nimfanyaje huyu mwanaume

nimfanyaje huyu mwanaume

dadayee

Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
7
Reaction score
0
alinitelekeza mtoto akiwa na miezi mitatu nimejitahidi kulea mtoto kwa kadri niwezavyo mpaka mtoto wangu nw anamwaka na miezi mitano.bila msaada salamu wala chochote kutoka kwa baba yake..

kipindi mtoto ni mchanga nilikuwa namuomba sana tusaidiane kulea mtoto majibu yake yalikuwa utajaza hakuna aliyekulazimisha uzae.na wakati ni kitu tulichopanga na kudhamiria wote wawili...

basi kwa kuwa nilikuwa na kazi na ninayo mpaka sasahivi niliamua kumwachia mungu na kuendelea na maisha yangu na mwanangu bila msaada wa baba yake.nashukuru mungu mwanangu hakuwahi kukosa mahitaji yoyote ya msingi
mpaka sasahivi ni mtoto wa mwaka mmoja na miezi mitano ni mchangamfu,mcheshi,na mwenye furaha saa zote

cha kushangaza leo hii baba wa mtoto asubuhi hii hii amenipigia simu na kuniuliza mtoto anaendeleaje kwa hasira nilimjibu jibu baya sana na kumwambia ulihisi atakufa bila msaada wako au???sikutaka aendelee kunikera nikakata simu hapohapo.akanitumia ujumbe NINAOMBA KUONGEA NA WEWE TAFUTA MUDA TUKAE TUONGEE.kwa kweli sijamjibu nimechukia na naona kama ameniharibia siku na sijui nimjibu jibu gani la kutaka aachane na mimi na mwanangu

 
Duuu....! pole..ujue hata kama alifanya nini uhalisia wa yeye kua baba hautabadilika.....Punguza hasira mama kaongee na mzazi mwenzio,shetan alimpita tu....af inawezekana kakosa kuzalisha huko kakumbuka anakid mahal ndo kama ivo karudi....
 
Kwa nini msioane?
Unaweza kuta ni Mume wa mtu.
Unaweza kukuta ulimlengesha bila yeye kuridhia ndio maana analiruka Kimanga.
Ushauri tuli na mwanmbie una mtu mwingine aliyemtunza mtoto, kama una hakika hamtaoana.
Harakisha kutafuta mchumba na akizidi kukufuata mwambie una mzigo wa mwanamume HATAKUFUATA
 
Ila kuna viumbe wa ajabu sana huku duniani
"
Kuna jamaa yangu aliwahi kuniambia kwa mzaha kuwa kuna binadamu wengine waliumbwa na malaika
"
Naanza kuhisi mzaha wake kama ukweli,maana kuna mambo watu wanafanya utadhani ubongo wameupeleka likizo.
"
Huyo jamaa yako inaonekana aliumbwa na malaika . . .Lol!
 
Ni heri umsamehee sasa hivi ili akusaidie kulea huyo mtoto, kuliko kuhangaika kulea mwenyewe halafu mtoto akiwa mkubwa anamtafuta baba yake tena na kumsaidia juu wakati baba yake hakumlea.

Usije ukafikiri mtoto kufika mwaka na miezi kadhaa ndio kakua na umemaliza kazi kisa anatembea na kuongea! My dear u got long way to go kabla hujasema umemaliza kulea.

Pia unatakiwa kujua MARA NYINGI mtoto anayelelewa na mzazi mmoja na huyo mzazi HAPATANI na mzazi mwezie (sio lazima kimapenzi) basi mtoto huyo huweza kuwa mtukukutu na ngumu kum-control tabia zake.
So my dear, think twice before hujaamua!!!
 
Jaribu kusikiliza moyo wako, usitake kujilazimisha kuishi na mtu ambaye atajakutesa moyo wako baadae, watu wasikudanganye kuwa lazima mtoto apate malezi kutoka pande zote mbili, umesema una kazi, lea mtoto wako na mungu atakusaidia utapata mwanaume mwingine mwenye kujali na atakae mjali na mtoto wako pia. Kuzalisha mwanamke sio kuitwa baba, to be father is more than that, mwanaume ambae hataki majukumu yake hatakama anawatoto wa kuzaa kumi, hafai kuitwa baba.
 
Ni heri umsamehee sasa hivi ili akusaidie kulea huyo mtoto, kuliko kuhangaika kulea mwenyewe halafu mtoto akiwa mkubwa anamtafuta baba yake tena na kumsaidia juu wakati baba yake hakumlea.

Usije ukafikiri mtoto kufika mwaka na miezi kadhaa ndio kakua na umemaliza kazi kisa anatembea na kuongea! My dear u got long way to go kabla hujasema umemaliza kulea.

Pia unatakiwa kujua MARA NYINGI mtoto anayelelewa na mzazi mmoja na huyo mzazi HAPATANI na mzazi mwezie (sio lazima kimapenzi) basi mtoto huyo huweza kuwa mtukukutu na ngumu kum-control tabia zake.
So my dear, think twice before hujaamua!!!

Nakupa tano!!! JF
 
Achana naye badilisha namba kabisa!! Haiwezekani mwaka mzima na miezi mi3 hajawai uliza mtoto anaendeleaje,huyo ni zaidi ya hitler kuna siku atakuja kukuchinja wewe na mtoto! Mkimbie kabisa yani mwambie kabisa aachane na wewe tena badirisha namba fasta,kuna kitu huyo anatafuta si bure!
 
