Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Watu wa Mungu mpoo?

Mimi ni member wa JF tangu miaka ilopita nimekuja na ID tofauti ili nieleze yaliyonikuta iwe funzo na ushuhuda kwa wengine.

Niliweka post hapa mika ilopita na kwa bahati tu sijui niseme nzuri au mbaya ila Mungu ndio anajua, nikapata mwanaume ambaye tulianza mahusiano ambayo yalikuwa siriazi kidogo.

Baada ya muda tukapanga mipango ya kuanza mikakati ya kufunga ndoa. Na wakati huo huo ujauzito ukawa umeingia kwangu. Sasa tangu nilipomwambia yule mwanaume kuwa nina ujauzito aliniblock simu na namba zote mawasiliano hakuna. Hadi leo amenitelekezea ujauzito. Alichoniambia mara ya mwisho kabla hajanikimbia ni "wewe ulivyobeba ujauzito si ulijua unabeba ujauzito na sina pesa za kukutunza" kwa maana hiyo nipambane na hali yangu mwenyewe.

Kiukweli maisha kwangu yamekuwa magumu maana ujauzito umefikisha miezi saba na siwezi kufanya kazi nilokuwa nafanya hapo mwanzo. Daktari alinisahuri niachane nayo maana ni kazi ya kusimama zaidi ya masaa saba endapo nitapata wateja mfululizo.

Me nimeleta hili janga lilonipata ili tuendelee kuwa makini humu. Tusikurupukie watu sio wote ni wazuri kama tunavyodhani

Pia nimekuja kuomba kwa yeyote anayeweza kuniajiri kwa kazi yoyote ambayo sio ya kusimama muda mrefu kwa muda wa miezi hii mitatu ya mwishoni nina uhitaji wa kazi ili walao nipate pesa kwa ajili ya kujifungua maana sina msaada wowote wa kifedha wala vifaa vya kujifungulia. Sina matatizo yoyote ya afya hadi sasa yatakayonifanya nishindwe kuhuduria kwenye kazi hiyo nitakayoipata.

Kwa vigezo mimi ni mhitimu wa elimu ya kidato cha sita najua lugha ya kiswahili na kiingereza pia ninajua kutumia komputa vizuri. Naahidi kwamba atakaeniajiri hatajuta licha ya kuwa mimi ni mjamzito.

Mungu awabariki sana.
Pole sana.
Ulipata ugonjwa mbaya unaowapata wengi na ugonjwa huu hupofusha, mtu haoni, hasikii wala hajijui.

Mapenzi.

Ungerudi nyuma kidogo kumchunguza huyo bwana ,lazima ungeona dalili za utapeli.
Kuwa mvumilivu, mtoto akizaliwa, kupitia ustawi wa jamii, pima DNA yako ,mtoto na baba.
Halafu dai hela ya matunzo.
 
🀣🀣🀣🀣🀣, hii scenario umeisoma vizuri lakini mkuu, ishu ni kuwa kapuku dont care. Yaani ambaye huna direction ya maisha.

Sasa kama mtu katelekeza mimba si obvious huyo hajielewi. Au hujui damu ya mtoto inaweza mtafuna mpaka anavyoingia kaburini....

Sijawahi ona ke mjinga kama mtoa mada...

Tatizo wabongo wengi ni wapumbavu kama sehemu zao za siri....

Mfano.
Hujawahi jiuliza kwann ma mbele ma single maza wanawezeshwa na serikali kupitia sheria kali za watoto kule hamna kukimbia mimba mkuuu. Ndo maana una shauriwa ufanye hata vasectomy ukienda huko..

Sasa huku wanakojolewa hovyo mpaka na wanywa gongo unategemea nn kama sio shida juu ya shida

Tena ukute chizi maarifa ndo aliyemtia mimba au genta aiseee.

