Nimfanyaje huyu dada? Yamenikuta leo asbh

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Ni wiki chache zimepita tangu nihamie kwenye kibanda chungu nilichojenga nje ya mji. Kwa sababu ya umbali wa ninakokaa na foleni za magari, inanilazimu kuondoka nyumbani kumi na mbili kasoro kuwahi traffic jam.

Siku ya kwanza nikiwa kwenye gari yangu nilikutana na huyu binti aliyesababisha leo niombe ushauri. Alikuwa anajitembelea pembeni ya barabara akielekea kazini. Kwa kuwa sikumfahamu, nilimpita.

Kesho yake muda kama huo nilikutana naye tena, aliniangalia sana, lakini nikampita. Siku ya tatu nikamkuta tena kwa huruma nikasimama, na kumkaribisha lifti mpaka mjini ambako kila mtu alielekea kzn kwake. Basi tangu siku hiyo ikawa ndo kupeana lifti na mazungumzo ya ndani yalikuwa ni salamu tu.

Juzi amehamia jirani mwingine mdada ambaye amejenga nyumba karibu na kwangu kabisa. Baada ya kutambulishana na jirani huyu, akaomba nayeye awe anapata lifti ya kwenda kazn. Nilimkubalia.

Cha kushangaza, leo nilimpa lifti jirani yangu huyu mpya ambaye alikaa siti ya mbele ya gari. Hatua chache mbele kidogo nikakutata na huyu mdada wa siku zote, kama kawaida nikasimama.

Akaja, akafungua mlango wa mbele, baada ya kugundua kuwa kuna dada mwingine amekaa siti ya mbele, akafyonza na kufunga mlango kisha akazira na kukataa kupanda gari.

Nauliza waungwana kosa langi ni lipi? Na nimtendeje huyu dada? Nahisi amenidhalilisha kwa jirani yangu!

Wasalaam,
HP
 
Ni wiki chache zimepita tangu nihamie kwenye kibanda chungu nilichojenga nje ya mji. Kwa sababu ya umbali wa ninakokaa na foleni za magari, inanilazimu kuondoka nyumbani kumi na mbili kasoro kuwahi traffic jam. Siku ya kwanza nikiwa kwenye gari yangu nilikutana na huyu binti aliyesababisha leo niombe ushauri. Alikuwa anajitembelea pembeni ya barabara akielekea kazini. Kwa kuwa sikumfahamu, nilimpita.Kesho yake muda kama huo nilikutana naye tena, aliniangalia sana, lakini nikampita. Siku ya tatu nikamkuta tena kwa huruma nikasimama, na kumkaribisha lifti mpaka mjini ambako kila mtu alielekea kzn kwake. Basi tangu siku hiyo ikawa ndo kupeana lifti na mazungumzo ya ndani yalikuwa ni salamu tu.Juzi amehamia jirani mwingine mdada ambaye amejenga nyumba karibu na kwangu kabisa. Baada ya kutambulishana na jirani huyu, akaomba nayeye awe anapata lifti ya kwenda kazn. Nilimkubalia.Cha kushangaza, leo nilimpa lifti jirani yangu huyu mpya ambaye alikaa siti ya mbele ya gari. Hatua chache mbele kidogo nikakutata na huyu mdada wa siku zote, kama kawaida nikasimama. Akaja, akafungua mlango wa mbele, baada ya kugundua kuwa kuna dada mwingine amekaa siti ya mbele, akafyonza na kufunga mlango kisha akazira na kukataa kupanda gari.Nauliza waungwana kosa langi ni lipi? Na nimtendeje huyu dada? Nahisi maenidhalilisha kwa jirani yangu!Wasalaam,HP
huyo dada ni jini kisigino muepuke sana!
 
Hii ni kali!
Nimesoma hadithi nyingi, huwa zinaelekeana lakini ya kwako hii ni ya aina yake!
Wanawake wana wivu sana na ni roho mbaya kichizi!

Lakini wewe mwenyewe huenda hujatulia, unaweza kukuta unajieleza mambo mazuri tu, usikute ushalikoroga sana na huyo mdada wa watu siku za nyuma!...kwanini asonye wakati hajui kuwa huyo ni dada yako au shangazi yako?
Anaijua tabia yako huyo mkuu!..badilika!
 
hebu tuambie mlikuwa mnaongeaga nini humo garini kwako?
halafu mmepeana hiyo lifti kw amuda gani?
 
Jamani, naapa kabisa sijawahi kumwambia neno lolote huyu dada isipokuwa salamu na kumjulia hali yeye na familia yake. Ni huruma tu ya kumsaidia lifti nahisi ndiyo imeniponza.
 
apo kuna kitu.ulimwambia haujaoa?nway saa ingine hata kama umeoa lazm kutakua na vijiinterest fulan umevionyesha kwake akajipa izo hope...........
 
Jamani, naapa kabisa sijawahi kumwambia neno lolote huyu dada isipokuwa salamu na kumjulia hali yeye na familia yake. Ni huruma tu ya kumsaidia lifti nahisi ndiyo imeniponza.
si ulisema kulikuwa kunamazungumzo mengine ya ndani..!??
Siku ya tatu nikamkuta tena kwa huruma nikasimama, na kumkaribisha lifti mpaka mjini ambako kila mtu alielekea kzn kwake. Basi tangu siku hiyo ikawa ndo kupeana lifti na mazungumzo ya ndani yalikuwa ni salamu tu.
 
Back
Top Bottom