Nimetengeneza 15,632,000/= kwenye betting ndani ya miezi minne

Sasa hii site mbona siona Kama inatabirii..
 
Kuna watu wanafanya kazi, but mafanikio zero, mungu amekupa akili, zitumie kupata kipato..unajua uzito wa 15M
Rafiki hata zingekuwa Na uzito kiasi gani in wa muda! Kama Mungu kakupa akili gundua vitu endelevu Na kwa jamii. Sio kamari
 
Sasa hii site mbona siona Kama inatabirii..
hio site haitabiri bali ina-compare odds za bookmakers wengi ambao wanatoa odds nzuri, kumbuka ina matangazo ya book makers pia ina refer wateja wajiunge na hao bookmakers kwahio kwa kupitia kwao mteja akienda wanakula commission kila bookmakers wanapopata pesa na kila mtu anapojiunga (affiliate program)

Ila hapa point ya kuweka hii site ni kuwaonyesha jamaa kuwa arbitrage / sure bets inawezekana.., kwamba unaweka wagers kwenye matokeo yote Draw, Win, Loose na ukifanikiwa kuweka una guarantee ya kushinda no matter the case...,

ingawa practically even hii ina downsides
 
Kuna rafiki angu anapiga pesa sana kwenye zile slot machine za mchina , nataka nimuombe anifundishe
 
Hebu nieleweshe hapo kuna guarantee gani ya kupata faida??? Toa maelezo acha Ku C&P
 
Hebu nieleweshe hapo kuna guarantee gani ya kupata faida??? Toa maelezo acha Ku C&P


Mkuu mbona kila kitu nimekupa hizo odds
1.65; win kampuni coobet
4.4 draw leon na
7.80 loose leon

percentage hapo inazidi 100 % ukibet kuna profit ya Units approximately 4; Kama una tshs 100 inabidi uigawe ifuatavto:-
63 kwenye win
23 draw
13 Loose
umeelewa
 
Siwezi kuacha kubeti aisee, wala sioni haramu kama wengine wanavyosema,maisha yenyewe ni betting tosha ,mtu leo mzima lakini hujui keshokutwa kama utakufa ama vipi? Tunaishi kwa imani tu! I' m fearless at all.dah nakumbumbuka nasubiria gemu moja nivute milioni 14 na fc basel mpaka dakika ya 60+:anaongoza 1-0.taratibu naanza kuingia be forwaded showroom naangalia gari zuri la kudraive, huku dakika zinayoyoma ,kufika dakika ya 81 watu wanasawazisha na ikaenda droo mpaka mwisho.betting hatari sana.
 
Hahaaa!!
 
kwa kufikiri uku hebu nipe sababu tano kwanini NSIKUITE MBWA..
 
Hapa sijakuelewa,
Nilidhani unaweka Bookie mmoja ambae Yenisey kapewa Odds nyingi kisha unaweka na Bookie mwengine ambae Anzhi kapewa odds nyingi, au mfano wako hauko hivyo? Nachoelewa hii kitu ni almost haipo, sababu odds zote unazoziona hawa bookies hawajitungii tu, primarily ni kama zinatokea from same source, ndio maana hata kupishana kwao ni kidogo
 
hao
hao ndo wanaume ...na had sasa yupo....sio wajinga kama wew...wana bet kwa bookmakers wa asia ambako sportrader hawafiki..
na hao nimekutajia maamuma kama wewe ili uki google uwapate....na wengi huwajui mkolomije weweee
 
Uchumi hautengenezwi na Bidhaa tu, usikariri. Kwani Bureau De Changes wanauza bidhaa gani? Hizo stakes tunazobet zinafanya makampuni yanapata faida na kulipa kodi.

Pili makampuni hayo yanaajiri wafanyakazi kupitia hizo stakes tunazobet nazo. Wafanyakazi hao hulipwa mishahara ambayo huitumia kuendeshea maisha yao na familia zao.

Tatu, kupitia stakes zetu, makampuni haya huweza kupanga majengo kwa ajili ya ofisi, hulipa kodi ya majengo ambayo wenye nyumba hutumia mapato hayo kwa shughuli zingine za ki uchumi.

Nne mikeka ikiwin, nakatwa kodi sawa sawa labda na mfanyakazi anaekatwa PAYE.

Multiplier Effect ya kubet ni kubwa kuliko unavyodhani.
 
Sijasema bidhaa tu, nimesema bidhaa au huduma, ndio maana nikatolea mfano wa kibarua, mtu anaefanya kibarua ni anatoa huduma yake kwa malipo, wewe vipi wewe, maneno meeengi kumbe hata hujasoma nilichoandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…