Nimesikitishwa sana na ukosefu wa maji Monduli

Ni kweli monduli kuna shida ya maji, lakini kuna mengi ya kujifunza nyuma ya tatizo hilo.
Monduli ni kubwa na kwa bahati nzuri/mbaya wakazi wengi wa monduli ni jamii ya wafugaji/wamasai, hawa hawatulii sehemu moja kwa ajili ya kutafuta malisho, hivyo inaleta ugumu kuwapatia huduma km maji, shule, zahanati au hata miundo mbinu.
Hivyo matatizo yao ni vigumu kusaidiwa na mtu mmoja ikiwa serikali haitaweka mkono.
Najua serikali imejitahidi kwa kushirikiana na world bank wametoa maji Arusha ngaramtoni hadi monduli maarufu maji ya lowasa na pia wametoa maji meru..bangata hadi monduli.
Hivyo serikali pamoja na aliyekuwa mbunge wao walijaribu kupunguza makali.

Hizo stori zenu za kusoma kwenye historia hazina nafasi tena kwenye ulimwengu huu.
Hivyo vijiji vya wamasai vingepatikanaje kama watu hawatulii?
Zahanati na baadhi ya vituo vya afya vilijengwaje kama watu hawatulii.
Stori za wamasai kuhama zilikuwa karne ya 17,18, na 20 mwanzoni na sio karne hii.
Matatizo ya maji na ardhi Monduli yatatuliwe acheni kudanganya.
Huko ndo home hivyo usidanganye.
 
Hivi rais wa nchi hii wote waliopita hawaoni aibu suala la maji kuwa kero baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhuru?! Ajabu sana kumtaja Lowasa wakati hajwahi pewa urais wa hii nchi.
 
ndio kwa yule anayeuchukia umasikini ambaye alivuta maji ya ziwa victoria had shinyanga akawa anajisifu mi nafikiri angejisifu namna gani ameondoa tatizo hilo monduli badala ya kujifanya aonekane kiongozi mzuri
 
Hizo stori zenu za kusoma kwenye historia hazina nafasi tena kwenye ulimwengu huu.
Hivyo vijiji vya wamasai vingepatikanaje kama watu hawatulii?
Zahanati na baadhi ya vituo vya afya vilijengwaje kama watu hawatulii.
Stori za wamasai kuhama zilikuwa karne ya 17,18, na 20 mwanzoni na sio karne hii.
Matatizo ya maji na ardhi Monduli yatatuliwe acheni kudanganya.
Huko ndo home hivyo usidanganye.
Nafikiri uko gizani, funguka kidogo, sio mkazi wa monduli, cna maslahi na lowasa, wala sio mpambe wake but ukweli ulio wazi katenda makuu monduli kushinda mbunge yeyote japo changamoto bado nyingi pia
 
Mchukia umaskini kwake hoi.
 
Hapa simlengi mtu wala chama wala kupinga mawazo tofauti.
Lakini kama Mtanzania imeniuma sana kuona binadamu wenzetu wa Monduli....kuwa na shida ya maji kiasi cha kuhatarisha maisha yao......

Ref: Kipindi Channel ten cha mimi na tanzania kinachoongozwa na Hoyce temu.

Naona inatosha manake naweza kuchuma dhambi.
Sikitika na Chalinze mkuu. Msoga hawajaoga mwezi wa 8 huu. Watu wananunua ndo ya maji ya Lita 20 kwa shilingi 3,000/-, Mwenda zake alivyoona ameanza kunuka jasho akaondoka kimya kimya. Riziwani anaishi Oysterbay. Madiwani wapo wapo na wao wana-share bwawa pamoja na ng'ombe na mafisi. Ni jirani tu kwa Rais Kikwete...
 
Kuna taarifa moja ya Monduli inanishangaza au labda sikumwelewa aliyeisema. Ni Dr. Slaa siku anatangaza kujiuzulu siasa. Alidai kuna ufisadi katika mradi wa maji ambapo yalitolewa mabilioni lakini vilichimbwa visima vichache. Na mkandarasi mchina alipata shida sana kulipwa. Kuna ukweli wa taarifa hii na nani mhusika? Kuna watu wa Monduli humu watujuze kwani tatizo la maji Monduli ni wimbo maarufu, sijui kwanini?
 
Wewe unaongelea kukosa maji monduli! Njoo uone shida ya maji mza. Watu wanaishi mita 100 kutoka ziwani ila hwajui swala la maji ya bomba.
 
Hali imekuwa mbaya kwa sababu pameoneshwa au?mbona kuna mitaa hali inatisha zaidi na hapaoneshwi na watu wapo kimya tu?Wewe una nia nyingine
 
Nafikiri uko gizani, funguka kidogo, sio mkazi wa monduli, cna maslahi na lowasa, wala sio mpambe wake but ukweli ulio wazi katenda makuu monduli kushinda mbunge yeyote japo changamoto bado nyingi pia

Hakuna aliyepinga baadhi ya maendeleo aliyoyafanya lowassa Monduli,na hiyo haikuwa hoja kwangu,hoja yangu ilikuwa kushindwa kuleta ,maendeleo kwa wamasai kisa kuhamahama,
Nikakuambia ishu ya kuhamahama ni historia ya zamani na haipo kwenye karne hizi.
Kama kuna mwanasiasa ama mtaalam anayesema alishindwa kupeleka kituo cha afya mti mmoja ama Nanja kwa kuwa watu wanahamahama basi atakuwa hamnazo.
Atafute sababu nyingine na sio hiyo.
 
Back
Top Bottom