Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 19,931
- 34,414
Heshima sana wanajamvi.
Nimekuwa na mazoea ya kwenda kwa Mrombo au ukipenda unaweza kupaita "Mahakama ya Mbuzi' kila mwisho wa week au siku za sikukuu za kiserekali au kidni kutafuna Mbuzi choma.
Juzi kati nimeanza kupata maumivu ya mguu wa kushoto sehemu ya kukanyagia,hali ilizidi kubadilika siku ya jumatatu ikabidi niende hospital kwaajili ya check up ndio nikaambiwa Muzee itabidi uachane na nyama choma hasa Mbuzi umepata ugonjwa wa gout dih salalehe nikaona imeshakuwa taabu kila nikifikiria Mbuzi choma alivyo mtamu na huku ugonjwa umeshanivamia hadi mwendo umebadilika nikitembea utadhani naogelea ikabidi niwe mpole nikubaliane na hali hali ambayo ni kusitisha zoezi la kwenda kwa Mrombo kul Mbuzi choma.
Ndugu,Jamaa na marafiki napenda kuwataarifu rasmi Mimi Ngongo mkaazi wa Njiro kwa Msolla nimeacha kula nyama choma (Mbuzi & Ng'ombe) kuanzia leo tarehe 24/12/2015 isipokuwa nitajikita zaidi kumtafuna Mnyama wa taifa kama nilivyoshauriwa na wataalamu wa afya (madaktari) kwamba hana madhara wala hawezi kuniletea ugonjwa wa gout.
Naomba kuwasilisha kwa mjadala wa afya si wa kidini.