Nimetapeliwa pesa, naombeni ushauri

Nimetapeliwa pesa, naombeni ushauri

mzeempili

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2021
Posts
327
Reaction score
531
Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2019 nilikuwa na kazi ya miezi mitano mkoani Kigoma. Nikiwa huko nilikutana na classmate na roommate wa chuo niliyesoma naye miaka ya nyuma DIT.

Tulipiga stori za hapa na pale, tukazoeana kiasi. Akajitambulisha kuwa anafanya kazi kwenye shirika la misaada, na pia anajishughulisha na kuagiza magari. Tulivyoendelea kukutana na kuzoeana tulizidi kufahamiana. Bahati mbaya nilijikuta nimefunguka kuwa nilikuwa ninapanga kununua gari.

Tulivyokuwa tunaendelea kuonana, jamaa alianza kunionyesha mawasiliano na kampuni za kuagiza magari, na kuniaminisha kuwa tunaweza ku-save hela kama ataagiza gari yeye, kisha gari likifika atanikabidhi.

Alinishawishi kuwa nimpatie kile kiasi cha kulipia nje huko, millioni 13. Kwa kumwamini, nilimwekea kwenye akaunti yake ya benki. Nikabaki na bank slip.

Ulipofika wakati wa gari kufika, jamaa alianza hadithi. Mwanzo alidai nimpe muda atoe gari, kisha atanipatia tumalizane. Zikapita zaidi ya wiki. Baadae akasema kuna mtu amelipenda, ananunua kwa bei nzuri, tuagize lingine. Akadai amesafiri, anarudi tutaonana.

Nilipoona anazunguka kinyume na makubaliano nikampeleka polisi. Afande niliyemkuta akampigia simu, jamaa akafika, akakubali kuwa ameuza gari ananirudishia pesa yangu na nyongeza. Tukaandikishana nikatulia.

Baada ya hapo, mpaka leo imekuwa ni mwendo wa kuzungushana kila mahali, na pesa sijapata. Kila akipigiwa simu anadai amepata majanga, mara vifo, nk.

Hajalipa pesa zangu.

Naombeni ushauri namna bora ya ku-deal na mtu wa aina hii.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Makampuni yote ya kuagiza magari yaliyojaa bongo hapa leo kweli ukamuwekee 13m mtu kwenye akaunti yake binafsi akuagizie gari?
Umepigwa kizembe sana aisee, pole sana.
Rafiki yako alijua wewe mzembe mzembe ndio maana akakulia timing, kukuingiza 'kingi' na kukupiga. Umepigwa kishamba sana mkuu.
 
Muweke ndani tena, na safari asitoke mpaka akuachie hela au nyumba yake.

Vaa sura ya simba kuanzia sasa.
 
Pole mkuu. Ni wazi huyo rafiki yako Ni tapeli na acha kusikiliza hizo excuse zake. Wewe Rudi polise chonga nao Kama vipi wapooze hao Askari, akamatwe atiwe ndani asitoke.

Usitake maelezo zaidi ya pesa, kama anamali aweke dhamana zipigwe Bei upate Chako.
 
Pole mkuu. Ni wazi huyo rafiki yako Ni tapeli na acha kusikiliza hizo excuse zake. Wewe Rudi polise chonga nao Kama vipi wapooze hao Askari, akamatwe atiwe ndani asitoke.

Usitake maelezo zaidi ya pesa, kama anamali aweke dhamana zipigwe Bei upate Chako.
Asante sana kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom