arudi kama zamani..
mueleze wazi kuwa hujawahi mcheat mkeo na wala huna mpango huo na pia umshauri na yeye asithubutu kujiingiza kwenye hilo janga..
unapomueleza hayo usionyeshe kama umejua anakutega wewe jifanye kama kuna mtu/boss anamtega basi aache..ofisini tupo kikazi tu..
baada ya hapo muangalie akibadilika endeleeni na urafiki ila usizidishe ukaribu, punguza ukaribu pole pole..kama hajabadilika basi zaidi ya salamu usiwe unamuongelesha mengine..kuwa serious na akikuuliza jambo mjibu kwa mkato...jifanye uko bize na wakati wote usimpe nafasi ya kuwa karibu na wewe..kama ni shida ya kwny computer ita mtu wa IT amsaidie, mwambie ww sio mtaalamu wa IT itakuwa vizuri amuite mtu wa IT..
na pia weka picha ya wife wako mezani kwako na kama ofisi ya wife haiko mbali muombe wife akusindikize lunch japo mara chache
hapo utakuwa umemkata maini na kumpunguzia speed anayokuja nayo...
 
Wana - JF nawasalimu sana!

Mwenzenu nina mtihani! Hapa ofini kwangu ni na bidada mmoja (ni mrembo wa haja tu, anatoka ule mkoa karibu na Dodoma na wadada wa mkoa huo wana ile sifa kama ya ule mkoa wa kanda ile isiotakiwa kutoa Mkulu). Ni mfanyakazi mwenzangu, tuliajiriwa mwezi mmoja, tumeishi kwa miaka mi3 kama kaka na dada, huku tukiheshimiana sana! Kama mnavyojua ofisi za serikali, huwa tunashirikiana sana katika mambo mengi sana ya kiofisi kuanzia kushare stories mpaka kupeana ushauri, asipokuwepo nafanya kazi zake, nisipokuwepo anafanya kazi zangu! Tunashirikiana ktk NIDO, majani ya chai, maji ya kunywa, vitafunio - hivi huwa tunapewa na ofisi, mpaka nauli!

Katika lunch pia hivo hivo, nina hela namuagizia lunch box, na yy akiwa nazo hivo hivo! Yaani tumekuwa dada na kaka wapenzi mpk ofisi zingine wanatuonea wivu! Wakati ofisi zingine wanashindana umbea na majungu, sisi kwetu ni kupendana na kujaliana! wakati mwingine majungu yakiwazidia wenzetu huwa wanakuja ofisini kwetu kupata relief!

Mimi nimeoa na yeye ameolewa! Mwenzangu ndoa yake ina mtihani, hawajabahatika kupata mtoto! Bahati mbaya ni kuwa, bi dada umri umeenda! Mimi amenizidi 2 years! Mimi kwa upande wangu mungu amenijaalia watoto wawili! Mwanzoni kabla sijamsoma, ilikuwa rahisi mimi kumueleza ama kupiga story kuhusu watoto, reference kwa wanangu! Kumbe mwenzangu moyoni alikuwa anaumia sana! ktk story zote tunazopiga, hizi za watoto hazipendi! zinamchoma! Baada ya kujua na mimi nimeacha kumuelezea lolote lile kuhusu watoto wangu! Hata kama naenda hospital kupeleka mtoto, basi yeye nitamuambia naenda k'koo ama posta, ili tu nisimuumize!

Sasa balaa ni hili hapa! Kaja na mpya!
Alianza kwa kuntumia video ya PILAU whatsapp! kwa kuwa ni mtu ambae uhusiano wetu haukuwai kufikia ktk kutumiana vitu km hivo, nikashtuka! nikahisi kakosea wa kumtumia! mimi sikumjibu bali nikai-delete fasta kabla mama nanii hajaiona! nikasubiri sms yake ama call ya apology! kimyaaaa! Baada ya siku kama 3, akanambia samahani ile video haikuwa yako, nilikosea kukutumia, nikamuambia sawa ila kuwa makini!

Hapo kabla alikuwa ni mpenzi wa sketi ndefu na blauz za kuficha matiti, siku hz ni mwendo wa vimini na blauz za manyonyo nje! Mbona nakoma mwenzenu!Siamini kama ananivalia mimi ama mwengine, lkn kazi ninayo! Na pia kesi za kuitwa nikamsaidie kitu ktk computer yake sk hz zimekuwa kibao, hasa za kumwelekeza program mbali mbali, tena wkt mwingine anakuja kwangu kuniinamia nimuelekeze, nakomaje! manyonyo yote, tiiii kwangu!