🀣🀣🀣🀣🀣🀣. Acha nicheke tu hii thread haijanigusa hata chembe na sijui kwann.
Kwa hiyo wanywa gongo hawana haki ya kuwa na watoto? Chambua maneno yako kabla hujaposti wangu. Maana comments zako zinadhihirisha yaliyojaa moyoni mwako. Maana kimtokacho mttu kinywani ndicho kilichojaa moyoni.
 
Duh mkuu kuwa na huruma huyu nae binaadamu. Kiufupi wame koseana hawa wapenzi ila huyu anahitaji msaada wa ajira ili aweze kula pamoja na kujitayarisha kuleta kiumbe chengine duniani. Unao msaada msaidie kama hauna muombe dua njema dua nayo pia sadaka. Tusiwe tuna wahukumu watu kwa makosa yao, tuwape msaada watatue shida zao.

Mleta mada kwanini hujaja na ID yako halisi? Kwasababu ID inaweza kufanya watu wakakusaidia kikweli hizi ID mpya watu wengi watapuuza au wataona tapeli tu. Pole sana
Huruma ya nini.. hawa viumbe sio wakuonea huruma wakatili na kivuli chao kujitetea ni uanamke.. always ata awe nani yang nasimama upande wa mwanaume so ww mleta mada ndo una matatizo sio mwana
 
Jitahidi kuhepa kutoa kauli batili kama hizi kwa watu wenyematatizo. usijisike fahari kuchochea maumivu kwa wengine wenye majanga.
Jitahidi kutumia akili ikuongoze na usiruhusu huruma ikuongoze, hasa kwenye huu mtandao wa fake ID.
Kwakifupi Jf member wamebadilika sana, na hauwezi kujua mkweli ni yupi na muongo ni nani.
Zamani watu walikua hawabadilishi au kuja na ID mpya kila wanapo kutana na changamoto, na hii ilisaidia walau member kutambua hata kidogo kuhusu mleta mada.
Hivi kwanza unamkumbuka Nyete...??
 
Jitahidi kutumia akili ikuongoze na usiruhusu huruma ikuongoze, hasa kwenye huu mtandao wa fake ID.
Kwakifupi Jf member wamebadilika sana, na hauwezi kujua mkweli ni yupi na muongo ni nani.
Zamani watu walikua hawabadilishi au kuja na ID mpya kila wanapo kutana na changamoto, na hii ilisaidia walau member kutambua hata kidogo kuhusu mleta mada.
Hivi kwanza unamkumbuka Nyete...??
πŸ’―πŸ’―
 
🀣🀣🀣, kaa chonjo. Wanawake walioumizwa kihisia si wazuri kwa afya yako.
Niliwahi kukutana na mmoja akaniambia kwamba yeye anatembea akiwa moyo wake unamatobo ya kutosha, lakini watu wanamuona ni mrembo tena mzima wa afya....🀣 huyu aliniambia kwamba anatembea na majeraha yake...😎
 
Jitahidi kutumia akili ikuongoze na usiruhusu huruma ikuongoze, hasa kwenye huu mtandao wa fake ID.
Kwakifupi Jf member wamebadilika sana, na hauwezi kujua mkweli ni yupi na muongo ni nani.
Zamani watu walikua hawabadilishi au kuja na ID mpya kila wanapo kutana na changamoto, na hii ilisaidia walau member kutambua hata kidogo kuhusu mleta mada.
Hivi kwanza unamkumbuka Nyete...??
Mie ndio nimesiaha muelewe mrembo, litalo nikuta na liweeeπŸ˜…πŸ˜…
 
Unajishtukia tu au ni wewe? Umejuaje umri wangu umeenda na kwenye post sijataja umri. Acha kupika taarifa mbazo hazipo wangu. Kama una connection ya kazi nisaidie otherwise nashukuru kwa mchango wako.
Hujasema Mkoa uliopo, au nao ni private?
Tuma namba inbox nikufanyie interview.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom