Heisenberg
JF-Expert Member
- Apr 26, 2017
- 1,688
- 2,981
- Thread starter
- #221
Nimeongea na watu wanasema nisiende
Kama una nia nenda nyumbani kwao, watakuelewa
Kama una nia nenda nyumbani kwao, watakuelewa
Wewe huna kosa mwanamke angekuwa anampenda jamaake asingekukubali kirahis hivyo, sasa huko ukienda kukutana na kosi lakukidhuru utafanyaje ? unaenda mwenyewe ? Alafu kitu kingine mnaenda kudiscuss nini ? mnaenda kuongelea namna wewe ulivyokuwa unamwibia jamaa mchumba ake mpaka akakukuta kwake ? Haya tuseme umefika wakakuomba umwachie jamaa mwanamke wake utafanyaje ? wewe vaa viatu vya jamaa na jamaa awe wewe, UNGEENDA ?
uItakugharimu wewe na uzao wako, asilimia 99 ya matatizo yanayowakumba wanadamu na uzao wake ni ya kujitakia.
Duh asee unasema aende tu ? labda Kama hao wazazi ni walokole sio ulokole was gwajimaboy...najenga picha Kama Mimi ningefumania ?, kama Mimi ningekuwa mzazi wa binti ? . kikubwa tulia sikiliza upepo lakini usiende huko ni aibu ya maumivu yanayoumiza kiundani undani .We nenda, kaombe msamaha, wala usimlaumu huyo mwanamke, beba dhambi, okoa ndoa ya watu,ni aibu sana kwa wazazi kudaiwa mahari kwa sababu ya aibu ya binti yao.....
Malalamiko ya hao wazazi ndugu yangu yatakupa shida sana sana, hakikisha wanarudiana aisee.... sioni ubaya ya huyo mwanamke, wengi wanakosea na anaweza kuwa mtu mzuri tu sana.....
Duh asee unasema aende tu ? labda Kama hao wazazi ni walokole sio ulokole was gwajimaboy...najenga picha Kama Mimi ningefumania ?, kama Mimi ningekuwa mzazi wa binti ? . kikubwa tulia sikiliza upepo lakini usiende huko ni aibu ya maumivu yanayoumiza kiundani undani .
Binti ndiye kajiaribia wala sio wewe kwani angekukatalia seriously kwake ungeenda kufanya nini?
Wanawake wa sasa hawana misimamo
Sawa mkuu nitakuja na taarifa. Ngoja nipate maoni ya wadau
Mkuu nipo tayari kwa kila kitu kuhakikisha familia yao inapata amani na binti anapata heshima niliyoipoteza
Ushauri mzuri. kwa kuongezea tu jamaa hapaswi kwenda peke yake. kwa tahadhari asiende peke yake.Inavyoonekana huyo mwanamke alipewa onyo juu yako na alipokushirikisha haukutilia maanani, maana inaonekana anakujuwa vizuri na ukute ulipofika majirani walimpa taarifa hivyo alikuja akiwa tayari ana maamuzi, yaani ndugu zake kumtuliza inakuwa ngumu.
Kibaya utakuta umeoa na haukuwa na nia ya kumuoa, kama unamuona ni mwanamke anayekufaa haupaswi urudi nyuma kama ambavyo ulifanya alipokupa onyo juu ya kuwa na mahusiano lakini haukupunguza mapenzi kwake.
Mapenzi yale yale uliyokuwa nayo ndiyo unapaswa uyaoneshe kwake...
Kwa ushauri wangu kubali kwenda ila usiende leo subiri kidogo papoe, naamini kwasasa labda ndugu wakawa na jazba zaidi.
Utakuta jamaa alikuwa anamtafutia sababu namna ya kumuacha sababu ameipata tena amekukabidhi wewe, lawama hapati tena na mahari akipewa anaanzisha biashara.