Nimeumia kwa kauli hii

Lupamba's grandson

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
1,232
1,192
Nikiwa ni mmoja wawatu walio bomolewa nyumba zao maeneo ya kimara ,pamoja na biashara kuharibika, jana nilipoona Muheshimiwa Mtukufu Raisi wangu kutamka maneno haya nimesikia moyo umekufa ganzi nikawaza kwanini sisi Na kwanini wao?? Of coz Nimeumia nikiwaza nilivyo vuja jasho kubeba zege nakufanikiwa kujenga kakibanda kangu na siku kana bomolewa nilitoa machozi na niliumia sana. Hii inaumiza
Screenshot_20180311-083019~2.jpg
 
Nikiwa ni mmoja wawatu walio bomolewa nyumba zao maeneo ya kimara ,pamoja na biashara kuharibika, jana nilipoona Muheshimiwa Mtukufu Raisi wangu kutamka maneno haya nimesikia moyo umekufa ganzi nikawaza kwanini sisi Na kwanini wao?? Of coz Nimeumia nikiwaza nilivyo vuja jasho kubeba zege nakufanikiwa kujenga kakibanda kangu na siku kana bomolewa nilitoa machozi na niliumia sana. Hii inaumiza View attachment 711081
Nyie mlimpigia kura mgombea wa Ukawa usilalamike kubali matokeo yeye ni rais wa wanyonge wote bila ubaguzi.
 
Ila huko dar si mlikua mnalalamika miundombinu mibovu mara barabara ndogo zinahitaji upanuzi bla bla tele, watu wa dar sion haja ya kuumia wakati jiji linajengwa na kuchongwa vizuri
 
Mipango ipo mbion kuanza jengwa. Huko anakosema wasibomoe ni kutulizwa kwa muda tu ila patabomolewa vizuri tu.
Hizo nyumba tangu zimebomolewa barabara ishajengwa? Au mkuu alikua anaonesha upendo wake kwa masikini?
 
Mipango ipo mbion kuanza jengwa. Huko anakosema wasibomoe ni kutulizwa kwa muda tu ila patabomolewa vizuri tu.
Kwahiyo unataka kusema mkuu ni muongo,anawadanganya hadharani hao masikini anaowapenda.

Kulikuwa na ulazima gani wa kubomoa kipindi ambacho mipango ya ujenzi kuanza haijawa tayari? Au huo ndio upendo anaousema kwa masikini?
 
Kila awamu na ahadi yake wanaolalamika saiv enzi za JK waliahidiwa hawatabomolewa sasa na hao wanaahidiwa hazitabomolewa watabomolewa awamu ijayo. Kila enzi na zama zake

Sijawah ona sehemu pana bomolewa paap na kujengwa hapo hapo haijawah tokea inachukua muda kidogo
Kwahiyo unataka kusema mkuu ni muongo,anawadanganya hadharani hao masikini anaowapenda.

Kulikuwa na ulazima gani wa kubomoa kipindi ambacho mipango ya ujenzi kuanza haijawa tayari? Au huo ndio upendo anaousema kwa masikini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom