Nimeumbuka

Nimeumbuka

Habari Wakuu.

Tarehe 21 mwezi wa kumi na Moja ni siku mbaya Sana kwangu iliyonitia huzuni na sonono japokuwa ilipaswa kuwa siku ya furaha na nderemo kwani ndio ilikuwa siku ya Mahafali yangu ya Shahada ya Awali kabisa katika Chuo kikuu Cha Dar es Salaam.

Siku ilikucha vizuri. Ndege wa angani walionekana wakiambaa ambaa angani huku sauti zao za Shangwe zikisikika. Niliamka kwa ajili ya kujiandaa na Mahafali nikiwa na kimue mue Kama mtu aliyepata donge nono la TATU MZUKA.

Niliichukua simu na kukuta jumbe nyingi zikinitakia kila la heri na kunipongeza kwa hatua niliyofikia. Uso wangu ulizingirwa na tabasamu jepesi huku macho yangu yakisawijika baada ya kuona Ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu ambaye yupo Mwanza. Nilifurahi Sana kwa namna ya uandishi wake.

Saa yangu iliyoukutani ilikuwa inasema ni Saa mbili kasoro dakika kumi. Sikuwa na muda mwingi hivyo nilijiandaa kwaajli ya kwenda Mlimani City kwaajili ya tukio muhimu Sana kwa Wasomi. Moyoni upepo wa furaha ulizunguka. Kichwa kilijawa na mawazo yenye amsha amsha ya ujana.

Mara Geti lilifunguliwa likifuatiwa na sauti za wadada wakicheka. Walikuwa ni Majirani zangu ambao ni Mamiss wa miaka iliyopita. Mmoja alikuwa Miss Kinondoni mwaka upo kapuni, Mwingine Miss mtwara, na watatu alikuwa ni Mtangazaji fulani wa Channel fulani kubwa hapa nchini.

Waliingia na kuanza kucheza huku wakinikumbatia Kama pongezi. Nilijisikia faraja Sana. Nilihisi jambo lenye ufahari Sana. Moyoni nilimshukuru Sana Mungu.

Tulichukua Uber na Moja kwa Moja tulichukua uelekeo wa Mlimani City. Ndani ya Uber zilikuwa Shangwe, watoto walipendeza Sana. Kutokana na kuzoeana sikuona umuhimu wa kushangaa mapaja yao makubwa yaliyokuwa yapo wazo kwa kiasi Cha kuvutia macho.

Punde tulijikuta tupo Mlimani City. Watu walikuwa wengi mno. Wahitimu pamoja na wageni waliokuja kuwapongeza ndugu zao walijaza eneo zima.

Nilishuka. Tukapiga vipicha vya kutosha Kama utangulizi na wale wadada. Ilibamba Sana. Nilifurahi kuonana na wahitimu wenzangu tulioachana kwa muda wa miezi mitano. Picha zilihusika.

Muda wa kuingia ukumbini Ulifika. Niliwaonyesha wageni wangu sehemu ya kukaa na ambapo nitawakuta muda nikitoka ukumbini.

Nikiwa ndani nilifurahi kuona jinsi Wahitimu tulivyokuwa wengi. Moyoni niliwaza jinsi nchi yetu Sasa inavyoendelea kwa kuzalisha Wasomi wengi kwa ngazi ya shahada. Nilijisemea; Sasa taifa litasonga.

Mbele yetu Wahitimu walikaa Watu wazito. Moja wa watu wale alionekana mtu mmoja mweupe akitabasamu kila Mara huku kofia yake ikizidi kumfanya apendeze. Alikuwa ni Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete. Nilifurahi Sana kumwona.

Tulitunukiwa Shahada ya Awali. Hakika ilikuwa siku ya namna yake.

Muda wa kutoka ukumbini uliwadia. Kila mmoja alienda walipo wageni wake. Nami nilienda kwa wageni wangu yaani wale wadada watu waliwashangaza watu wengi kwa mavazi yao na uzuri wao.

Tukiwa tunaondoka Mara sauti ilisikika kutoka nyuma yetu ikiita; Michael! Micky Michael!
Iliita Mara tatu. Niligeuka Mara. Sikuamini yule niliyemuona. Nilibaki nimesimama wima Kama Dr. Shika. Moyo ulisimama kwa kitambo huku mtirirriko wa mawazo ukiwa umevurugika. Sikujua Kama nimesimama au nimelala. Kwa wale wasioelewa hilo ndilo linaitwa Bumbuwazi. Bumbuwazi lililoliniacha Mdogo wazi.

"Michael hata kunialika!"
Binti huyo aliongea akiwa amenikaribia Kama mita Moja.
Alikuwa ni Rehema. Mwanamke niliyekuwa naye kwenye mahusiano pindi nipo Moshi.

Mapenzi yetu yaliingiliwa na jinamizi la mazingira. Hii ni baada ya yeye kupata Scholarship ya kwenda kusoma Australia. Na ndipo penzi letu lilipokauka kau Kama mate kwa mwenye kiu.

