alinitelekeza mtoto akiwa na miezi mitatu nimejitahidi kulea mtoto kwa kadri niwezavyo mpaka mtoto wangu nw anamwaka na miezi mitano.bila msaada salamu wala chochote kutoka kwa baba yake..
kipindi mtoto ni mchanga nilikuwa namuomba sana tusaidiane kulea mtoto majibu yake yalikuwa utajaza hakuna aliyekulazimisha uzae.na wakati ni kitu tulichopanga na kudhamiria wote wawili...
basi kwa kuwa nilikuwa na kazi na ninayo mpaka sasahivi niliamua kumwachia mungu na kuendelea na maisha yangu na mwanangu bila msaada wa baba yake.nashukuru mungu mwanangu hakuwahi kukosa mahitaji yoyote ya msingi
mpaka sasahivi ni mtoto wa mwaka mmoja na miezi mitano ni mchangamfu,mcheshi,na mwenye furaha saa zote
cha kushangaza leo hii baba wa mtoto asubuhi hii hii amenipigia simu na kuniuliza mtoto anaendeleaje kwa hasira nilimjibu jibu baya sana na kumwambia ulihisi atakufa bila msaada wako au???sikutaka aendelee kunikera nikakata simu hapohapo.akanitumia ujumbe NINAOMBA KUONGEA NA WEWE TAFUTA MUDA TUKAE TUONGEE.kwa kweli sijamjibu nimechukia na naona kama ameniharibia siku na sijui nimjibu jibu gani la kutaka aachane na mimi na mwanangu