Nimevunja uchumba wa watu

Nimevunja uchumba wa watu

Ila mtu kama hakupendi kwa nini akuite kwake? Mwenye kosa ni huyo mwanaume, ukute haeleweki na wewe unaelewaka sema ni Mume wa Mtu, kama dini inaruhusu muoe na yeye, ila huyo mwanaume aache kususa susa kama binti
Kweli watu tuko tofauti yaani niwe na mchumba afu nigundue anatoka na mtu naanzaje kuendelea nae kwa mfano,watu wa dizaini hii ndio huwa mnajinyonga wanawake ni wengi kwa nn kulazimisha kumuoa mtu hakutaki? Mimi hata wife tunamalizana kwa amani unless sijajiridhisha aisee
 
Habari za eid

Kuna binti niponae kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa toka mwaka huu uanze. Nimekuwa nikimpenda sana kiasi cha kujitoa sana kifedha na ki hali kwa muda wote huu.

Lakini binti amekuwa akinisisitiza kuwa yeye ni mchumba wa jamaa fulani na wanasubiri ndoa tuu. Hiyo hali haikunirudisha nyuma kwa mapenzi niliyokuwa nayo kwake.

Juzi jioni Baada ya kutoka kutafuta Ugali wa watoto nikampigia bint kuwa niende kwake au yeye aje kwangu. Binti akasema niende. Basi bila kusita nilifunga safari nikaenda. Tukawa kwake akapika tukala

Hamad mida ya saa4 mlango ukagongwa. Sikuwa na wasiwasi kumbe ni mchumba wake. jamaa akaingia ndani akanikuta nimekaa kwenye sofa, jamaa akaniangalia akaniuliza hivi bado unaendelea na mchumba wangu?? Mm nikawa kimya jamaa akaingia chumbani kwa mwanamke akabeba vitu vyake na kuondoka. Mm nikabaki na yule mwanamke.


Amelia usiku kucha na kunitupia mm izo lawama. Asubuhi jana jamaa ameambatana na mshenga wake wameenda nyumbani kwa akina Binti kudai mahari. Ndugu wa mwanamke wameomba jamaa na mshenga waende Jumamosi ili kikao cha familia kilichopokea mahari kikutane. Baba na mama ya binti wameshindwa kumtuliza jamaa ili wayamalize. Jana jioni nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mzazi wa binti, niliongea nae aiwa analia sana. Nimeomba leo niende nyumbani kwa akina binti nikawasikilize wazazi wake.

Nimemuuliza binti kuwa niende kwao au nisiende binti hataki kusema. Nikampigia dada ake binti kuwa vipi niende kwao?? Dada yake akasema niende.

Hapa nilipo najiaandaa kwenda. Ni mkoa jirani. Ni mwendo wa masaa 4 tu ntakuwa nimefika.

Kesho usilete uzi ya kwamba umemuoa dada ila analiwa na mchumba wake wa zamani what goes around comes around
 
heeee we jambaa mbona lipumbavu sana!? una akili wewe au fuse moja imeblow up
 
Kweli watu tuko tofauti yaani niwe na mchumba afu nigundue anatoka na mtu naanzaje kuendelea nae kwa mfano,watu wa dizaini hii ndio huwa mnajinyonga wanawake ni wengi kwa nn kulazimisha kumuoa mtu hakutaki? Mimi hata wife tunamalizana kwa amani unless sijajiridhisha aisee
Mkuu umeiamini hiyo stori
 
Anachotakiwa kufanya ni kuongea na mwanaume mwenzie, amuunganishe na binti kisha achape lapa.
Akifanya hivyo, familia zote mbili zitamheshimu mno.
Akatafute wa kwake, wanawake wengi hivi halafu anakuja kushiriki dhambi ya kutenganisha wachumba kwa makusudi
Hivi buda ukifahamu nakula mwanamke ambaye ni dem wako na una malengo ya kumuowa na nikakufuata tujadili utaendelea kuwa na hilo limwanamke?

Au unaweza kunisikiliza? Wallah utakuwa Boya, fala dunia nzima na utaendelea kuchapiwa mpaka mwisho wako kama utakubaliana na huo upuuzi.

Sijui kwanini kadri siku zinavyozidi kwenda nakuwa mkatiri
 
Hivi buda ukifahamu nakula mwanamke ambaye ni dem wako na una malengo ya kumuowa na nikakufuata tujadili utaendelea kuwa na hilo limwanamke?

Au unaweza kunisikiliza? Wallah utakuwa Boya, fala dunia nzima na utaendelea kuchapiwa mpaka mwisho wako kama utakubaliana na huo upuuzi.

Sijui kwanini kadri siku zinavyozidi kwenda nakuwa mkatiri
Buda huyu jamaa kafosi kingi, huyo manzi hakuwa na time naye. Ndiyo maana alimchana live, ajue kabisa hana malengo naye.

Kufikia huko ni manzi moyo wake kuingia huruma na kuchoka kusumbuliwa, hata huyo mchumba wake inaonekana wazi alishaambiwa na demu mwenyewe juu ya kero za jamaa
 
Ni mwanaume usiye jitambua utamgamganiaje mwanamke ambaye unajua amechumbiwa, na huku wanawake wamejaa huku mtaani, alafu kwenda nyumban Kwa mwanamke ambaye unajua ana MTU wake maksudi ni ujinga wa hali ya juu utakuja kubakwa
 
Kuna wakat huwa nawashangaa sana wanawake mpaka napata hasira.Nashindwa tu kutukana maana na mm nina watoto wa kike ila huyo manzi alichofanya ni kuzingua.Hata hajui anampenda nan kati yenu!!
 
Hujavunja uchumba wa mtu,binti kavunja uchumba wake kwa kunogewa na penzi lako mbona wanaume tunabebeshwa lawama zisizotuhusu angekukataa kwa kuwa alikuwa na mchumba.
 
Wewe na yule jamaa huyo mwanamke hawafai ukiamua umuoe ipo siku utamkuta na yule mchumba wake wa zamani ni swala la muda tu,au jitoe mhanga tu maisha hayatabiliki
 
Back
Top Bottom