Nimesitisha rasmi kuchangia harusi

Hivi kwa nini watu hupanga kufanya mambo ambayo hawana uwezo nayo na mwishowe wanaishia kuwa kero tu kwa wenzao?

Kwani hawawezi tu kufunga ndoa bila makeke kama uchumi hauruhusu?

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Mimi sijachangiwa, sitachangiwa, na nitachangia ninapojisikia.

Waswahili walisema "Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba".

Naona hata harusi inageuka msiba.

Jamii yetu inabidi ijikite katika kujutegemea zaidi. Watu waanze kujiandaa wenyewe katika gharama za harusi, kama kuchangua watu wachangie token, kwa hiyari. Sio wanafanya mchango kama kiingilio cha harusini.

Pia, harusi ya kifahari si lazima. Watu wafanye harusi kwa uwezo wao. Sio ynafanya harusi ya kujuzidi kimo kwa kujitutumua na kutegemea michango ya watu.

Watu wanne tu Mikadi Beach wanatosha kumaliza harusi.

Wengine wanaweza kuisikia kwenye gazeti.

Gharama hata laki mbiki haifiki.

Ukifanya hivyo utakuwa hujaoa?
 

This is a good example....
 
Nimeweka azimio kuwa sichangii,na niliweka kwenye status ya whatsapp nafurah nimeeleweka.
Walioniuliza nimewaambia #MagufuliEffects.
Michango ya Harus No
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha

Unacheka? Ni kweli nachosema.

Watu wanapenda sana kulazimisha mambo na kuishia kuwa kero tu.

Halafu ukikutana na jitu lililo lipumbavu hata u-reason nalo vipi wala halitakuelewa.

Sana sana litaishia kukushangaa wewe ulivyo wa ajabu kwa sababu hutaki kuchangia harusi yake.
 
Kulipia ada za shule watoto, au wagonjwa hospitalini hamna mtu anachangia. Maamuzi yako ni ya busara.
 
michango nayo ni jipu...jpm apige marufuku hamna namna...
mkiambiwa changieni madawati mnasikia hakuna pesa...harusi ya kula na kunywa siku moja uko tayari ukope ila usikose...
mimi mwenyewe nshaacha kiaina...uzuri ndugu zangu pia wako against hii makitu...hivyo ni bila bila
 
Heri yangu mimi niliyeacha huo ujinga kitambo, sio kwamba michango inakera tu, hizo ndoa zenyewe siku hizi hazidumu kabisa. Mtu unatoa mchango leo hata mwaka haushi mme/mke full kubanjuka na michepuko. Na ukiwa hujaoa michango ya harusi ni kama deci.
 
Hata mm sichangii haruc kama ww kwanza kadi huwa nakataa ya mchango wa haruc.
 
Huo ni uwoga na kukwepa maaumuzi, kwani akikataa harusi hataolewa au kuoa?
 
Mimi nilishatoka kuchangia harusi mwaka wa pili sasa,we unakuta ofcn una card kama tatu,mtaani unakoishi una card mbili,kwa ndugu pia.ndani ya mwezi unatakiwa kuchangia harusi kiwango kizima cha mshahara wa mtu,huo ujinga nishauacha siku hz,ila ukija unachangisha pesa ya kuhudumia wajane na yatima nitatoa,lakini lijamaa na mchumba wake wameamua wenyewe kuoana wanataka wanunue na friji kupitia michango yetu wakwendeee...sitaki siku hz hzo mambo
 
ukiendekeza haya mambo ni kero, juzi kuna mama kaja ana sare ya dera na mchango wa kitchen party alishaolewa miaka karibia nane sasa, walifunga ndoa bila sherehe eti leo ndiyo wanafanya harusi,
nimeona ni ujinga kuchangia vitu kama hivi.
 
. Wengi humu tunawatoto wadogo sana ngoja wakuwe wafikie kuoa na kuolewa ndio mtajua umuhimu wa kushiriki jambo hili. Na wengi wenu mmevutana hamjafunga Ndoa ndio maana mnapinga jambo hili.
Wengine hatuna mpango na harusi!
 
Duh hela yote hiyo unatoa mchango?????

Nilishaacha kitambo kuchangia....na ikitokea ni lazima sana kuchanga sizidishi 60,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…