Alipoenda Australia nilijikuta nimepoteza mawasiliaono naye. Hata hivyo na yeye hakunitafuta hivyo kila mtu alianza ukurasa Mwingine. Leo uso kwa macho na mrembo Rehema.

Haikuwa shida. Nilimtambulisha kwa wageni wangu. Na kumuomba ajumuike nasi. Bila hiyana Rehema alijumuika.

Nilimuuliza Mlimani City alikuja kufanya nini. Akasema alikuja kuweka hela. Basi hao tukatoka getini. Tukiwa Getini tunapiga simu kwa Uber. Mara paap! Uso wangu ulishikwa na usumaku na kuvutwa. Alikuwa ni Asinath aliyekuwa mbele yetu Kama mita tano hivi. Alikuwa Kama hajaniona hivyo ilibidi nifanye jitihada za kujificha kinamna nyuma ya mgongo wa miss Kinondoni ambaye ni mrefu kidogo kwangu.

Kwa bahati mbaya aliniona. Ilikuwa tabu Sana. Alikuja kwa madoido katikati ya kukimbia na kutembea na kunikumbatia. Alinipiga mabusu mazito watu wakitizama video bila kupakua(upload).

"Yaani Zena kaniambia Jana kuwa Leo ndio Mahafali yako. Nikasema hata Kama hujanambia nitakuja. Labda nisikuone na kwa bahati nimekuona"
Asinath aliongea huku wale aliokuwa nao wakinitizama kwa kunikagua mimi na wageni wangu.

Hapo ndipo kimbembe kilipoanza.
Rehema alibwatuka;
"Michy babby tuondoke tunachelewa"
Tafrani yake haikuwa kitoto. Asinath alikuja juu na kuanza kumtukana Rehema.
"We Malaya kaa kimya, huna hadhi ya kutembea na Michy. Tafuta wa tandale ndio Saizi yako"
Vurugu ilikuwa si mchezo. Walianza kurushiana makofi mazito huku wale wadada wakigeuka kuwa waamuzi.

Kwa maumbile na muonekano Asinath ni mweupe wenye mkolezo wa kichotara(kipijini). Na shepu matata. Hivyo alikuwa kumfotabo Sana.

Niliondoka kinyemela na kuwakimbia nikiacha ugomvi ukiendelea. Nilichukua bajaji nikapotea kwa muelekeo wa Sinza.

Hivyo ndivyo nilivyoumbuka na siku yangu ya Mahafali ilivyogeuka kutoka kwenye kicheko na kuwa kioja.


Michaelray.
Huu mwezi ukifika inatakiwa uhuruke
 
Ni simulizi nzuri bila kujali uhalisia.
FUNZO
-Kuwa mkweli katika mambo yako mengi katika jamii
-Usipende mazoea kupitiliza na mtu hasa asiye mpenzi wako
-Usiwe mwepesi kumkaribisha katika mipaka yako mtu asiye na staha
-Ukiwa chanzo cha timbwili, linapoanza usikimbie. Jinsi unavyoendelea kushuhudia kinachoendelea ni fursa kwako kurekebisha makosa hapo mbeleni
-Uwapo na tukio lihusulo umati mkubwa, penda kualika watu wa jinsia mbalimbali wakusindikize eneo husika. Hii itakusaidia, si mara zote ila mara nyingi,kufunika uovu wako. Kwa sababu, kama kuna mtu anataka kukileyea songombingo ataogopa aibu na ushahidi WA macho itakaomgharimu.
Wewe ni Moja ya Great thinker Mkuu.

Nilitegemea watu Kama ninyi mnaojua kuchambua na kuhakiki mambo Kama haya.

Ahsante kwa ushauri
 
Hakuna ujinga mkubwa kama kupigana sababu ya mwanaume, ona sasa walipigana mwisho wa siku mwanaume mwenyewe keshakimbia!! Inauma lakini kupigana ni kujichoresha tuu
Kwa kweli ni aibu. Alafu ni watu ambao hawajaalikwa.
 
Hiyo inadhihirisha ni namna gani ulivyo Malaya, aibu hiyo umejitakia! Angekuja na huyo uliyemsema kuwa ni mpenzi wako wa Mwanza, cjui hali ingekuwaje! Jiulize then take action! Nyambafuu!
Ahsante Sana.

Aibu iliisha saa 12 nilifika kwenye sherehe. Huko ndipo Nilisahau habari za Mlimani City
 
Tushajua unaishi na ma miss na watu wenye maisha poa na warembo
Ushajua na nani?

Usipende kutoa maoni yako kwa kujumuisha na wengine. Ni Moja ya dalili ya mtu asiyejiamini.

Hata hivyo nayo ni maoni yako. Hivyo ahsante kwa kuhusika
 
Hakuna ujinga mkubwa kama kupigana sababu ya mwanaume, ona sasa walipigana mwisho wa siku mwanaume mwenyewe keshakimbia!! Inauma lakini kupigana ni kujichoresha tuu
Mwengine walipotezana muda tu alipoenda kusoma Australia. Mwengine haieleweki alikua wapi. Walipigana kwa lipi hasa
 
Back
Top Bottom