Nimetumiwa ujumbe wa kitapeli

Nimetumiwa ujumbe wa kitapeli

Nimetumiwa ujumbe huu sasahivi:
HABARI ZA SIKU NDUGU, ILE NAFASI ULIYONIOMBA KWA AJILI YA KIJANA KUJIUNGA NA JESHI IMEPATIKANA, MWANDAE AFIKE HAPA KAMBINI KABLA YA TAREHE 14.
Number iliyotuma: 0713375482 imesajiliwa tigo Pesa kwa Jina la Jacob Bwire.
Note:Wengi wataumia kama vyombo vinavyohusika havitaingilia kati
Nimetumiwa ujumbe huu sasahivi:
HABARI ZA SIKU NDUGU, ILE NAFASI ULIYONIOMBA KWA AJILI YA KIJANA KUJIUNGA NA JESHI IMEPATIKANA, MWANDAE AFIKE HAPA KAMBINI KABLA YA TAREHE 14.
Number iliyotuma: 0713375482 imesajiliwa tigo Pesa kwa Jina la Jacob Bwire.
Note:Wengi wataumia kama vyombo vinavyohusika havitaingilia kati

Huo ni mtego. Anakuvuta ili na wewe umuombe akusaidie ili mwanao apate kazi huko. Ukishaingia katika mtego huu utakombwa pesa na kazi asipate. Chukua Tahadhari kabla ya Hatari.
 
Mi mwenyewe nishatumiwa mara mbili huo ujumbe na kwa namba hiyo hiyo! Mara ya pili nilimwambia anifanyie mpango ila hakujibu

Mambo kama haya yasiposhughulikiwa yanaitia aibu serikali.Kila kitu kimwekwa wazi,jina la mtumaji,mtandao uliohusika,kosa lenyewe.Hatua haichukuliwi.JPM akichukua hatua tunasema anakurupuka.

Kwa nini mamlaka husika haichukui hatua hadi Rais aingilie.Uhalali wa sisi kuwa kwenye nafasi tusizotimiza wajibu wetu unaotoka wapi? faida ya kusajili laini za simu ni zipi?

Wengi tumeibiwa fedha kwa kupitia laini za simu zilizosajiliwa,ukienda polisi kitengo cha cyber crime wanakwambia uhalifu huu upo juu yao hasa kwa walio nje ya Dar.Umeibiwa,unataja jina la mhusika kwenye simu iliyotumika,benki iliyopitisha uhuni huu na hakuna hatua zinazochukuliwa.Halafu wapuuzi wa taasisi husika nao wanalia eti vipi salary increament,kwa kazi ipi?
 
HABARI ZA LEO NDUGU YANGU! SASA ILE NAFASI ULIYONIOMBA YA KIJANA WAKO KUJIUNGA NA JESHI IMEPATIKANA TENA NI YA JW (TPDF) NA WALE VIJANA WAWILI ULIOSEMA NAO WAAMBIE WAJIANDAE NI ZAHARAKA NAOMBA TUWASILIANE KAMA BADO UNAHITAJI.
 
~~>>>Nimeshawahi kutumiwa Ujumbe huo mara mbili..... Mara ya kwanza nilidhani amekosea namba....

Nikamtumia ujumbe kuwa amekoaea namba hivyo aangalie vizuri .... Hakunijibu


Baada ya siku kadhaa akanitumia tena Ujumbe kama huo... Nikaona huyu ni fala tu
 
Back
Top Bottom