Likaja la kuonyeshwa chachandu! mimi sijui kama tangu zamani anavaa ama ameanza kuvaa siku hz, na kama anavaa siku hz, ananivalia mimi ama mr wake, mm sijui! ila kila siku naonyeshwa chachandu, lazima nionyeshwe chachandu, kama si asubuhi basi mchana! na anajua style nzuri za kunionyesha chachandu zake! tena anajua kuchagua, zinamkaa vzr kweli kiunoni! (bahati mbaya hajui kama mimi ni ugonjwa wng, hii bidhaa mimi huwa naumwa nikiiona! daah kila m'me na madhaifu yake jamani)

Yote kwa yote mimi si mfuasi wa michepuko! Na bado tunaheshiana sana, japo nimeshaanza juhudi za kupunguza mapenzi ya udada-ukaka ili huko mbele yasije yakawa mazito! Shida yangu wanaJF, naomba mnisaidie njia sahihi ya kumuomba kama ananitega, basi mimi hapana, siko huko! anionee huruma, coz mateso ninayopata, kila siku nakuwa wa kwanza kusepa ofisini na wa mwisho kuingia, na hii inanipunguzia ufanisi kazini! Nambieni nitumie njia gani ili nimrekebishe na turudi ktk undugu wetu kama zamani, nia yangu ujumbe umfikie japo naogopa mashushu ya bimdada! Msaada jamani!
Mtongoze kishambashamba, maana kama hajakudharau, basi walau kwa mara ya kwanza atakujibu "Hapana", then uchukulie ndio jibu la mwisho....! Kuanzia hapo atakuwa mbali nawe, na kamwe hutasumbuliwa tena.
 
Pia amkatishe tamaa like sipendi madudu haya wanawake wanaovaa vitu hivi wananishangaza, naona kama waganga wa kimasai, apende kumuongelea mke wake pia like I real love and respect my wife yaani anavaaga nguo ndefu anapendeza saana, na ukiona matiti yake anza kusifia za wife wako tu like my wife ana saa 6 utasema hajanyonyesha, yani akimkatisha tamaa itapunguza kidogo

Laussane hii pia nimeichikua!
 
mchane laivu wala usimuendekeze oohoooo! ukicheka na nyani utavuna mabua!
 
Kaa nae chini mwambie unavyojisikia kuhusu yeye, sababu mnajuana tangu zamani nina uhakika atakuelewa, mwambie wewe dada yangu ninakuheshimu sana sikuwahi kukuona na mavazi ya namna hii, mbona siku hizi umebadilika sana kitabia

Kuwa muwazi atakuelewa

Good,tena uwe serious kbs atakuelewa.
 
kwa sababu umemzoea kama unavosema basi siku moja toka naye out ya lunch wakati wa kazi..mkifika huko muulize kwa nini amebadilika siku hizi? mwambie wazi kuwa hupendezwi na mavazi yake ya vimini na pia kuacha matiti wazi..
mwambie kuwa hayo yamekufanya umuogope na umkwepe kwa sababu yeye ni mke wa mtu na wewe ni mume wa mtu, na wewe kama mwanaume unaogopa vishawishi vitakavyoharibu urafiki wenu..mwambie wazi hupendezwi na tabia yake na umuombe abadilike arudi kama zamani..
mueleze wazi kuwa hujawahi mcheat mkeo na wala huna mpango huo na pia umshauri na yeye asithubutu kujiingiza kwenye hilo janga..
unapomueleza hayo usionyeshe kama umejua anakutega wewe jifanye kama kuna mtu/boss anamtega basi aache..ofisini tupo kikazi tu..
baada ya hapo muangalie akibadilika endeleeni na urafiki ila usizidishe ukaribu, punguza ukaribu pole pole..kama hajabadilika basi zaidi ya salamu usiwe unamuongelesha mengine..kuwa serious na akikuuliza jambo mjibu kwa mkato...jifanye uko bize na wakati wote usimpe nafasi ya kuwa karibu na wewe..kama ni shida ya kwny computer ita mtu wa IT amsaidie, mwambie ww sio mtaalamu wa IT itakuwa vizuri amuite mtu wa IT..
na pia weka picha ya wife wako mezani kwako na kama ofisi ya wife haiko mbali muombe wife akusindikize lunch japo mara chache
hapo utakuwa umemkata maini na kumpunguzia speed anayokuja nayo...

Mkuu Kamusi nashukuru, ushauri mzuri!
 
.....muendelezee story zako za wanao na mkeo, atakuacha, na ikibidi weka fremu ya picha ya familia yako mezani kwako.

#MosKwito !

Mkuu ushauri wako mzuri, sijui kama picha itasaidia kwa sababu si mara 1 ama 2 nimemleta wife hapa ofisini, wanajuana kwa sura na hata kuwasiliana kwa simu, ni basi tu bidada kaamua kuvaa uso wa mbuzi!
 
Kwani ukimpotezea, ukamdharau na mambo yake utapungukiwa nini
au ndi sitaki nataka?

Ni kweli sintapungukiwa na kitu, ila nataka kuweka mipaka ya heshima baina yetu! namna ambavyo yeye anajiweka itachora taswira ya ss sote tulivo hapa ofisini kwetu!
 
Back
Top Bottom