Kabla ya kujikita sana inabidi tuende kwenye kuweka kanuni za mwanzo na definitions kwanza.
Mtu anaposema "maajabu" katika habari hii anamaanisha nini?
Maana mwingine anaweza kukwambia "ni maajabu mimi kukubaliwa na msichana yule". Au "ni maajabu mimi kupata mkopo benki".
Sasa mimi nataka kujua maajabu ni nini?
Tunaongelea maajabu kwa maana ya kanuni zinazojulikana za sayansi kupinda kama vile tunavyosoma Musa alivyopasua bahari na kupitisha wana Wa Isaraeli?
Au maajabu ya mtu kufunga goli la tikitaka mita kumi kutoka langoni?
Kabla ya kujibu sana inabidi tukubaliane maajabu ni nini.
Maana mwingine anaweza kusema kwamba mvua kunyesha Okavango ni jambo la ajabu, wakati karibu kila mwaka inanyehsa, japo hata kama ni mara moja kwa mwaka.