Nimeshuhudia muujiza wa ajabu nchini Germany!

Nimeshuhudia muujiza wa ajabu nchini Germany!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,362
Reaction score
29,374
Wana JF, hivi karibuni nikiwa katika matembezi katika mitaa ya jiji la Frankfurt nchini Germany, nimekutana na muujiza ambao hadi leo nashindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kinatendeka. Niliwakuta watu wawili wa asili ya kiarabu wakiwa wamebebana kwa njia ya ajabu kama inavyoonekana katika picha. Walikuwa wamekaa hivyo kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili ya kuchoka au kutumia nguvu. Niliweza kuhakikisha wote wawili walikuwa ni bnadamu hai na sio picha wala sanamu. Walifanya hivi ili kujipatia chochote toka kwa watu.

Kuna mtu anaelewa hili?
 

Attachments

  • Muujiza 1.JPG
    Muujiza 1.JPG
    120.9 KB · Views: 4,382
  • Muujiza2.JPG
    Muujiza2.JPG
    127.3 KB · Views: 1,171
  • Muujiza3.JPG
    Muujiza3.JPG
    113.2 KB · Views: 1,255
  • Muujiza4.JPG
    Muujiza4.JPG
    101.3 KB · Views: 5,219
Mhhh mi,eangalia pic mimeshindwa kuelewa kwa kweli......ni ajambu naweza sema
 
hakuna maajabu , kuna chuma kigumu mithili ya nondo, kimekunjwa kwa weledi kikitokea chini alipokaa jamaa kikipitia kwenye manguoa yao kufuata mkono , na kisha hiko chuma ndio kilichooundwa mithili ya kiti ambayo jamaa wa juu kakalia.

balance ya mtu mwa juu inategemea zuzo wa mtu wa chini ambae pia amekaa kwenye kitu kilichoundwa mithili ya stand za kuwekea maua.
hata mie naweza....kumbe naweza kula vichwa vya waTz nikirudi
 
Usiziamini kila roho, inafika kipindi inatakiwa tuzijaribu
 
mzizimkavu idara yako hii.njoo ututoe gizani mkuu.
 
Mhhh mi,eangalia pic mimeshindwa kuelewa kwa kweli......ni ajambu naweza sema

Wasingevaa nguo za kucover mwili mzima ningeamini.

Jiulize kwanini huyo wa juu kavaa gloves pia wakati aliye chini hajavaa? anaficha nini? kwenye mashati yao mikononi kumetuna sivyo kawaida, kunasupport gani ya ziada?
 
hii mbona cha mtoto kuna jamaaa mtoni kwa azizi ally nilimkuta kakakaa juu ya mkuki akiwa mtupu wallahi tena.aisee
 
Last edited by a moderator:
Mh...! Ngoja niondoke hapa,naumiza kichwa bure...! Ngoja niingie jukwaa langu pendwa la uchumi na biashara.
 
hawa Roms bwana wanajua kuombaomba,mara wapige sijui piano kwenye Metro
 
Huyu mtu kajipaka rangi mpaka usoni na anasimama muda wote.
Wien_Shloss.jpg
Hela zinatafutwa jamani kwa kila njia, lakini ni bora maana hawaibi.
 
Hawa wanatumia mapepo hasa aina ya majini kuwabeba wakae hivyo kwa muda mrefu. Ingia kwenye You Tube utakutana na mtu ananyofoa kichwa chake ama kiuno anatembea nacho huku akiwa nusu! hayo ni mapepo tu!
 
Back
Top Bottom