Use the bastard. Lakini control hisia zako. Chop the money, akisepa unaendelea.
Time for payback with love.
:target::bowl:
 
Kwanza tafuta sababu ya kumkumbuka huyo mtoto.....
 
Ukweli utabaki pale pale kwamba huyo ni baba wa mtoto.. Cha msingi msikilize anachotaka kuongea kama hakina maana achana nae na kama atakubali ku take responsibilities let him do that! Sababu mwanao hataliona hilo baadae.. watu wanatelekezwa na mzazi wao na wakikua badae wanawatafuta..
 
Nenda umsikilize ana sera gani usikatae wito ! Pili anaweza akawa amejitafakari na akaamua kubadilika, kama kaamua kubadilika msamehe na mlee mtoto wenu, hata ukikataa mtoto akikuwa atamtafuta tu baba yake.
 
nazani bado unasafari ndefu ya malezi ya mwanao,ni bora ukaitikia mwito,msikilize ana sera zipi,ujue sababu za kurudi kwako then ufikie maamuzi yenye tija kwako na mwanao kwa pamoja.
 
Huyo mtoto akikuwa utamla? na mtu umezaa naye halafu hutaki kuwasiliana nae huyo mtoto akifa leo utamla? au utamzuia asihusike na msiba au asilie? acha ujinga bwana mmekosana nyinyi lakini kumuunganisha mtoto na baba yake ni moja wapo ya malezi bora unayotakiwa kumpa ili usimharibie flow ya fikra zake. Sio lazima kila unalofanya liwe na faida kwako ht likiwa na faida kwa mtoto au baba yake ni poa tu usiwe m-binafsi kiasi hicho utakufa siku si zako.
 
Use the bastard. Lakini control hisia zako. Chop the money, akisepa unaendelea.
Time for payback with love.
:target::bowl:
she shouldn't stoop down to his level. usilipe ubaya kwa ubaya sis
 
she shouldn't stoop down to his level. usilipe ubaya kwa ubaya sis
Hahaha, my revenge mode is so onn, kid brother. Yaani give himthetaste of hisown medicine kabisaa. Meet him, take arrears on the child support and probably sue the bastard for child support. Plus ratiba ngumu ya kumuona mtoto. Kuna wapuuzi hawanyooki.
 
Nenda umsikilize ana sera gani usikatae wito ! Pili anaweza akawa amejitafakari na akaamua kubadilika, kama kaamua kubadilika msamehe na mlee mtoto wenu, hata ukikataa mtoto akikuwa atamtafuta tu baba yake.

Hata akimtafuta baba yake kuna shida gani? Cha msingi kwa sasa ni kukaa mbali naye! Haiwezekani mtu ametoka kujifungua then amtelekeze kwa mwaka mzima na nusu leo ndio aanze kukumbuka,huyo jamaa ni mchumia tumbo alishafulia au alishachunwa huko alipokua sasa anataka kuja kula kwa zilipendwa wake!!
 
Pole sana kwa kulea mtoto peke yako hasa katika kipindi ambacho ulihitaji ukaribu wa mzazi mwenzio, inauma sana, pole sana.

Kusema ukweli baadhi ya wanaume (na niseme walio wengi) huogopa kitu mimba hasa kinapotokea nje ya ndoa. Sielewi ni kwa nini lakini hupenda sana kuitwa baba wanaume wa namna hii.. Niliwahi kusimuliwa kisa cha namna hii na mdada ninayefahamiana naye kikazi na yeye hili limemtokea mara mbili kutoka kwa mwanaume huyo huyo mmoja. Yaani alimmimba na kusepa, alipojifungua baada ya miezi kadhaa kupita akamtuma rafiki yake akachungulie kama mtoto anafanana naye, akakuta ni hivyo, alikujaje haraka haraka na pickup la mahitaji ya mtoto na samahani zisizo na idadi... Mtoto alipofikisha umri wa miaka miwili na zaidi mdada wa watu mimba nyingine ya huyu huyu bwana... Bwana kujua hilo akakata mguu bibi kahangaika na mimba hadi dakika za mwisho karibia na kujifungua, ikawa bahati mbaya mdada kalazwa Tumbi zaidi ya wiki maana mimba ilikuwa imeharibika kipindi, kujiuguza mwenyewe, kwa miezi kadhaa hadi kutengamaa kurejea kazini na kunihadithia kisa chote bwana hana hata taarifa ya kinachoendelea!!

Ila huyu bwana ni mume wa mtu. Ushauri jifikirie mara kadhaa ukiweza msikilize kwa minaajili ya kupokea msaada wa malezi ya mtoto lakini angali usiingie katika mtego wa kutoa penzi na kubeba ya pili ukatekelezwa tena...., kubali matunzo ya mtoto kwa kuwa kama alivyosema mmojawapo humu kwamba mtoto akikua atamtafuta babaye na hasa kama mtoto ni wa kike ndo kabisa akimjua babaye huna lako wakati ulihangaika peke yako kumlea wakati nafasi ya mzazi mwenzio alijileta kutaka kuchangia malezi... Utaumia zaidi ya unavyohisi...
 
Back
Top Bottom